(Mfululizo wa Majibu ya Mwanachuoni Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa Hizb ut-Tahrir, kwa Maswali ya Wageni wa Ukurasa Wake wa Facebook)
Kwa "Abu Abdurrahman al-Tumayzi"
Swali:
Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Hili ni swali ambapo ninalinganisha wakati wa kupata Nusra kwa Mtume (saw) na kuanza kwa Hijra ya Maswahaba wake, na kile kinachotokea sasa nchini Syria.
Hizb ut-Tahrir ni chama cha kisiasa kinachofuata njia ya Mtume kusimamisha Dola ya Kiislamu. Na sasa Hizb ut-Tahrir imeanza kupata Nusra nchini Syria na tumeona hilo kwenye Ofisi ya Habari ya Kati ya Hizb,
Swali: Kwa nini Hizb ut-Tahrir haiwaombi wanachama wake kufanya Hijra kwenda Syria kama Mtume alivyowaomba wanachama wake? Au hali halisi ni tofauti? Tafadhali fafanua jambo hili.
Jawabu:
Walaikum Assalam Warahmatullahi Wabarakatuh.
Naam, kwa hakika Mtume (saw) aliwaamrisha Maswahaba kufanya Hijra kwenda Madinah, lakini hii ilikuwa baada ya Mtume (saw) kupata Nusra kutoka kwa watu wa Madinah, yaani baada ya Bai'at ya pili ya al-Aqaba. Nayo ni Bai'at ya utawala, yaani Madinah ilikuwa imeshakuwa Dar al-Islam kisheria (hukman) kwa sababu nguvu ilikuwa imeshapatikana humo kwa ajili ya Uislamu na Waislamu, na ilikuwa ikingojea kuwasili kwa Mtume wa Allah (saw) ili iwe Dar al-Islam kiuhalisia (fi'lan) ambapo sheria zitatekelezwa...
Na wakati tutakapofikia mfano wa Bai'at ya pili ya al-Aqaba, hapo ndipo Hijra itakuwa katika uhakika wake kulingana na hukumu za kisheria.
Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Facebook
Kiungo cha jawabu kutoka kwenye tovuti ya Amir
Kiungo cha jawabu kutoka kwenye ukurasa wa Amir wa Google Plus