Swali:
Kutokana na kuangalia mwendo wa matukio, ukweli wa mambo umeingiliana na kutatanisha mbele yangu:
1- Tunajua kwamba ushawishi halisi nchini Misri ni wa Marekani, hivyo basi, ni vipi Saudi Arabia, Imarati na Kuwait zinaunga mkono kifedha utawala mpya nchini Misri, ilhali nchi hizi ni wafuasi wa Uingereza?
2- Isitoshe, Imarati iliunga mkono Ufaransa nchini Mali na ikatuma msaada wa kifedha kwa Mali, licha ya kuwa ushawishi halisi nchini Mali si wa Uingereza?
3- Vilevile, tunaona utofauti katika misimamo ya vyombo vya habari kati ya chaneli ya Al-Arabiya nchini Imarati, na chaneli ya Al-Jazeera nchini Qatar, licha ya kuwa Imarati na Qatar ni mawakala wa Waingereza. Na je, mabadiliko ya hivi karibuni nchini Qatar yanaathiri sera ya Uingereza huko?
4- Kisha tunaona kana kwamba watu wa Saudi Arabia katika muungano wa upinzani (Coalition) kama vile Al-Jarba wana jukumu la dhati tofauti na watu wa Qatar, je, udhaifu umeanza kupenya kwa watu wa Qatar katika matukio yanayoendelea nchini Syria na kwamba watu wa Saudi Arabia wamepata nguvu?
5- Mwishowe, je, kuachwa kwa Morsi na Marekani kunamaanisha kuwa imeachana na wazo la kurahisisha kuingia madarakani kwa kile inachokiita "Uislamu wa wastani"?
Ninaomba "univumilie" katika swali hili kwa urefu wake na Mwenyezi Mungu akulipe kheri. Naomba radhi mapema kwa urefu na wingi wake, lakini tunajua upana wa kifua cha Amir wetu pamoja na upana wa elimu yake, labda tutapata kwake kile kitakachoondoa mkanganyiko wetu na kutuliza vifua vyetu.
Jibu:
Hili, ndugu yangu, si swali moja bali ni "rundo" la maswali!! Kwa vyovyote vile, hili hapa ndilo jibu kwa muhtasari bila kuathiri maana, Insha Allah:
Kuna misingi mikuu kuhusiana na sera ya Uingereza inayokusaidia kuelewa kinachoendelea:
1- Uingereza kwa sasa haina uthubutu wa kusimama dhidi ya Marekani waziwazi, bali huonekana kana kwamba iko upande wake, lakini hufanya vurugu na kukwamisha sera za Marekani kwa siri na kupitia mawakala wake baada ya kuandaa mipango madhubuti ili ionekane kwa sura ya udanganyifu...
2- Mengi ya majukumu ambayo Uingereza huwapa mawakala wake ni kuonekana kama yeye, kana kwamba wako katika mwelekeo uleule ambao Marekani inaelekea bila kugongana nayo. Kwa mfano, uhusiano wa Jordan na Marekani kwa mtu asiye na upeo wa kisiasa anaweza kudhani kuwa iko upande wa Marekani, ilhali ni nguzo imara ya Uingereza. Ndivyo ilivyo kwa Imarati na mawakala wengine... Isipokuwa kwamba Uingereza huwaacha baadhi ya mawakala wake wasimame dhidi ya Marekani kama vile Qatar, na hili ni jukumu tofauti na baadhi ya mawakala wengine na kadhalika... Yaani, mawakala wake wana majukumu tofauti: wengi wao huitabasamu Marekani na kuonyesha urafiki huku wakiisumbua kwa nyuma ya pazia kama inavyofanya Uingereza, bosi wa mawakala hawa, na wachache wao jukumu lao husababisha usumbufu kwa Marekani kwa njia ya wazi zaidi...
3- Uingereza inashirikiana na Ufaransa katika kukabiliana na sera za Marekani, na hiyo ni ndani ya sera ya Ulaya, hususan Uingereza na Ufaransa. Tofauti ni kwamba Uingereza hufanya mambo kwa ujanja na hila na kwa sauti laini ya kudanganya kuelekea Marekani, huku Ufaransa ikifanya mambo kwa sauti ya juu na kelele... Mara nyingi Uingereza hutekeleza sera yake nyuma ya Ufaransa! Methali maarufu inasema "Uingereza hupigana mpaka askari wa mwisho wa Kifaransa" hata kama hili lilikuwa zamani, lakini athari yake bado ipo ingawa kwa kiwango kidogo.
4- Utawala nchini Saudi Arabia, ingawa unaongozwa na Mfalme Abdullah ambaye ni mfuasi wa Uingereza, lakini Marekani ina ushawishi kwa baadhi ya wanamfalme wengine, na ushawishi huu unaifanya sera yake kuwa na nafasi...
Kutokana na hayo, jibu la maswali yako linaweza kuwa wazi:
a- Kuhusu Qatar, Amir wa zamani wa Qatar na Waziri wake wa Mambo ya Nje waliweza kuifanya Qatar kuwa kituo kikuu cha Uingereza katika Ghuba, na akaanza kuingilia kati katika nchi kadhaa kwa njia mbili zenye athari: vyombo vya habari (Al-Jazeera), na fedha (mafuta)... Hatua zake zilikuwa na athari katika kusumbua sera ya Marekani nchini Syria, Palestina, na hata Misri na kwingineko... Na kutoridhika kwa Marekani hakukuwa siri kwa Uingereza. Na kwa sababu Uingereza hujaribu kuonekana katika picha bila kuisumbua Marekani, ilikubali kumbadilisha Amir huyo, lakini si kwa kumweka mtu aliye mbali naye, bali mbadala wake alikuwa mwanawe. Yaani sera ya Uingereza haijabadilika, lakini mtoto huyu anahitaji muda ili awe na ushawishi kama babake katika kuisumbua Marekani. Hivyo, Uingereza ilituliza kutoridhika kwa Marekani kwa njia hiyo... Yaani kilichofanyika ni mbinu ya Uingereza ya kuiridhisha Marekani kijuujuu tu bila kubadili msingi!
b- Jukumu la Qatar limepungua kidogo na mabadiliko haya kwa sababu watu wa utawala mpya wana uzoefu mdogo katika kazi za kisiasa zenye athari kuliko watu wa utawala uliopita. Lakini Qatar bado iko ndani ya sera ya Uingereza, ikifanya kazi kwa ujanja na hila, isipokuwa kwa jukumu ambalo ufanisi wake wa wazi ni mdogo kuliko jukumu la awali. Hivyo basi, watu wake nchini Syria ufanisi wao umekuwa mdogo kuliko hapo awali.
c- Ama watu wa Saudi Arabia, wao wana ufanisi zaidi na wanakubalika zaidi na Marekani na Uingereza kwa sababu Mfalme utii wake ni kwa Uingereza na kwa sababu Marekani inafanya kazi kwa bidii na baadhi ya wanamfalme katika familia ya kifalme.
Ama Al-Jarba, ingawa yuko karibu na Saudi Arabia, lakini yuko ndani ya sera ya Marekani, na hawezi kutoka nje ya utii wa Marekani hata iweje msaada wa Saudi Arabia kwake. Kwani muungano (Coalition) kwa ujumla wake ni bidhaa ya Marekani, na hawezi kuendelea katika urais wake isipokuwa yule aliye mnyenyekevu kwa Marekani.
d- Ama kuhusu Mali, na misaada ya kifedha ya Imarati... unajua kuwa Marekani ndiyo ilikuwa nyuma ya mabadiliko ya kwanza nchini Mali yaliyotokea tarehe 22/03/2012, na lilikuwa pigo chungu kwa Ufaransa. Ufaransa imefanya kazi kwa bidii kurejesha ushawishi wake. Na Uingereza inatambua kuwa haina ushawishi nchini Mali bali ni wa Ufaransa, na Marekani inashindana nayo. Hivyo, Uingereza huisaidia Ufaransa ikiwa mgogoro umezama kati ya Marekani na Ufaransa, na misaada ya kifedha ya Imarati kwa utawala wa Mali unaoiunga mkono Ufaransa inaenda sambamba na msaada wa Uingereza kwa Ufaransa.
e- Ama tafsiri ya msimamo wa Uingereza kuhusu yaliyotokea Misri kuanzia ziara za ujumbe wa Imarati na Mfalme wa Jordan, na msaada wa kifedha kutoka kwa mawakala wa Uingereza kwenda Misri, haitoki nje ya misingi mikuu iliyotajwa hapo juu... Ama mkanganyiko unaotokana na tofauti ya jukumu la Imarati na jukumu la Qatar, ni mgawanyo wa majukumu kulingana na sera ya Uingereza. Huyu anajisogeza karibu na yule anajitenga akisubiri matokeo ya matukio ya Misri... Na Imarati kuwahifadhi watu wa utawala wa Mubarak pia haitoki nje ya misingi mikuu, kwani kutarajia kurejea kwa watu wa Mubarak upya itakuwa ni mlango, hata kama ni mwembamba, kwa sera ya Uingereza kupitia Imarati, hata kama ni kwa ajili ya kurudisha fadhila!
f- Ama kuhusu swali ikiwa Marekani kuachana na Morsi kunamaanisha kuwa imeachana na kurahisisha kurejea kwa watu wanaoitwa "Waislamu wa wastani" madarakani, suala si kuachana au kutokuachana, bali ni kufanikisha utulivu wa ushawishi wa Marekani nchini Misri. Ushawishi wa Marekani nchini Misri umekita mizizi katika tabaka kubwa la kisiasa tangu miongo kadhaa iliyopita. Marekani inajali kuwa Misri iendelee kuwa kituo cha utulivu kwa ushawishi wa Marekani, na utulivu unaokusudiwa hapa si kwa ajili ya maslahi ya Misri, bali ili Marekani iweze kuifanya Misri kuwa kituo salama cha ushawishi na miradi yake... Wakati harakati za wananchi zilipoishangaza tarehe 25/01/2011, na Mubarak akashindwa kudhibiti harakati hizi na kurejesha utulivu ili Misri iwe mazingira yanayofaa kwa kuendelea kufanikisha maslahi ya Marekani, ilipomwona hivyo ilimtupa kando, na kupanda wimbi la harakati za wananchi. Kisha ikamleta Morsi baada ya kumhakikishia utekelezaji wa miradi yake, hususan mkataba wa Camp David na vyombo vya Kiyahudi, na kisha ikamuunga mkono... Iilitaraji kuwa atafanikisha utulivu kwa kuzingatia kuwa Ikhwan ndio chama cha Rais na chama kikubwa zaidi kilichopangwa vizuri baada ya kufutwa kwa Chama cha Kitaifa (National Party). Ilitarajia kuwa watafanya kazi ya kutuliza hali kama alivyofanya Chama cha Kitaifa na Rais aliyeondolewa... Lakini Morsi hakuweza, hivyo ikamwacha... Nayo ikawa nyuma ya utawala mpya wa tarehe 03/07/2013 na kuuunga mkono...
Hivyo basi, Marekani kuachana na wenye "Uislamu wa wastani" nchini Misri kulikuwa ni kwa sababu iliyo nje ya sera ya Marekani ya miaka ya hivi karibuni ya kurahisisha kuingia madarakani kwa wale wanaoitwa "Waislamu wa wastani". Marekani ilichukua sera hii ili kuua ndege wawili kwa jiwe moja kama isemavyo:
Kwanza: Kudanganya umma wa Waislamu wanaotarajia utawala wa Kiislamu... Kwani pamoja na kwamba "Waislamu wa wastani" wanatangaza demokrasia na jamhuri na kuapa kwayo! Lakini kuitwa kwao "Waislamu" kunachezea hisia za umma wa Waislamu na hivyo kudhani kuwa kuingia kwa Waislamu hawa kutaingiza Uislamu madarakani, na hivyo azma zao za kufanya kazi sahihi ya kusimamisha utawala wa Kiislamu, yaani mfumo wa Khilafah, kufifia... Na kufifisha azma za Waislamu katika kufanya kazi ya Khilafah ndicho Marekani inachokitaka, kwani Khilafah inaivuruga usingizi wake...
Pili: Kutoa utulivu kwa ushawishi wake kwa kuwatumia Waislamu kupitia hisia za watu... Lakini wasipoweza kutoa utulivu kwa ushawishi wa Marekani, yeye huwaacha, kama alivyofanya kwa Morsi, na kuwaunga mkono wengine, hasa kwa kuwa haina uhaba wa wanasiasa mawakala wake ambao imewatayarisha nchini Misri katika kipindi hicho kirefu!
g- Ni lazima kwa watu wa Kinanah (Misri) kutambua jambo hili, na kwamba Marekani bado ndiyo yenye ushawishi halisi katika enzi ya Mubarak aliyeondolewa, na katika enzi ya Morsi aliyeondolewa, na katika enzi ya utawala wa sasa. Yeye ndiye chimbuko la ugonjwa na chanzo cha balaa. Ni wajibu kwa kila Muislamu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kufanya kazi kwa bidii na juhudi ya kung'oa ushawishi wa Marekani na kuwaondoa mawakala wake, na kurejesha utawala wa Kiislamu, Khilafah ya Rashidah, katika ardhi ya Kinanah ili irejee kuwa kituo cha nchi za Kiislamu. Itawaangamiza maadui wa Uislamu na Waislamu, na kukiangamiza chombo cha Kiyahudi, na kuirejesha Ardhi Takatifu kwa Uislamu na Waislamu kama ilivyofanya katika kuwaangamiza Wanamsalaba na Watatari, na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu.