Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Maana ya "Uwezo" katika Masharti ya Kusimama kwa Khilafah

November 20, 2014
4280

(Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook "Fikri")

Kwa Ntham Rd

Swali:

Bismillahir Rahmanir Rahim, Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Nina swali: Imekuja katika kitabu cha Ash-Shakhsiyyah al-Islamiyyah Juzuu ya Pili, uk. 33, kipengele cha saba cha masharti ya Khalifah ni "Uwezo" (al-Qudrah), kisha kikaendelea kufafanua uwezo huo mpaka kufikia kauli ifuatayo: (Vilevile si sharti kwa ajili ya kusimama kwa Khilafah kwa Khalifah kuwa jasiri, au miongoni mwa watu wenye maoni yanayopelekea kwenye siasa ya raia na kusimamia maslahi). Swali langu ni: Je, hayo siyo sehemu ya uwezo?

Jibu:

Wa Alaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.

Kilichokuja katika kitabu ni: (Vilevile si sharti kwa ajili ya kusimama kwa Khilafah kwa Khalifah kuwa jasiri, au miongoni mwa watu wenye maoni yanayopelekea kwenye siasa ya raia na kusimamia maslahi, kwa sababu hakuna Hadithi sahihi iliyokuja kuhusu hilo, na wala haingii chini ya hukumu ya kisheria inayoifanya hiyo kuwa sharti la kusimama (shart in'iqad), ingawa ni bora zaidi kuwa jasiri, mwenye maoni na busara) mwisho wa nukuu. Kama unavyojua, sharti la kusimama (shart in'iqad) linamaanisha kuwa ikiwa Ummah utamchagua Khalifah ambaye hatimizi masharti ya kusimama, basi Khilafah yake ni batili... Kwa kuyazingatia mambo haya mawili uliyoyataja, inabainika kuwa hayo si miongoni mwa masharti ya kusimama, kwa maana kwamba ikiwa Ummah utamchagua Khalifah asiyetimiza sifa hizo, Khilafah yake haibatiliki kwa sababu dalili za kisheria hazionyeshi hivyo. Lakini hayo ni miongoni mwa masharti ya ubora (shurut al-afdhaliyyah), yaani ni bora kwa Ummah kuzingatia masharti haya mawili wakati wa kumchagua Khalifah, hivyo ujitahidi kumchagua yule ambaye anatimiza masharti ya kusimama na idadi kubwa zaidi ya masharti ya ubora; kwani hilo ni bora na madhubuti zaidi.

Ama uwezo (al-Qudrah), hiyo ni miongoni mwa masharti ya kusimama (shurut al-in'iqad), na inamaanisha kuwa Khalifah awe na uwezo wa kutekeleza majukumu mazito ya Khilafah, bila kuuwekea uwezo huo mipaka ya kitu maalum. Hivyo, kila kitu kinachoathiri uwezo wa kutekeleza majukumu ya Khilafah athari inayovuruga utendaji, kinachukuliwa kuwa ni chenye kuvunja sharti la uwezo. Hii ni kwa sababu kazi ya Khalifah ni kutekeleza hukumu za Sharia, na jambo hili linahitaji uwezo wa kusimamia mambo yeye mwenyewe au kufuatilia mambo yeye mwenyewe ikiwa atamteua mwingine kuyatekeleza. Ikiwa hana uwezo wa kufanya hivyo, basi hawezi kutimiza mkataba wa Khilafah uliowekwa kwa nafsi yake kwa ajili ya kutekeleza hukumu za Sharia. Inatosha katika hilo kutimia kwa masharti ya kusimama, na miongoni mwayo ni uwezo; ikiwa uwezo huo utatoweka, basi mkataba wa Khilafah hautaendelea kuwa sahihi. Mfano ni ikiwa Khalifah atapatwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, au kuingia katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa muda mrefu, au maradhi mengineyo ambapo ugonjwa huo unaendelea naye kwa muda mrefu unaoathiri usalama wa utawala katika Dola, kiasi kwamba Khalifah hawezi tena kusimamia mambo yeye mwenyewe au kufuatilia mambo yeye mwenyewe ikiwa atamteua mwingine kuyafanya... Na Mahakama ya Malalamiko (Mahkamah al-Mazhalim) ndiyo inayohusika na kuchukua hatua za kuthibitisha kutokuwepo kwa uwezo huo, na kisha kutoa uamuzi unaohitajika kutangaza kuwa nafasi ya Khilafah iko wazi...

Ama kutokutimia kwa masharti ya ubora, hakubatilishi mkataba wa Khilafah. Hivyo, kuwa jasiri anayemudu mbinu za hali ya juu za kivita, au kuwa miongoni mwa watu wenye maoni waliopata elimu katika vyuo vikuu vya juu kabisa... yote haya si sharti la kusimama, hivyo hayabatilishi mkataba wa Khilafah, kwa sababu hakuna dalili ya kisheria juu ya hilo, na kwa sababu masharti kama haya hayaathiri utekelezaji wa majukumu ya Khilafah athari inayovuruga utendaji. Kwani Khalifah, ikiwa jambo litahitaji ushujaa unaofaa katika baadhi ya mambo kama vile vita kwa mfano, anaweza kutafuta msaada kwa baadhi ya watu wenye ushujaa katika jambo hilo. Vilevile ikiwa jambo litahitaji maoni ya wenye masomo ya juu ya vyuo vikuu, basi Khalifah anaweza kurejea kwa watu kama hao miongoni mwa raia wake. Pamoja na hayo, kama tulivyosema awali, ni bora zaidi kwa Ummah kumchagua Khalifah anayemiliki masharti ya kusimama na masharti ya ubora. Lakini ikiwa Ummah utamchagua mwenye masharti ya kusimama pekee na asimiliki masharti yote ya ubora, basi Khilafah yake ni sahihi madamu ametimiza masharti ya kusimama, kwani dalili sahihi za kisheria zinafahamisha hilo.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus

Share Article

Share this article with your network