Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Madhara ya Uturuki Kuiangusha Ndege ya Urusi!

November 26, 2015
4060

Jibu la Swali

Swali:

Swali langu ni kuhusu madhara ya kuiangusha ndege ya Urusi: Je, jambo hilo litasababisha kuongezeka kwa operesheni za jeshi la anga katika anga ya Syria? Na je, hilo litaenea hadi katika anga ya Uturuki? Shukrani.

Jibu:

1- Kuhusu anga ya Syria:

  • Ikiwa makusudio ya kuongezeka kwa operesheni ni ndege za kivita kuzunguka anga ya Syria na kushambulia ardhi yake pamoja na watu, miti, na mawe, basi hilo tayari linafanyika na ndege hizo hazijaacha jitihada yoyote katika hilo...

  • Na ikiwa makusudio ya kuongezeka huko ni ndege hizi kupigana zenyewe kwa zenyewe na kuingia katika vita vya anga, basi hili ni jambo lisilotarajiwa, angalau katika muda wa karibu unaoonekana, kutokana na sababu tulizozitaja katika toleo letu la tarehe 11/10/2015 na jibu la swali la tarehe 18/11/2015.

2- Kuhusu kuenea kwa mivutano hadi katika anga ya Uturuki, kana kwamba unakusudia kuibuka kwa vita vya anga kati ya Urusi na Uturuki ambapo ndege za Urusi zingeziashambulia ndege za Uturuki kama radiamali ya kuangushwa kwa ndege ya Urusi... Ikiwa hili ndilo makusudio, basi jibu ni kwamba hili pia halitarajiwi, angalau katika muda wa karibu unaoonekana, kwa sababu zifuatazo:

  • Kuingilia kati kwa Urusi nchini Syria kulifanyika kwa makubaliano na Marekani, na utawala wa kisiasa wa sasa wa Uturuki ni miongoni mwa wafuasi wa Marekani, na hivyo hauwezi kukiuka makubaliano yaliyofanywa na Marekani...

  • Ushahidi wa makubaliano hayo uko wazi na tuliufafanua katika toleo na jibu la swali lililotajwa hapo juu... Na huyu hapa Putin anafichua hilo akisema huko Sochi siku ya Jumanne, Novemba 24, akielezea tukio la kuangushwa kwa ndege hiyo kuwa ni "choma kisu mgongoni" (Radio Sawa 24/11/2015). Hii ina maana kwamba kulikuwa na makubaliano yaliyofanyika na yakakiukwa...

  • Inavyoelekea ni kwamba kuiangusha ndege hiyo kulifanyika bila uamuzi kutoka kwa uongozi wa kisiasa wa Uturuki, bali kutoka kwa viongozi jeshini wenye malengo ya kisiasa yanayotofautiana na Erdogan, kisha ikachanganyika na ghera kutokana na yale wanayoyaona ya mashambulizi ya Urusi dhidi ya ndugu zao wa Turkmen kwenye mipaka yao...

Na hili ndilo lililoonekana nyuma ya maneno, na hata waziwazi, katika tamko la Waziri Mkuu wa Uturuki: "Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoğlu, alieleza kwa upande wake kwamba uamuzi wa majeshi ya Uturuki kuiangusha ndege ya Urusi ulitokana na nia ya kulinda mipaka..." (Radio Sawa 24/11/2015).

  • Urusi inaelekea kutambua kuwa serikali ya Uturuki haikuvunja makubaliano, kwani hii si mara ya kwanza kwa ndege za Urusi kukiuka mipaka ya Uturuki na serikali ya Uturuki haikuizuia. Utambuzi wa Urusi kuwa kuangushwa kwa ndege hiyo si uamuzi wa kisiasa wa serikali bali ni kutoka kwa baadhi ya viongozi wa jeshi unaleta uwezekano wa kudhibiti hali hiyo, na hivyo kuepusha vita kati ya Urusi na Uturuki... Kinachotarajiwa ni kwamba mambo yatatuliwa kwa njia za kisiasa ambazo zitahifadhi heshima ya pande zote, iwe kupitia mahusiano ya kibiashara, kidiplomasia, upatanishi, au Urusi kuimarisha mashambulizi katika maeneo ambayo ndege hiyo iliangushwa au mfano wa hayo kama njia ya kurejesha heshima... Marekani inaweza kuwa na dori kuu katika hilo, hasa katika suala la kudhibiti jeshi...

Pamoja na kutafuta mianya ya kutoa tafsiri ya wapi na vipi ndege hiyo iliangushwa ili kuridhisha pande zote mbili. Afisa mmoja wa Marekani alisema jana 24/11/2015: "Washington inaamini kuwa ndege hiyo ilipigwa ndani ya anga ya Syria baada ya kuingia kwa muda mfupi katika anga ya Uturuki, kulingana na tathmini iliyozingatia ufuatiliaji wa joto la ndege hiyo." (Deutsche Welle 25/11/2015). Hapa inajaribu kuridhisha pande zote mbili!

  • Kama tulivyotaja katika jibu letu "angalau katika muda wa karibu unaoonekana", yaani kulingana na data zilizopo. Vinginevyo, kuingiliana kwa operesheni za kijeshi na hatua za kisiasa hufanya uwezekano wa mabadiliko ya ghafla katika matukio na matokeo yake kuwa jambo linalowezekana...

  • Mwisho, ni jambo la kusikitisha kwamba licha ya nchi hizi kuwa za Kiislamu, matokeo na matukio ndani yake yanadhibitiwa na makafiri wakoloni na vibaraka wao! Pamoja na hayo, siku hubadilika na hautapita muda mrefu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, mpaka nuru ya Khilafah itakapomulika katika nchi za Kiislamu, na hata kuenea katika kila pembe ya dunia, na maadui wa Uislamu watarudi makwao kwa unyonge... Ikiwa watabakiwa na makao.

وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ

"Na hakika mtajua habari zake baada ya muda kupita." (QS Sad [38]: 88).

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amiri

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network