** (Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook)**
Kwa Durrah al-Sham
Swali:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh
Mimi si mwanachama wa chama hiki, lakini nina ombi kwenu tafadhali...
Mna mfumo wa elimu, programu, na mambo mengine niliyoyasoma na yakanivutia sana.
Je, hakuna mtaala uliokamilika kwa ajili ya madarasa yote, kwa masomo yote ya kisharia na ya kisayansi... ambao tunaweza kuusoma katika maeneo yaliyokombolewa huko Sham kwa mfano, au sehemu yoyote yenye uhuru wa elimu? Hususan katika mazingira haya ambapo kila anayetaka anafungua shule binafsi, awe ana lengo na fikra au hana... na sijui kizazi hiki kitalelewa vipi, Mwenyezi Mungu atusaidie na awasaidie.
Nilifikiria kutoa wazo hili kwa kila mwenye uwezo wa kuandika mtaala na mwenye uchungu kwa watoto wake ili wasije wakalelewa na watu baki kutoka nchi zote za Kiislamu, ili uwe mtaala mpana.
Lakini niliwaza kuwa ikiwa mtaala huu upo kwenu, kwa nini nipoteze muda kuandaa mtaala mwingine? Afadhali nikamilishe pale mlipoishia, hata kama nitaanza na jamaa zangu na wapendwa wangu. Mwenyezi Mungu awalipe kheri, iwe mtajibu au hamtajibu.
Jibu:
Wa Alaikum Salam Wa Rahmatullahi Wa Barakatuh
Naam, tunao mtaala wa elimu, lakini unahitaji wenye kuanzisha shule na walimu wa kuufundisha. Jambo hili linahitaji mamlaka (sultah) itakayoutekeleza kwa msingi wa hukumu za Sharia, na kuutambua kama cheti cha shule ili mwanafunzi aweze kukamilisha hatua za kimasomo. Haya yote yanahitaji Dola inayohukumu kwa Uislamu na kuupitisha mtaala huu katika elimu.
Mamlaka hii kwa sasa haipo, hivyo utawezaje kuufundisha na wapi? Kwa vyovyote vile, tunafanya kazi kwa bidii kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashidah, ambayo itatekeleza mtaala wa elimu kulingana na hukumu za Sharia, InshaAllah, na tunatumai itakuwa hivi karibuni.
Mwisho, Mwenyezi Mungu akubarikie kwa bidii na shauku yako.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Amir: Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus