Maamuzi ya kiutawala kwetu ni kwamba Wilaya hutangaza vifo vya vijana wake, na Ameer hutangaza vifo vya wajumbe wa Ofisi wa sasa na wa zamani... Na kwa sababu Abu Muhammad "Sabri al-Aruri" ana hadhi kubwa katika dawah hii safi na takatifu, Mwenyezi Mungu akipenda, nimeona kuwa yeye asamehewe (astathniwe) kutokana na maamuzi haya ya kiutawala...
- Kwa hiyo, Ameer na ofisi yake wanatoa rambirambi kwa mtu huyu mkubwa ambaye alikuwa ndani ya dawah hii kama alama maarufu yenye nuru, jabali refu ambalo halishindwi, na nguzo imara katika kupambana na madhalimu asiyedhoofika azma yake, wala halei msimamo wake, na hamuogopi yeyote isipokuwa Allah... na miaka ya kukamatwa kwake mikononi mwa madhalimu inashuhudia hilo, na nina mhesabu kuwa miongoni mwa wale ambao Allah amesema kuwahusu:
مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا
"Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Allah. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi yao wanangojea; wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo." (QS. Al-Ahzab [33]: 23)
Allah (swt) ametaka tutengane kwa miaka kadhaa baada ya kuwa karibu sana tangu nilipohama kutoka eneo la Al-Khalil (Hebron) kwenda Amman kutokana na kazi yangu kama mhandisi katika Wizara ya Kazi za Umma mjini Amman. Anwani ambayo uongozi wa Al-Khalil ulinipa ili nianze kazi yangu ya dawah huko ilikuwa ni anwani ya mtu mwenye nguvu na mcha Mungu, Abu Muhammad, na hatumtakasi yeyote mbele ya Allah. Baada ya hapo, mikutano yetu iliendelea kwa vipindi vya karibu... kisha tukatengana kama nilivyotaja hapo awali kwa miaka kadhaa ambapo hatukuonana ana kwa ana wala hata kupitia mawasiliano isipokuwa mara chache sana...
Siku moja, takriban miezi minne kabla ya kufariki kwake (rehma za Allah ziwe juu yake), niliiona barua kwenye Facebook-Private kutoka kwa ndugu mwema, na hii ndiyo nakala yake:
(Assalamu Alaykum Warahmatullahi Taala Wabarakatuh, hii ni barua kutoka kwa baba Sheikh Sabri al-Aruri kwenda kwa Sheikh wetu Abu Yasin: Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh kaka yangu na mpenzi wangu Abu Yasin... Allah akubalie ibada zako na kila mwaka uwe na kheri, afya, amani na uthabiti... Ndugu yangu, nakuombea dua kwa Allah mchana na usiku akupe mafanikio, hifadhi, amani na usahihi katika mambo na maoni... Allah awe nanyi popote mlipo, Allah akulindeni na atukutanishe nanyi hivi karibuni katika Daulah ya Kiislamu... Ndugu yenu Abu Muhammad Sabri... mwezi wa 9/2016, imepokelewa kupitia ujumbe wa faragha) mwisho.
- Ilikuwa barua tukufu kutoka kwa ndugu mtukufu, hivyo nikamjibu kwenye ukurasa wa Facebook-Private:
(Kwa mtoto wa ndugu mpendwa mtukufu, Sheikh wetu "Abu Muhammad Sabri al-Aruri"...
Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Jazakallahu Khairan ewe Khalid wa kheri, kwani umetuunganisha na mpendwa wetu Sheikh Abu Muhammad. Umetukumbusha historia hiyo nzuri ya mmoja wa watu wakubwa ambaye hakutetereka mbele ya dhiki alizokutana nazo, na zilikuwa nyingi... lakini alibaki imara hata alipokuwa mgonjwa alikuwa mwenye nguvu, na alipokuwa mzima alikuwa mwenye nguvu zaidi... na tunatamani sana kukutana naye chini ya kivuli cha bendera ya Uislamu, bendera ya Mtume wa Allah (saw), tukumbushane siku zile za zamani ambapo Abu Muhammad alikuwa katika kile "duka", ambapo kilikuwa ni mnara kwa vijana waliokuwa wakija kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Ninakumbuka nilipofika Amman ule mkutano mzuri ulionikutanisha naye, akawa msaada kwangu. Allah ambariki yeye na kupitia kwake, na ninaomba kwa Allah (swt) kwamba juhudi zake nzuri alizozitumia katika kubeba dawah na anazozitumia sasa hata akiwa anaugua ugonjwa—Allah amponye na ampe afya—ninaomba kwa Allah juhudi hizo ziwe katika mizani ya mema yake siku ambayo mali wala watoto hawatofaa kitu isipokuwa yule atakayemfikia Allah akiwa na moyo safi... Na ninamuomba (swt) ikiwa haijaandikwa katika kitabu Chake tukutane duniani, basi atukutanishe Akhera pamoja, karibu na Mtume wa Allah (saw) na maswahaba zake katika kiti cha ukweli mbele ya Mfalme Mwenye Uwezo... Ewe Allah, itakabali dua yetu, kwani Wewe ni Msikivu, Mwenye Kujibu.
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh
17 Muharram 1437 H - 18/10/2016 M
Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah) mwisho.
Subhanallah... Nilitamani tukutane duniani bendera ya Khilafah ikituvunika lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu akataka jambo jingine. Namuomba (swt) ajibu dua yangu ya mwisho katika barua yangu iliyotajwa hapo juu (Na ninamuomba (swt) ikiwa haijaandikwa katika kitabu Chake tukutane duniani, basi atukutanishe Akhera pamoja, karibu na Mtume wa Allah (saw) na maswahaba zake katika kiti cha ukweli mbele ya Mfalme Mwenye Uwezo... Ewe Allah, itakabali dua yetu, kwani Wewe ni Msikivu, Mwenye Kujibu).
Allah amrehemu Abu Muhammad na amfufue pamoja na Mitume, Masiddiqi, Mashahidi na Waja wema, na hao ndio marafiki bora... Na nawaombea watoto wake wa kiume na wa kike na wapendwa wake wawe miongoni mwa wale ambao Allah amesema kuwahusu:
الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَواتٌ مِنْ رَبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ
"Wale ambao pindi msiba unapowasibu husema: Hakika sisi ni wa Allah na kwake Yeye tutarejea. Hao ndio wanaopata baraka na rehema kutoka kwa Mola wao, na hao ndio wenye kuongoka." (QS. Al-Baqarah [2]: 156-157)
Allah akurehemu ewe Abu Muhammad, na hakika tunahuzunika kwa kuondoka kwako, na hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu (swt)...
لِلَّهِ مَا أَخَذَ وَلَهُ مَا أَعْطَى، وَكُلُّ شَيْءٍ عِنْدَهُ بِأَجَلٍ مُسَمًّى
"Ni cha Allah kile alichokitwaa na ni Chake kile alichokitoa, na kila kitu Kwake kina muda maalumu uliopangwa."
Na hakika sisi ni wa Allah na Kwake tutarejea.
8 Jumada al-Ula 1438 H
Ndugu yako na rafiki yako
5/2/2017 M
Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah