Jibu la Swali: Kuhusu Ash-Sham na Mapinduzi yake
Kwa Abu Alabed Alansary
Swali:
Assalam Alaykum, Sheikh mpendwa, Mwenyezi Mungu akuhifadhi kwa kutoa heri, Mwenyezi Mungu awanusuru,
Ujumbe kwa Hizb ut-Tahrir,
Assalam Alaykum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,
Pengine imekuwa ni kawaida kwetu kufafanua mambo kwa kina na kutoa taswira fulani, na kulingana na hilo tunatoa wazo na kuusoma ukweli halisi usomaji mzuri, na kuona ni maoni gani sahihi ndani yake kutoka kwa wale tunaowaamini (Kiongozi ambaye siku zote ni mkweli na hamdanganyi watu wake), Mwenyezi Mungu awalipe heri.
Lakini nitaingia kwenye mada moja kwa moja na ujumbe wangu ni swali moja tu.
Ni lini Hizb itakusudia kuamsha maoni ya umma katika nchi na miji mikuu ya Waislamu kwa ajili ya kunusuru mapinduzi ya Ash-Sham?
Mtu anaweza kusema kwamba kusoma mwenendo wa mapinduzi, mwelekeo wake, na hatua itakazopitia katika siku zijazo kutashughulikiwa kulingana na matukio na hali yake, hasa yale yanayoasubiri ya mshangao yanayofanya kazi kwa maslahi yake au vitimbi vinavyopangwa na kuandaliwa dhidi yake. Ni lazima kwetu kusoma ukweli wa kila hatua kulingana na mambo mapya yanayojitokeza na matokeo ya msimamo wa kimataifa yanayohusiana nayo.
Hakuna shaka kwamba kasi ya matukio imeanza kuongezeka kwa nguvu na hatua za kuvunjana mifupa zinaongezeka; ama mapinduzi haya yawe na subira na kutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu (swt), au yalegee mbele ya shinikizo na njama zinazowekwa juu yake kutoka kwa rafiki na wa karibu kabla ya adui mkuu na zana zake.
Tunajibu kwa ufupi na kusema hapana shaka kwamba mapinduzi ya Ash-Sham ni mazuri na yenye baraka na ni ya ikhlasi, lakini hayakuwa bila uchafu kutoka kwa wale waliojaribu kuyaparamia, miongoni mwa watu wake, na hii haikomei tu katika pande za kisiasa kama vile Baraza la Kitaifa au Muungano wa Kitaifa, bali hata iliathiri makundi ya kijeshi katika mabaraza ya kijeshi.
Ni haki yetu kama Waislamu kuuliza na kuwauliza wale tunaowaamini na kuamini ikhlasi yao na kazi yao katika Umma, kwani ninyi baada ya Mwenyezi Mungu (swt) ndio tumaini la Umma huu, uongozi na vijana.
Yale niliyoyataja hapo awali kama swali langu yana taswira moja niliyoijengea swali hili:
Naomba maneno yangu yasieleweke kama vile ninatoa maelekezo, kwani sisi tunajifunza kutoka kwenu.
Je, kuamsha miji mikuu ya ulimwengu wa Kiislamu si jambo litakalopelekea kuamsha Umma na kuufanya uamke na kuwanusuru watu wake huko Ash-Sham kwa njia zote unazopaswa kuzitafuta ili kupata upenyo au njia ya kufanya hivyo?
Je, hili halichukuliwi kuwa na matokeo chanya katika kuimarisha uthabiti na kusimama imara kwa watu wa Ash-Sham watakapoona kuwa Umma mzima uko pamoja nao, hivyo nguvu zao zikaongezeka, wakapewa msaada, na uthabiti wao na kusimama kwao imara kukaongezeka InshaAllah juu ya haki, hasa baada ya huu ubaridi na kukatishwa tamaa kulikosababishwa na Muungano (Coalition) wa khaini na upinzani ulioparamia mapinduzi?
Kisha kuunganisha safu za Umma ili uthibitishe kuwepo kwake mbele ya maadui zake, hasa madola ya kikafiri ya Magharibi na mkuu wao Marekani, je, hili halina athari chanya kwa mapinduzi ya ndani na kisha kwa Umma kwa ujumla katika maeneo mbalimbali uliyopo? Hivyo tuipe Marekani ujumbe mzito kwamba sisi ni Umma mmoja na unaanza kunyanyuka, na hamtapita juu ya mapinduzi yetu na kuvuna matunda yake, na tutapambana nanyi kwa kila tulicho nacho.
Sheikh wangu mpendwa, Mwenyezi Mungu akuhifadhi na kukulinda, ewe mtoaji wa heri, baraka, na ushindi wa wazi, InshaAllah uwe mikononi mwako, itangaze na upige takbira, kwani wallahi ambaye hakuna mungu isipokuwa Yeye, tutakuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mkono utakaopigia.
Tukifanya vyema ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na tukikosea ni kutoka kwangu na kwa Shetani, na ni udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).
Ndugu yenu Abu Alabed Alansary / Baitul Maqdis - Palestina
Jibu:
Ndugu mpendwa Abu Alabed Alansary
Wa Alaykum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh.
Nimeusoma ujumbe wako, na ni ujumbe wa heshima kutoka kwa ndugu mwenye heshima...
Ama kuhusu mada ya Ash-Sham na mapinduzi yake, kama unavyojua kuwa eneo ambalo tumetoa matoleo mengi zaidi kutoka kwa Hizb na wilaya zake ni Ash-Sham. Hatukuacha jambo dogo wala kubwa isipokuwa tumelifafanua kadiri ya uwezo wetu, na hatukutosheka na maandishi tu bali hata jumbe za sauti...
Ama kuhusu kile kinachoendelea huko Ash-Sham kwamba si chote ni safi, hilo ni kweli, na tayari tulishafafanua hilo hapo awali. Ukweli wa kile kinachoendelea huko ni kama ifuatavyo:
Wachache waliohadaiwa na utamaduni wa Magharibi, walioathiriwa na fikra na dhana zake, wanasema yale inayoyasema, na wanatoa mwito wa dola ya kiraia (civil state), ya kidemokrasia na kisekula, inayotenganisha dini na maisha...
Kundi lingine lenye idadi kubwa zaidi kuliko hao wachache, na lenye uzito zaidi... Hao ni Waislamu ambao macho yao yana utando: wanapenda Uislamu na wanataka Khilafah, na wanaipenda bendera ya Mtume (saw), lakini hawatangazi kile wanachokipenda na kukitaka kwa hofu ya kuyachokoza madola ya kikoloni, na wala hawaibebe bendera kwa hofu ya kuwakasirisha wale wanaodai utaifa!
Kundi linalotoa mwito wa utawala wa Kiislamu, nalo limegawanyika sehemu mbili:
Sehemu inayotumia vitendo vya kinguvu (material acts) na kutoa mwito wa utawala wa Kiislamu, lakini haina ufahamu kamili na sahihi juu ya fikra za Kiislamu na hukumu zake, na juu ya matukio yanayoendelea... n.k.
Na sehemu ya kweli na yenye ikhlasi inayotaka utawala wa Kiislamu "Khilafah ya Rashidun", kwa njia aliyoifuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), hivyo inatafuta Nusrah (msaada wa kinguvu) kutoka kwa watu wake...
Sisi, ewe ndugu mpendwa, katika vitendo vyetu vyote tunashikamana na njia ya Mtume (saw) na tunaweka mstari ulionyooka kando ya mstari uliopinda, na tunadhihirisha haki na kuhimiza kwayo, si huko Ash-Sham pekee, bali kuna kazi tunazozifanya katika maeneo mengine, hasa katika maeneo yanayopakana na Ash-Sham, na ni kazi zinazoshuhudiwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na tunamuomba Yeye (swt) msaada na taufiki.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwa tovuti ya Amir
Kiungo cha jibu kutoka kwa ukurasa wa Amir kwenye Google Plus