Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jawabu la Swali: Mchakato wa Kuyeyusha Kabla na Baada ya Kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu

April 27, 2016
5249

** (Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Ameer wa Hizb ut Tahrir, kwa Maswali ya Wageni kwenye Ukurasa Wake wa Facebook "Fikri")**

Jawabu la Swali

Kwa: Mustapha El Mawed

Swali:

Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Je, ni ipi taswira yenu kuhusu jinsi ya kutekeleza mchakato wa kuyeyusha (Al-Amaliyyah al-Sahriyyah) baada ya kushika utawala? Je, itakuwa ni kupitia halaka za utamaduni wa pamoja (thakafa jama'iyyah), au mihadhara, au kupitia vyombo vya habari, au mitaala ya elimu? Jazakumullah Khayran.

Jawabu:

Waalaykum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh,

Kabla ya kujibu swali lako, nakunukulia kutoka katika kitabu cha At-Takattul (Mshikamano wa Kihizbi) baadhi ya yale yanayobainisha kiini cha mchakato wa kuyeyusha:

(...Chama cha kifikra (mubda'i) hukua kiasili katika pande mbili: moja ni kuongezeka kwa seli zake kwa kutengeneza seli nyingine zinazofuata mfumo huo kwa ufahamu na utambuzi kamili, na ya pili ni kutengeneza ufahamu wa jumla (wa’y al-aam) kuhusu mfumo huo kwa Umma mzima. Kutokana na ufahamu huu wa jumla wa mfumo huo, kunatokea kuunganishwa kwa fikra, maoni, na itikadi miongoni mwa Umma; muungano wa kijumuiya ikiwa si wa kauli moja (ijma'i). Kwa njia hiyo, lengo la Umma huunganishwa, itikadi yake huunganishwa, na mtazamo wake wa maisha huunganishwa. Kwa hali hii, Chama kinakuwa kama tanuru linalouyeyusha Umma, kikisafisha kutokana na uchafu na uharibifu uliosababisha kuporomoka kwake, au uliozuka wakati wa kuporomoka huko. Mchakato huu wa kuyeyusha hufanywa na Chama ndani ya Umma, na ndio unaosababisha mwamko (nahdah). Na huu ni mchakato mgumu. Kwa hiyo, hakuna anayeweza kuufanya isipokuwa Chama kinachoishi kwa fikra yake, kikayafanya maisha yake kuwa wakfu kwa ajili ya fikra hiyo, na kutambua kila hatua katika hatua zake.) Mwisho wa nukuu.

Hivyo basi, Chama hufanya mchakato wa kuyeyusha ndani ya Umma, na kinatumia kila njia na mbinu kinazoweza ili kuufanikisha mchakato huu kwa njia bora zaidi... Kwa sasa, Chama kinatekeleza mchakato wa kuyeyusha kwa kutumia mbinu na njia zinazopatikana... Na baada ya kusimamishwa Dola kwa idhini ya Allah, Chama kitaendelea na mchakato huu... Lakini tofauti itakuwepo katika nyanja zifuatazo:

A- Kwamba Uislamu ndio utakaokuwa unatekelezwa baada ya kusimamishwa kwa Dola, na bila shaka jambo hili litakuwa na athari kubwa katika kuharakisha mchakato wa kuyeyusha... Hii ni kwa sababu mfumo utakaokuwa unatekelezwa na shughuli za utunzaji (ra'ayah) zinazoendeshwa zitaendana na mchakato wa kuyeyusha unaofanywa na Chama... Tofauti na hali ya sasa ambapo mifumo ya kikafiri inatekelezwa na Waislamu wanatawaliwa na watawala wanaoufanyia uadui Umma na dini yake, jambo linalofanya mafanikio katika mchakato wa kuyeyusha kutokuwa mepesi...

B- Kwamba njia na mbinu zenye athari ambazo Chama kinaweza kuwafikia watu zitakuwa wazi bila vizuizi, kwa sababu Dola inawajibika kisheria kutoa nafasi kwa vyama vya kisiasa vilivyosimama juu ya msingi wa Uislamu, bali inawajibika kuviuunga mkono vyama hivyo katika shughuli zao... Kwa hiyo, televisheni, redio, mitandao ya intaneti, misikiti, na mikutano mbalimbali... na njia zote na mbinu kama ulivyozitaja katika swali, zitakuwa chini ya usimamizi wa vyama hivi vya kisiasa bila vikwazo au usumbufu... Na bila shaka, jambo hili litaharakisha mchakato wa kuyeyusha na kuupelekea kukamilika na kufanikiwa kwa idhini ya Allah.

Na bila shaka, Chama kitaendelea na kazi zake zote: thakafa ya umakini (tathqif murakkaz), thakafa ya kijumla (tathqif jama'i), pambano la kifikra, mapambano ya kisiasa, na kupigania maslahi ya Umma...

C- Utekelezaji wa Uislamu na Dola utakuwa na mchango mkubwa katika kujenga ufahamu wa jumla (wa'y al-aam) kwa Umma mzima. Kutokana na ufahamu huu wa jumla kuhusu mfumo huu, kutatokea kuunganishwa kwa fikra, maoni, na itikadi ndani ya Umma... Hii itaharakisha mchakato wa kuyeyusha, na kufuatiwa na mwamko wa Umma... Hivyo basi, kazi katika uwanja huu itakuwa rahisi zaidi na yenye kasi zaidi kwa idhini ya Allah baada ya kusimamishwa Dola kuliko ilivyo kabla yake...

Natumai kuwa mada hii imebainika kwa kiasi cha kutosha kwa idhini ya Allah Subhanahu.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

20 Rajab 1437 H Sawia na 27/04/2016 M

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Ameer: facebook

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Google Plus wa Ameer: Googleplus

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Twitter wa Ameer: Twitter

Kiungo cha jawabu kutoka kwenye tovuti ya Ameer

Share Article

Share this article with your network