Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Kuhusu Demokrasia

June 01, 2013
4947

(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni wa Ukurasa Wake wa Facebook)

Jibu la Swali: Kuhusu Demokrasia

Kwa Irfan Abu Naveed

Swali:

Hakika Umma wa Kiislamu katika zama zetu hizi umevamiwa na dhana potofu na itikadi batili ngeni kwa dini yetu tukufu, ambazo zinapingana na kugongana na itikadi ya Kiislamu kwa kila namna na upande, na miongoni mwa hizo ni demokrasia batili. Tatizo hatari tulilo nalo ni kwamba baadhi ya Waislamu nchini Indonesia wanadai kuwa demokrasia inatokana na Uislamu, na wanatolea dalili za kisheria kutoka katika Qur'ani Tukufu na Sunnah za Mtume kwa kutumia dhana potofu na kulazimisha matumizi ya dalili hizi.

  1. Je, nini maoni yako ewe Sheikh wetu kuhusu demokrasia?

  2. Na ni vipi tunaweza kujikwamua na tatizo hili hatari?

  3. Nataka kuandika kitabu kuhusu jambo hili. Nini maoni yako ewe Sheikh wetu? Na nakuomba ushauri kuhusiana na jambo hili.

Jibu:

Waalaykum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh

Demokrasia maana yake ni kuwa enzi ni ya wananchi, hivyo wao ndio wanaotunga sheria badala ya Allah, yaani wanahalalisha na kuharamisha badala ya Allah, na Allah (swt) anasema:

إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ يَقُصُّ الْحَقَّ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ

"Hukumu si ya yeyote ila ni ya Allah tu; Yeye anahadithia yaliyo kweli, naye ni Mbora wa wenye kupambanua." (Al-An'am [6]: 57)

Na katika Hadith Tukufu iliyopokelewa na At-Tabarani katika Al-Kabir kutoka kwa Adi bin Hatim amesema: "Nilimjia Mtume (saw) na shingoni mwangu mlikuwa na msalaba wa dhahabu, akasema: 'Ewe Adi, tupa hicho kinyago shingoni mwako', basi nikakitupa na nikafika kwake naye akisoma Surah Bara'ah (At-Tawbah), akasoma aya hii:

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللهِ

"Wamewafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allah." (At-Tawbah [9]: 31)

Mpaka akaimaliza, nikasema: 'Hakika sisi hatuwaabudu', akasema: 'Je, si wanaharamisha alichohalalisha Allah nanyi mnaharamisha, na wanahalalisha alichoharamisha Allah nanyi mnahalalisha?' Nikasema: 'Ndiyo', akasema: 'Basi huko ndiko kuwaabudu'." Kwa hiyo, yeyote anayetunga sheria badala ya Allah, dhambi yake ni kubwa mno.

• Kwa hiyo, demokrasia kupitia mlango huu ni mfumo wa kikafiri kwa sababu unafanya utungaji sheria kuwa ni wa wanadamu na si wa Mola wa wanadamu.

Na kupitia mlango mwingine, demokrasia inajengwa juu ya uhuru nne: Uhuru wa itikadi, uhuru wa kifikra, uhuru wa miliki, na uhuru wa shakhsia.

Hivyo, inaruhusu mtu kuamini anachotaka, anaweza kubadili dini yake anavyotaka, anaweza kusema maoni yoyote anayotaka hata kama yatatusi matukufu... na anaweza kumiliki kwa njia ya halali au haramu, na anaweza kufanya zinaa mradi tu pande mbili zimeridhiana. Na jambo hili ni haramu katika Uislamu, kwani kuritadi ni haramu, zinaa ni haramu, kumiliki kwa njia zisizo za kisheria ni haramu, na kusema kwa matusi na kashfa vivyo hivyo ni haramu.

• Hivyo basi, demokrasia kwa kuruhusu uhuru huu pia ni mfumo wa kikafiri kwa sababu inamaanisha kujivua na hukumu za kisheria.

Kuna kitabu kinachoitwa Demokrasia ni Mfumo wa Kikafiri (Ad-Dimuqratiyya Nidhamu Kufr), kiombe kutoka katika ofisi ya Hizb katika nchi yako, kwani ndani yake mna ufafanuzi wa suala la demokrasia na jinsi ambavyo ni mfumo wa kikafiri.

Mwishoni, nakutumia salamu, na nakuombea msaada na taufiki katika kile unachoandika katika kheri kwa ajili ya Uislamu na Waislamu.

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka katika ukurasa wa Amir kwenye Facebook

Kiungo cha jibu kutoka katika tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka katika ukurasa wa Amir kwenye Google Plus

Share Article

Share this article with your network