Home About Articles Ask the Sheikh
Masuala

Salamu za Pongezi za Amir wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, kwa Waislamu kwa Jumla na kwa Vijana (Shabab) kwa Hasa, kwa Mnasaba wa Eid al-Adha ya Mwaka 1446 H sawia na 2025 M

June 06, 2025
1362

Sifa zote njema ni za Allah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Allah, na familia yake, maswahaba zake na waliomfuata. Baada ya hapo...

الله أكبر الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله، الله أكبر الله أكبر، ولله الحمد...

"Allah ni Mkubwa, Allah ni Mkubwa, Allah ni Mkubwa, hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Allah ni Mkubwa, Allah ni Mkubwa, na sifa njema zote ni za Allah..."

Kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla... Umma bora uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Allah, Mwenye nguvu, Mwenye hikima...

Kwa wabeba dawah hususan... Allah afungue (nusura) kupitia mikono yao, na awaidhi kwa msaada Wake ili wasimamishe Dola ya Kiislamu; Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume...

Kwa wageni watukufu wa ukurasa huu wanaoelekea kwenye kheri iliyobeba... wanaojitahidi kusimama kwenye haki na kuwaunga mkono watu wake...

Kwa hawa wote... Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Nawapongeza kwa Eid al-Adha iliyobarikiwa 1446 H... na namuomba Allah, Mwenye nguvu, Mwenye uwezo, iwe ni ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu wote...

Ndugu Watukufu..

Eid hii inakuja huku uvamizi wa mayahudi ukisaidiwa na Marekani na silaha zake ukiendelea dhidi ya Gaza na Palestina yote.. na watawala katika nchi za Waislamu wanatazama tu kinachoendelea, wakihesabu mashahidi na kuwaita wafu! Na mbora wao katika njia ni yule anayepatanisha kana kwamba yuko upande wowote, bali yuko karibu zaidi na mayahudi! Si ajabu kwamba Marekani na makafiri wakoloni na kiumbe chao, dola ya mayahudi, wanatushambulia kwani wao ni maadui wa Uislamu na Waislamu tangu miaka mingi iliyopita.. wala si ajabu kwamba makafiri wakoloni wakiitegemea Sheria ya Kimataifa wanaweza kushambulia nchi za Waislamu kwa sababu sheria hii ilianza dhidi ya Waislamu na dola yao (Dola ya Othmaniyyah) katika mkutano wa Westphalia mwaka 1648 M ambapo baadaye ilikuja kuwa Umoja wa Mataifa kisha Umoja wa Mataifa.. yote haya si ajabu, lakini la ajabu ni kwamba watawala katika nchi za Waislamu jirani na Palestina wanatazama jinai na mauaji yanayotokea huko, huku wakiwa kimya wakiyazuia majeshi kuisaidia Gaza bali Palestina yote, bali wanahakikisha utekelezaji wa maazimio ya kimataifa yanayowaua Waislamu, Allah awaangamize, vipi wanageuzwa!

Na mwisho, basi simameni enyi majeshi katika nchi za Waislamu kuwanusuru ndugu zenu huko Gaza, na ikiwa mifumo ya utawala wa kidikteta iliyopo katika nchi za Waislamu itasimama mbele yenu, basi wapigeni kwa kila namna.. na simamisheni utawala wa Allah badala yao, Khilafah kwa njia ya Utume, ili kutimiza bishara ya Mtume wa Allah ﷺ:

ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ

"Kisha kutakuwepo na utawala wa kidikteta, utakuwepo kwa muda ambao Allah amekadiria uwepo, kisha Atauondoa Atakapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza." (Musnad ya Imam Ahmad)

..na hapo basi, Khalifah na wasaidizi wake na askari wa Uislamu kutoka vyeo vya juu hadi vya chini watahama kutoka ushindi mmoja kwenda mwingine, wakipiga takbira na Umma ukipiga takbira pamoja nao, wakiwa wenye nguvu kupitia kwa Mola wao, wenye izza kwa dini yao, kiasi kwamba adui hatathubutu kuwa na mamlaka yoyote katika ardhi ya Kiislamu..

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo waumini watafurahi * Kwa nusura ya Allah; Yeye humnusuru amtakaye, Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (Surat Ar-Rum [30]: 4-5)

Mwisho wa yote, namuomba Yeye Subhaanahu iwe Eid hii ni ufunguzi wa kheri, baraka na utukufu kwa Uislamu na Waislamu,

وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُون

"Na Allah ndiye Mwenye kushinda katika jambo Lake, lakini watu wengi hawajui." (Surat Yusuf [12]: 21)

الله أكبر الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله، الله أكبر الله أكبر، ولله الحمد...

Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.

10 Dhul-Hijjah 1446 H Ndugu yenu

Sawia na 06/06/2025 M Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network