Home About Articles Ask the Sheikh
Masuala

Pongezi Kutoka kwa Ameer wa Hizb ut-Tahrir kwa Ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa Mwaka 1439 Hijria sawia na 2018 Miladia

May 15, 2018
3591

Sifa zote njema ni za Allah, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Allah, jamaa zake, maswahaba zake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kwa Umma bora uliotolewa kwa watu...

Kwa wanaume barabara ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Allah...

Kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa huu...

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Nawapongeza kwa kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ

"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi." (Al-Baqarah [2]: 185)

...Mwezi ambao Allah amewakirimu Waislamu kwayo: mwanzo wake ni rehema, katikati yake ni maghfirah (msamaha), na mwisho wake ni kuacha huru kutokana na moto... Humo iliteremshwa Qur'ani Tukufu, na humo kulikuwa na ushindi na ufunguzi ulio wazi... Ni mwezi wa kazi, juhudi na bidii, na mwezi wa ibada, subira na jihadi... Hivyo basi jitahidini enyi Waislamu, na shindaneni katika kheri, ambapo malipo na thawabu huongezwa maradufu...

Namuomba Allah (swt) awakubalie Waislamu funga zao, kisimamo chao (swala) na amali zote, na aujaalie mwezi huu mtukufu uwe ufunguo wa kheri na baraka, na tangulizi ya ushindi, utukufu na utawala kwa kusimamishwa Khilafah Rashidah, ili Umma ufunikwe na kivuli cha bendera ya Al-Uqab, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah. Na hilo kwa Allah si jambo gumu:

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo waumini watafurahi. Kwa nusura ya Allah; Hunusuru amtakaye, Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (Ar-Rum [30]: 4-5)

Na mwisho, nawasalimia na kuwaombea kheri, na Allah ndiye Msimamizi wa waumini wanaume na wanawake wema.

Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh

Usiku wa Jumatano, kukamilisha mwezi wa Sha'aban 1439 H Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Sawia na 15/05/2018 M Ameer wa Hizb ut-Tahrir

Share Article

Share this article with your network