Mtu mkuu, anayeongoza chama kikuu, na anayefanya kazi kwa ajili ya lengo kuu, akiishi kama mgeni, asiyejulikana jina lake halisi wala sura yake hata kwa baadhi ya wapenzi wake. Mjukuu anamwona baada ya kutokuwepo kwa muda mrefu, lakini hamkumbatii wala kucheza naye, kama afanyavyo babu kwa mjukuu wake, kwa hofu ya usalama wake usije ukajulikana kupitia neno hapa au pale, likawafikia mashetani wa kiwanadamu na kijini miongoni mwa wapelelezi wa madhalimu.
Mtu adhimu aliyebeba roho yake kiganjani mwake katika kazi ya mfululizo ya kuamsha Umma, kuitukuza dini yake, kufikia utukufu wake, na kulinda heshima yake. Alitumia maisha yake akitafuta kheri kwa ajili ya Umma kwa bidii, akisubiri kwa subira pale Umma ulipompa kisogo, akihurumia hali yake, huku akiuona ukikanyagwa na madhalimu bila kuchukua hatua au kuasi, bali unaamka na kulala kwenye dhuluma, ukionja uchungu wa giza, usimamizi mbaya wa mambo, dhiki ya maisha, na mzigo mzito wa kodi.
Mtu adhimu anafariki na watu hawakusanyiki wakati wa kufa kwake, wala mabega yao hayasongamani katika kubeba jeneza lake, kwani msafara nyuma yake ulikuwa mdogo, na umati ulikuwa haba.
Mtu adhimu anafariki, na hawatembei nyuma yake isipokuwa makumi machache ya wanaume wasiozidi hapo, watu hawaungani na jeneza lake linapopita karibu nao, bali hawalijali wala kulisindikiza. Hawajui kuwa ndani ya jeneza hilo kuna mtu ambaye jina lake lilitikisa madhalimu, na lile lengo alilokuwa akilifanyia kazi—Khilafah Rashidah—liliwapigisha ganzi makafiri wakoloni huko Washington, London, Paris, Moscow, na Roma, bila kusahau vibaraka wao wadhalilifu.
Mtu adhimu anafariki, na madhalimu wanaogopa kifo chake kama walivyoogopa uhai wake, hivyo wanaziamrisha magazeti yao yasichapishe habari ya kifo chake ili macho ya watu yasiangukie jina lake na kuwapata kizunguzungu kama kilivyokuwa kikiwapata kabla ya kifo chake.
Usihuzunike Ewe Abu Yusuf, kwani unahamia kwenye nyumba iliyo bora kuliko nyumba hii, nyumba tukufu ambayo hakuna mwenye mamlaka ndani yake isipokuwa Mola wa walimwengu wote. Na hakika huko utawakuta, kwa idhini ya Allah, wapenzi wako; Mtume wa Allah (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam), maswahaba wake (Radhiya Allahu 'anhum), waliowafuata kwa wema (Tabi'un), na wale waliokutangulia kwa imani. Na ni nyumba bora ilioje hiyo na wakazi wake ni bora walioje!
Usihuzunike Ewe Abu Yusuf kwa uchache wa watu waliokufuata wakati wa kifo chako, kwani kilicho kwa Allah ni bora zaidi. Malaika wa rehema watakupokea katika mabustani ya Pepo, na rehema ya Allah, mapenzi Yake, na radhi Zake vitakuzingira.
Usihuzunike Ewe Abu Yusuf, kwani Hizb (chama) ulichokijenga ulichorithi kutoka kwa mtangulizi wako mwema, na ukakiimarisha kwa mikono yako mitukufu, kitaendelezwa na sahiba wako baada yako katika kukiimarisha hadi itakapopandikizwa juu ya kilele chake Bendera ya Al-Uqab, bendera ya "La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah".
Usihuzunike Ewe Abu Yusuf, kwani viongozi wa jeshi watakuja kukuzuru wakiwa wamefungiwa bendera kwa majina ya Mtume, maswahaba wake na waliowafuata kwa wema. Itakujia kikosi cha Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam), Abu Bakr, Umar, Uthman, Ali, Hasan, Husayn, Khalid, Al-Mu'tasim, Salahu ad-Din, Az-Zahir, na Al-Fatih. Kitakujia kikosi cha Taqiyuddin na kikosi cha Abdul Qadeem, vyote vikinyanyua bendera vilivyofungiwa. Wanajeshi wake watakujia makundi kwa makundi wakiwa washindi, wakizuru kaburi lako na kaburi la sahiba wako aliyekutangulia wakipiga takbira, na kwa utukufu na nguvu wakisema: "Hakika Khilafah imesimamishwa, nyumba ya watu waumini, na umekoma uwepo wa mayahudi, na Roma imefunguliwa, na haki imekuja na batili imetoweka, na Uislamu na Waislamu wametukuka na ukafiri na makafiri wamedhalilika."
Usihuzunike Ewe Abu Yusuf, kwani vijana uliowaacha nyuma yako ni vijana wenye nyuso zenye nuru na waliobarikiwa, wanaoendelea katika njia ile ile aliyoichora Mtume wa Allah (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) kwa wahyi kutoka kwa Mola wa walimwengu wote. Wanafuata nyayo za Mtume wa Allah (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) bila kugeuka, wakimuomba Allah kwa ajili yako usiku na mchana ili Allah akufunike kwa rehema Zake pana na akushushe katika makazi Aliyoyaandaa Allah kwa ajili ya mawalii Wake wateule, Firdaus al-A'la pamoja na Mtume na maswahaba wake. Kwani wewe, kwa idhini ya Allah, ni miongoni mwa watu wa utiifu Kwake na wenye kupendwa naye.
وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقاً
"Na wanaomtii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao watakuwa pamoja na wale alio neemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Waja wema. Na uzuri ulioje wa rafiki hao!" (QS. An-Nisa [4]: 69)
Sahiba wako baada yako