Home About Articles Ask the Sheikh
Uchumi

Jibu la Swali: Mgogoro wa Kiuchumi wa Kimataifa

January 19, 2013
3911
استمع للمقال

Swali:

Ni wapi umefikia mgogoro wa kiuchumi ulioanzia Amerika na kuisambaratisha Ulaya kisha ulimwengu mzima?

Jibu:

Ili kuangazia mada hii, tunataja yafuatayo:

1- Kuanguka kwa soko la nyumba nchini Marekani kumeenea sehemu zote za ulimwengu, jambo lililosababisha kuporomoka kwa benki nyingi, na kupelekea uingiliaji kati wa serikali ambao haujawahi kushuhudiwa ili kusimamisha anguko la kiuchumi duniani. Pamoja na hayo, matokeo yake yamekuwa kile kinachoitwa sasa mdororo mkubwa wa kiuchumi, ambao ni mbaya zaidi tangu ule wa mwaka 1929. Mgogoro huu wa kifedha wa kimataifa umebainisha ukweli kwamba ukuaji wa kiuchumi wa mwongo uliopita ulikuwa ni matokeo ya madeni. Na huku kufeli kwa mataifa makubwa kiuchumi duniani katika kutatua mgogoro huu, ambao sasa una miaka mitano, kunaendelea!

2- Kumekuwa na majaribio ya pamoja kutoka kwa nchi zenye uchumi mkubwa duniani kwa nia ya kuratibu kazi ili kufikia suluhu la mgogoro huo. Msingi wa uratibu huu ulikuwa ni hoja ya kuunganishwa kwa uchumi wa dunia kutokana na athari za utandawazi, na kwamba mbinu ya pamoja ya kimataifa ingekuwa bora kwa maslahi ya dunia. Lakini mbinu hii ya umoja haikudumu kwa muda mrefu kutokana na kuenea kwa uzalendo wa kiuchumi (economic nationalism) – ambapo kila nchi inapambana peke yake ili kunusurika, kwa sababu kila nchi inatarajia mataifa mengine yatafadhili akiba ya kimataifa. Hilo limeonekana katika mikutano mbalimbali ya nchi za G20 katika majaribio yake ya kufadhili uokoaji wa nchi zenye uchumi ulioporomoka, ambapo matokeo yake ni kwamba miradi mingi ya ufadhili haikuvuka karatasi ilipoandikwa, kutokana na mtazamo wa kizalendo wa kiuchumi wa nchi kubwa. Gazeti la The Economist liliandika mwaka 2010: "Lakini kurejea kwa kivuli cha kipindi cha giza zaidi katika historia ya kisasa kunahitaji jibu tofauti na la dhati. Uzalendo wa kiuchumi unaolenga kulinda fursa za ajira na rasilimali ndani ya nchi umesababisha kugeuka kwa mgogoro wa kiuchumi kuwa mgogoro wa kisiasa na kutishia ulimwengu kwa mdororo. Ikiwa uzalendo wa kiuchumi hautazikwa mara moja, matokeo yatakuwa mabaya sana."

3- Kulitokea mijadala mikali kati ya Wajerumani na Waamerika kuhusu njia bora ya mustakabali wa uchumi wa dunia. Angela Merkel, pamoja na idadi kubwa ya nchi nyingine, waliona kuwa mfano wa ukuaji usio endelevu unaotumiwa na Marekani – ambao ni ukuaji unaochochewa na mikopo (credit) na madeni ya bei nafuu, kulingana na mtazamo wa serikali kutumia fedha kuchochea ukuaji – kuwa ni mfano uliopitwa na wakati. Ama mbinu ya Ulaya ilijikita katika haja ya kudhibiti viwango vya nakisi ya bajeti katika kila nchi kupitia hatua za kubana matumizi (austerity measures). Hatua za kubana matumizi kwa kawaida huchukuliwa ikiwa kuna tishio kwamba serikali haiwezi kutekeleza ahadi zake za kulipa deni. Jambo hili linachukuliwa kuwa ni lengo lenyewe tofauti na ukuaji wa kiuchumi. Kwa kuwepo kwa tishio kwa viwango vya mikopo (credit ratings) vya mataifa mengi yenye uchumi mkubwa duniani, mengi yalielekea kwenye kubana matumizi, yaani kupunguza nakisi ya serikali ili kuridhisha masoko ya kifedha. Tatizo la mbinu ya kubana matumizi ni kwamba sera kama hiyo kwa kweli hailengi kuleta ukuaji, ambao ungezalisha fursa za ajira na kipato katika jamii, na hivyo kupelekea ukuaji wa kiuchumi kwa ujumla, bali inalenga kupunguza deni la serikali.

4- Mbinu ya Marekani ya kutafuta kuchochea ukuaji haikuleta matokeo bora zaidi. Uchochezi huo unahitaji kuongezeka kwa matumizi ya serikali kwa kutumia fedha zilizokopwa kwanza kabisa kutoka nje (kama vile China) kama ilivyo hali ya Marekani, au fedha zinazopumpuliwa na benki kuu kwa kuingiza tu tarakimu kwenye kompyuta. Hatua hizi zote ni za muda mfupi ambazo zinaweza kusogeza uchumi uliokwama kwa muda, lakini si kusaidia ukuaji wa kiuchumi endelevu. Kile kilichofikiwa katika ukuaji kiukweli ni matokeo yaliyopulizwa yanayotokana na hatua za uchochezi ambazo zilokusudiwa athari zake ziwe za muda, na hivyo basi uchochezi ni msaada tu kwa kazi za serikali na sekta ya huduma ambazo huisha pale uchochezi unapoisha, huku ukiacha uchumi wa nchi mara nyingi ukiwa katika hali ile ile uliyokuwa nayo wakati uchochezi ulipoanza.

5- Serikali za Magharibi pia zimeelekea kwenye kile kinachoitwa urahisishaji wa kiasi (Quantitative Easing), ambalo ni maendeleo mapya yaliyotumiwa kama njia ya kielektroniki ya kuchapa pesa. Sera hii isiyo ya kawaida ilitumiwa na benki kuu (yaani serikali) kuchochea uchumi wa kitaifa wakati sera za kawaida zilipofeli. Kulingana na hilo, benki hizi kuu zimekuwa zikitekeleza kile kinachojulikana kama Quantitative Easing au QE kupitia kununua mali za kifedha (Financial assets) kama vile hati za mikopo na hisa... ili kuingiza kiasi fulani cha pesa kilichopangwa mapema kwenye uchumi. Hili hufikiwa kwa serikali kununua mali za kifedha kutoka kwa benki kwa pesa mpya zilizotengenezwa kielektroniki, yaani serikali kulipa bei za mali hizi za kifedha kwa benki kielektroniki na si kihalisia, hivyo hatua hii huongeza akiba ya benki. Pamoja na haya yote, uchumi wa dunia mwanzoni mwa mwaka 2013 si bora kuliko ulivyokuwa mwanzoni mwa mwaka 2012, bali mdororo wa kiuchumi umetafuna mifupa ya baadhi ya nchi zilizokuwa zikijaribu kujiokoa na mdororo kamili. Na hizi hapa ripoti tangu mwanzo wa mwaka 2013 zinazozungumzia kwa nguvu uwezekano wa Uingereza kuingia katika mdororo mkubwa wa kiuchumi kama nchi nyingine za Ulaya zilizoelemewa na madeni ambayo sasa yanahesabiwa kwa mabilioni ya mabilioni ya dola (trillions). Hivyo basi, urahisishaji wa kiasi uliishia kiukweli bila matokeo madhubuti, bali uchumi wa dunia baada ya miaka 5 ya mgogoro wa kiuchumi bado unateseka, hasa kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa ukosefu wa ajira, na tayari machafuko ya kijamii yameanza Ulaya. Majaribio yote ya kutatua mgogoro hayakushughulikia tatizo la ukuaji unaotegemea madeni. Wakati madeni yakiwa ndiyo sababu ya tatizo, majaribio ya kutatua mgogoro hayakuzaa chochote isipokuwa madeni zaidi, na hivyo serikali za Magharibi zilijaribu kumtibu mgonjwa kwa ugonjwa ule ule.

6- Hatimaye, kuna uwezekano wa aina tatu ambao unaweza kupelekea ufufukaji wa kiuchumi, tunazitaja kuanzia ile dhaifu hadi yenye nguvu:

Kwanza ni kwamba mdororo mara mbili (double-dip recession) ugeuke kuwa mdororo mkuu (depression) na kuanguka kwa bei, jambo ambalo hupelekea kushuka kwa bei za mikopo, nyumba, na bidhaa, hivyo kutoa msukumo wa kuanza ukuaji wa kiuchumi unaowakilishwa na urahisi wa kulipa mikopo hii. Uwezekano huu ni dhaifu kwa sababu uchumi wa kirasimali umejengwa kimsingi juu ya mikopo na riba inayotokana nayo, na kushuka kwa bei za mikopo (riba) hakudumu kwa muda mrefu maadamu uchumi wa kirasimali upo.

Uwezekano wa pili ni kwamba China iokoe Magharibi. Biashara kubwa ya China na fedha zake za ziada zimeunganishwa na madeni ya Marekani, Uingereza, na sekta pana za eneo la Euro, na ni madeni makubwa yasiyo endelevu. Itakuwa kwa maslahi ya China kuokoa Magharibi. Hii inamaanisha pia ulimwengu wa Magharibi kulazimika kukubali uongozi wa kimataifa wa China. Lakini suala hapa si kama Magharibi itakubali uokoaji huo, bali ni ikiwa China itachukua sera kama hiyo.

Uwezekano wa tatu: Ni kuchomoza kwa jua la dola ya Khilafah, na kutekelezwa kwa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu, ambapo si dola ya Khilafah pekee itakayofaidika, bali nchi za ulimwengu zinazofanya nayo biashara, jambo ambalo litafanya migogoro kama hii ya kimataifa kutokuwepo au kuwa katika hali inayoweza kudhibitiwa.

Share Article

Share this article with your network