Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

JIBU LA SWALI: BABA WA MUME NI KAFIRI

July 28, 2004
2837

Swali:

Mwanamke Muislamu aliyeolewa na mwanamume Muislamu ambaye baba yake ni kafiri; je, baba wa mume ambaye ni kafiri anachukuliwa kuwa ni mahram kwa mwanamke huyu? Na je, inajuzu kwake kuonyesha mbele yake katika awrah yake kile ambacho mwanamke huonyesha kwa baba wa mume wake aliye Muislamu?

Jibu:

Baba wa mume ni miongoni mwa mahram, iwe ni Muislamu au si Muislamu. Kwani aya:

أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ

“...au baba wa waume zao...” (QS. An-Nur [24]: 31)

haikuhusishwa na Uislamu pekee, hivyo basi muamala wake ni mmoja iwe ni Muislamu au kafiri.

Na katika hadithi: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alimkubalia (Mama wa Waumini) Ummu Habiba binti Abi Sufyan kutojihijabi mbele ya baba yake, pamoja na kwamba alikuwa kafiri wakati alipokuja Madina kuhuisha mkataba wa Hudaybiyyah na akashuka (kufikia) kwake naye hakujihijabi mbele yake. Na lau kama ukafiri wake ungemfanya kuwa si kama baba Muislamu, basi angejihijabi mbele yake.

Hii ina maana kwamba:

أَوْ آبَائِهِنَّ

“...au baba zao...” (QS. An-Nur [24]: 31)

ambayo ilitangulia kabla ya (au baba wa waume zao) inajumuisha baba kafiri na Muislamu kwa usawa kuhusiana na mahram, na hivyo hivyo (baba wa waume zao). Kwa hivyo, inajuzu kwa mke Muislamu wa mshiriki kumtendea baba kafiri wa mume wake muamala wa baba Muislamu kuhusiana na awrah. Na hapa ni kujuzu (jaiz) na si lazima (wajib), yaani kuonyesha awrah mbele yake kama mahram Muislamu ni jambo linalojuzu na kutokuonyesha pia kunajuzu, na mimi napendelea kupunguza kuonyesha awrah mbele ya mahram kafiri kwa sababu ya ukafiri wake.

28/07/2004 M.

Share Article

Share this article with your network