Sifa njema zote ni za Allah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Allah, na jamaa zake na maswahaba zake na waliomfuata, na baada ya hapo:
Kwa Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimu kwa kusema:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ
"Mlikuwa bora ya Umma uliotolewa kwa ajili ya watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Allah..." (QS. Ali 'Imran [3]: 110)
Kwa wabebaji da'wah safi na wacha mungu – na hatumtakasi yeyote mbele ya Allah – ambao husema yaliyo mazuri na kufanya matendo mema, ambapo Allah amewasifu wenye sifa hizi kwa kusema:
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين
"Na ni nani mbora wa kusema kuliko anayemlingania Allah na akatenda mema, na akasema: 'Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu'?" (QS. Fussilat [41]: 33)
Kwa watembeleaji watukufu wa kurasa hizi, wanaozijia kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri zilizomo ndani yake, Allah awalipe kheri...
Kwa hawa wote, nawapa pongezi za Eid al-Fitr, na nakuombeni kwa Allah (swt) akubali saumu zenu na kusimama kwenu usiku (ibada) na awajaalie kuwa miongoni mwa watakaowekwa huru na moto katika mwezi huu mtukufu. Kadhalika namuomba Yeye (swt) kwamba Eid hii iwe ni ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu, ili Eid ijayo ifike tukiwa chini ya kivuli cha Khilafah Rashidah, bendera ya La ilaha illa Allah, Muhammad Rasulullah, na hilo kwa Allah si jambo gumu...
Mwisho, nakupeeni salamu na nakuombeeni kheri, na Allah akubali ibada zenu, na awahifadhi kutokana na kila ubaya, na awalipe kutokana na kila shari:
فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ
"Basi Allah ndiye Mbora wa kuhifadhi, Naye ndiye Mwingi wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote." (QS. Yusuf [12]: 64)
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Usiku wa Eid al-Fitr, 1 Shawwal 1438 H Ndugu yenu Sawia na 25/06/2017 M Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah