Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

JIBU LA SWALI: KUHUSU MAANA HALISI YA DEMOKRASIA

October 02, 2011
2358

Swali:

Imenukuliwa katika kitabu "Al-Ajhizah" (Vifaa vya Dola), ukurasa wa 16, usemi unaosema: "Mfumo wa utawala katika Uislamu si wa kidemokrasia kwa maana halisi ya demokrasia," kana kwamba kuna utatanishi fulani katika usemi huo... Ni nini faida ya kutaja "maana halisi"? Tunaomba ufafanuzi, na Mwenyezi Mungu akulipe kheri.

Jibu:

Kilichoelezwa katika kitabu "Al-Ajhizah", ukurasa wa 16 ni kama ifuatavyo:

"Na mfumo wa utawala katika Uislamu si wa kidemokrasia kwa maana halisi ya demokrasia, kwa upande kwamba utungaji sheria ni wa watu; watu ndio wanaohalalisha na kuharamisha, na kuamua kizuri na kibaya. Na kwa upande wa kutofungamana na hukumu za kisheria kwa kisingizio cha uhuru mbalimbali. Makafiri wanatambua kuwa Waislamu hawatakubali demokrasia katika maana yake halisi; kwa hiyo, mataifa ya kikoloni ya kikafiri (na hasa Marekani leo) yanajaribu kuipigia debe katika nchi za Waislamu kwa kuingiza upotoshaji kwamba demokrasia ni njia tu ya kumchagua mtawala... Na wamezunguka na kuficha sehemu ya msingi ya demokrasia, ambayo ni kwamba utungaji sheria, uhalalishaji, na uharamishaji unakuwa ni wa wanadamu na si wa Mola wa wanadamu... wakijiepusha na maana halisi iliyowekwa na wenyewe (Wamagharibi) kwamba demokrasia ina maana ya mamlaka (sovereignty) kuwa ni ya watu, ambapo watu hutunga sheria wanazotaka kwa maoni ya wengi, wanahalalisha na kuharamisha, wanaamua kizuri na kibaya, na kwamba mtu yuko 'huru' katika matendo yake, anafanya anachotaka, anakunywa pombe, anazini, anaritadi (kuacha dini), anatukana vitu vitukufu na kuvisuta, yote hayo chini ya jina la demokrasia na uhuru wake. Hii ndiyo demokrasia, huu ndio uhalisia wake, maana yake na ukweli wake. Basi inawezekanaje kwa Muislamu anayemwamini Mwenyezi Mungu akadiriki kusema kuwa demokrasia inaruhusiwa, au kwamba inatokana na Uislamu?!

Ama kuhusu suala la Ummah kumchagua mtawala, yaani kumchagua Khalifa, hilo ni jambo lililowekwa wazi na maandiko (nass)..." mwisho wa nukuu.

Ni wazi kutokana na hayo kwamba kutajwa kwa "maana halisi" ilikuwa ni kwa ajili ya kutofautisha kati ya demokrasia katika maana yake halisi ya istilahi (kitaalamu) na maana wanayoipigia debe kwamba ni uchaguzi tu... Hii ni kwa sababu baadhi ya watu wanadhani kuwa demokrasia ni mchakato wa uchaguzi tu, na hii siyo maana halisi ya demokrasia.

Ama kuhusu kumchagua mtawala na kumpa bay'ah (kiapo cha utii), hili lipo katika Uislamu karne nyingi kabla ya nchi za Magharibi kulijua.

Share Article

Share this article with your network