Home About Articles Ask the Sheikh
Sheria

Jibu la Swali: Jinsi ya Kuwatendea Wasio Waislamu katika Masuala ya Chakula na Mavazi Kulingana na Dini Zao

August 18, 2014
4445

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya watembeleaji wa ukurasa wake wa Facebook "Fiqhi")

Kwa Adnan Khan

Swali:

Salaams Sheikh

My question is on an article in the Constitution. In article 7, clause 4 or clause D from the English translation of the second edition 2010, it is stated: The non-Muslims will be treated in matters related to foodstuffs and clothing according to their faith and within the scope of what the Shari'ah rules permit. My question is related to clothing.

Will Non-Muslim women be allowed to wear any clothing as long as it covers the bodies and is modest, such as long dresses or trousers and a shirt? Or will they be required to wear Khimar and Jilbaab like the Muslim women?

How was the non-Muslim women's dress was dealt with throughout Islamic history? i.e. were they allowed ot wear what they wanted or was the Islamic dress enforced upon them.

May allah reward you

From your Brother Adnan from the UK

Tafsiri ya Swali:

Swali langu linahusu kipengele katika mswada wa Katiba, nacho ni Ibara ya 7, kipengele cha 4 au "d", kutoka katika tafsiri ya Kiingereza ya mwaka 2010: (d - Wasio Waislamu watatendewa katika masuala ya chakula na mavazi kulingana na dini zao ndani ya kile kinachoruhusiwa na hukmu za kisharia.) Swali langu ni kuhusu mavazi; je, wanawake wasio Waislamu wanaruhusiwa kuvaa vazi lolote mradi tu lisiwe na mshiko mwilini na lisiwe la kuvutia macho, kama vile rida ndefu au suruali na shati, au wanatakiwa kuvaa Khimar na Jilbab kama wanawake wa Kiislamu? Na je, vazi la wanawake wasio Waislamu lilishughulikiwa vipi katika historia yote ya Kiislamu? Je, waliruhusiwa kuvaa watakacho au walilazimishwa kuvaa vazi la Kiislamu?

Namuomba Mwenyezi Mungu akulipe kheri,

Ndugu yako Adnan kutoka Uingereza.

Jibu:

Walaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.

Kipengele "d" kutoka katika Ibara iliyotajwa hapo juu ulichoulizia, matini yake ni hii: "Wasio Waislamu watatendewa katika masuala ya chakula na mavazi kulingana na dini zao ndani ya kile kinachoruhusiwa na hukmu za kisharia." Nawe unauliza kuhusu mavazi, na jibu ni kama ifuatavyo:

Kipengele hicho kilichotajwa hapo juu kimeainisha masharti mawili kwa ajili ya mavazi:

Sharti la kwanza: "Kulingana na dini zao." Wanaruhusiwa kuvaa mavazi kulingana na dini zao, na mavazi kulingana na dini zao ni yale yanayovaliwa na viongozi wao wa kidini (wanaume na wanawake), yaani mavazi ya mapadri, watawa wa kiume... na kadhalika, pamoja na mavazi ya watawa wa kike. Haya ndiyo mavazi yaliyowekwa katika dini zao, hivyo inajuzu kwa wanaume na wanawake wao kuvaa mavazi haya; hili ni kuhusiana na sharti la kwanza.

Ama sharti la pili "ndani ya kile kinachoruhusiwa na hukmu za kisharia", nazo ni hukmu za maisha ya hadhara ambazo zinawahusu raia wote, Waislamu na wasio Waislamu, kwa wanaume na wanawake.

  • Isipokuwa ni kwa mavazi kulingana na dini zao pekee.
  • Ama mavazi mengine yasiyo ya kidini, yanafanyiwa kazi na hukmu za kisharia katika maisha ya hadhara. Na hii ni kwa wanaume na wanawake.

Vazi hili limefafanuliwa kwa ukamilifu katika Nidhamu ya Kijamii, na linatumika kwa raia wote, Waislamu na wasio Waislamu. Hakuna anayesamehewa miongoni mwa wasio Waislamu isipokuwa mavazi kulingana na dini zao kama tulivyotaja hapo juu. Ama kinyume na hivyo, ni lazima kusitiri aura na kutofanya tabarruj, pamoja na kuvaa Jilbab na Khimar. Na kwa sababu suruali ni miongoni mwa tabarruj, haijuzu kwa mwanamke kuivaa katika maisha ya hadhara, hata kama inasitiri mwili.

Kuhusu hali halisi ya kihistoria, katika kipindi chote cha utawala wa Khilafah, wanawake (Waislamu au wasio Waislamu) walikuwa wakivaa Jilbab, yaani vazi pana juu ya nguo zao za ndani, na walikuwa wakifunika vichwa vyao. Kulikuwa na baadhi ya vijiji ambavyo vilikuwa na wanawake wa Kiislamu na wasio Waislamu ambapo mavazi yao hayakuwa na tofauti... Hata baada ya kuvunjwa kwa Khilafah, athari za jambo hilo zilibaki kwa kiasi fulani. Lau ungewauliza wazee wenye umri wa zaidi ya miaka sabini au themanini, wangekuambia kuhusu walichokiona katika baadhi ya vijiji vya Palestina; jinsi walivyokuwa wakiwaona wanawake wa Kikristo na wa Kiislamu wakiwa katika mavazi yanayofanana katika vijiji hivyo.

Natumai jibu hili linatosheleza swali lako.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network