Home About Articles Ask the Sheikh
Maswali na Majibu

Jibu la Swali: Ni vipi Tutaweza Kuhukumu kwa Uislamu?

November 11, 2013
3561

** (Mfululizo wa majibu ya mwanachuoni Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook)**

Kwa Abu Ghazi al-Zain

Swali:

Assalamu Alaikum, hali yako vipi Amir wetu? Tunakuombea neema ya afya njema, na tunamuomba Allah (swt) akushike mkono kwa yale anayoyapenda na kuyaridhia na ayasididie hatua zako. Swali langu ni:

Maswali yamekuwa mengi siku hizi kutoka kwa watu kwamba, wakati Allah atakapotuneemesha kwa kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah kwa njia ya Utume, ni vipi tutaweza kuhukumu kwa Uislamu? Na tunajua kuwa Uislamu lazima utekelezwe kikamilifu kuanzia siku zake za kwanza. Hivyo, ni yapi maamuzi, taratibu, na hatua za kivitendo ambazo lazima zichukuliwe mara tu baada ya kutangazwa kwa Khilafah ya Kiislamu? Na nini jukumu letu kama vijana wa kundi hili katika nchi zinazozunguka Dola ya Khilafah, mara tu baada ya kutangazwa kwake kwa idhini ya Allah Ta'ala?

Na Allah akujazi kheri kwa juhudi zako.

Abu Ghazi kutoka Tripoli, Sham.

Jibu:

Wa Alaikum Salaam wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Mambo yana nyakati zake, hivyo usifanye haraka. Vijana wameandaliwa kwa jambo hili kwa ujumla. Hakika fikra za Chama (Hizb) na dhana (mafahim) zake, na yale yaliyomo katika vitabu vyake kuhusu mifumo (anidhimah) na katiba (dustur)... na njia (tariqah) wanayofuata, yote hayo yanawafanya vijana kuwa tayari kwa ajili ya jambo hili kwa idhini ya Allah. Hii ni kwa ujumla...

Ama kwa upande wa maelezo ya kina, itakuwa wakati wake ukifika InshaAllah. Na Allah akubarikie kwa hima na umakini wako.

Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amir

Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Google Plus wa Amir

Share Article

Share this article with your network