Sifa zote njema ni za Allah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Allah, familia yake, maswahaba wake, na wanaomfuata, ama baada ya hayo:
Kwa Umma mtukufu wa Kiislamu, umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu...
Kwa wabebaji lingano, wanaume shupavu ambao biashara wala kuuza hakuwapumbazi na kumdhukuru Allah...
Kwa wageni watukufu wa ukurasa huu wanaopenda kheri na watu wake na kuifanyia kazi...
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Nawapongeza kwa mwezi huu mtukufu:
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ
"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’an kuwa ni uongofu kwa watu na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi." (QS. Al-Baqarah [2]: 185)
Na namuomba Allah Subhanahu wa Ta'ala awakubalie Waislamu wote saumu zao na visimamo vyao, na uwe mwanzo wa kheri na baraka, na utangulizi wa ushindi kwa kusimamisha Khilafah Rashidah, ili Umma upate kivuli cha bendera ya Al-Uqab, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na urejee kama ulivyokuwa, Umma mtukufu, wenye nguvu kwa Mola wake, mwingi wa izza kwa dini yake:
وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
"Na siku hiyo waumini watafurahi * Kwa ushindi wa Allah; humsaidia amtakaye, Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS. Ar-Rum [30]: 4-5)
Na mwisho, nawapelekea salamu, nawaombea kheri, na Allah akubali saumu na visimamo, na Allah Subhanahu wa Ta'ala ndiye mlinzi wa waja wema.
Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah