** (Silsila ya majibu ya mwanachuoni mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Amiri wa Hizb ut-Tahrir, kwa maswali ya wafuasi wa ukurasa wake wa Facebook)**
Kwa Lone Traveller
Swali:
(Assalamu Alaikum our honorable Ameer: We say that establishment of Khilafah and Jihad are different obligations justifying the point that Jihad can't be the methodology to establish the Khilafah. Can you explain that these two are different obligations? May Allah (swt) accept you and give you the responsibility to guide the Ummah) end
Tafsiri ya Swali:
(Assalamu Alaikum Amiri wetu mtukufu: Tunasema kwamba kusimamisha Khilafah ni faradhi na Jihadi ni faradhi nyingine, na kwamba Jihadi siyo njia ya kusimamisha Khilafah... Naomba ufafanuzi wa jambo hili... Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) akutakabali na kukuneemesha kwa uongozi wa Umma).
Jibu:
Waalaikum Salaam Warahmatullahi Wabarakatuh.
Kuna mambo ya kimsingi ambayo ni lazima yaeleweke vyema kwa sababu yanabainisha jibu:
1- Dalili zinazohitajika ili kutoa hukumu ya kisheria (istimbat) kwa suala fulani ni dalili zinazohusu suala hilo lenyewe, na si dalili za suala jingine:
a- Kwa mfano, nikitaka kujua jinsi ya kutawadha, nitatafuta dalili za udhu popote zilipo, ziwe zilitelemshwa Makka au Madina, na hukumu ya kisheria hutolewa kutoka humo kulingana na misingi (Usul) inayofuatwa... Lakini sitafuti dalili za funga ili kuchukua kutoka humo hukumu ya udhu na namna yake.
b- Na kwa mfano, nikitaka kujua hukumu za Hajj, vilevile nitatafuta dalili za Hajj popote zilipo, ziwe zilitelemshwa Makka au Madina, na hukumu ya kisheria hutolewa kutoka humo kulingana na misingi inayofuatwa, lakini sitafuti dalili za swala ili kuchukua kutoka humo hukumu ya Hajj na namna yake.
c- Na kwa mfano, nikitaka kujua hukumu za Jihadi: ikiwa ni faradhi ya mtu binafsi (fardhu 'ayn) au faradhi ya kutosheleza (fardhu kifayah), katika kujihami au kuanza, na nini kinachotokana na Jihadi miongoni mwa hukumu za ufunguzi (fath) na kueneza Uislamu, iwe ufunguzi huo ni kwa nguvu au kwa suluhu... basi nitatafuta dalili za Jihadi popote zilipo, ziwe zilitelemshwa Makka au Madina, na hukumu ya kisheria hutolewa kutoka humo kulingana na misingi inayofuatwa, lakini sitafuti dalili za Zaka ili kuchukua kutoka humo hukumu ya Jihadi na maelezo yake.
d- Na hivi ndivyo ilivyo katika kila suala, ambapo dalili zake hutafutwa popote zilipokuja, iwe Makka au Madina, na hukumu ya kisheria ya suala hilo huchukuliwa kutoka katika dalili hizi kulingana na misingi inayofuatwa.
2- Sasa tunakuja kwenye suala la kusimamisha Dola ya Kiislamu, na tunatafuta dalili zake, ziwe zilitelemshwa Makka au Madina, na tunatoa hukumu ya kisheria kutoka humo kulingana na misingi inayofuatwa.
a- Hatupati dalili zozote za kusimamisha Dola ya Kiislamu isipokuwa zile alizozibainisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika maisha yake (seerah) kule Makka Al-Mukarramah; alilingania kuelekea kwenye Uislamu kwa siri, akatengeneza kundi (kutla) la waumini wenye kusubiri... kisha akatangaza ulinganifu miongoni mwa watu kule Makka na katika misimu ya Hajj... kisha akatafuta nusra (msaada wa kijeshi) kutoka kwa watu wenye nguvu na ulinzi (ahl al-quwwah wal-man'ah), na Mwenyezi Mungu (swt) akamkirimu kwa Maansari, akahamia kwao na kusimamisha Dola.
b- Mtume (saw) hakupigana na watu wa Makka ili kusimamisha dola, na wala hakupigana na kabila lolote ili kusimamisha dola, pamoja na kwamba yeye (saw) na maswahaba wake (ra) walikuwa mashujaa katika vita, wenye nguvu na wachamungu... Lakini yeye (saw) hakutumia mapigano kusimamisha dola, bali aliendelea kulingania na kutafuta nusra ya wenye nguvu mpaka Maansari walipomwitikia, ndipo akasimamisha dola.
c- Kisha hukumu za Jihadi zikafaradhiwa kwa ajili ya ufunguzi (fath), kueneza Uislamu, na kulinda Dola ya Kiislamu. Jihadi haikufaradhiwa kwa ajili ya kusimamisha dola, na haya yote yako wazi katika seerah yake (saw).
d- Hivyo basi, ikiwa inatakiwa kujulikana namna ya kusimamisha dola, basi inachukuliwa kutoka katika kitendo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) cha kulingania, kutafuta nusra, kuitikiwa na Maansari na kusimamisha dola... Na ikiwa inatakiwa kujulikana hukumu za Jihadi, basi zinachukuliwa kutoka katika dalili za kisheria zinazohusiana na Jihadi. Kila faradhi huchukuliwa dalili zake kutoka katika dalili za kisheria zinazohusiana nayo; hivyo kusimamisha dola huchukuliwa kutoka katika dalili za kusimamisha dola, na Jihadi kutoka katika dalili za Jihadi, na hilo hufuatwa vile lilivyo. Na Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mwongozi wa mafanikio.
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri wa Facebook
Kiungo cha jibu kutoka kwenye tovuti ya Amiri
Kiungo cha jibu kutoka kwenye ukurasa wa Amiri wa Google Plus