Jibu la Swali
Ibn Salman na Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mayahudi
Swali:
BBC News عربي ilitangaza kwenye tovuti yake mnamo Septemba 21, 2023: (Mwanamfalme wa Saudi Arabia alitangaza katika mahojiano na mtandao wa Fox News wa Marekani, yaliyorushwa sehemu yake siku ya Jumatano, kwamba Ufalme huo "unapiga hatua" kuelekea kuanzisha uhusiano wa kawaida (normalization) na Israel. Alisema: "Kila siku tunakaribia zaidi kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel"... Aliongeza kwa kusema "Kuna uungaji mkono kutoka kwa serikali ya Rais Biden kufikia hatua hiyo...") Na kulikuwa na ujumbe wa Kiyahudi ulioshiriki hadharani nchini Saudi Arabia: (Mamlaka za Israel zilielezea furaha yake kwa kuwepo kwa ujumbe wa serikali nchini Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) mjini Riyadh, ikizingatia kuwa ni hatua ya kwanza katika njia ya kuanzisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. France 24, 11/9/2023). Je, Saudi Arabia iko karibu kufuata makubaliano ya khiyana ya Kiarabu na kujenga uhusiano na kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi?
Jibu:
Ili jibu liwe wazi, tunapitia mambo yafuatayo:
Kwanza: Kulingana na habari zinazoenea, wahusika wa mchakato wa kuanzisha uhusiano ni kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi, Saudi Arabia, na Marekani. Kuna ukweli unaohusu pande hizi tatu:
Kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi kinaona kuwa kuanzisha uhusiano wowote na nchi yoyote katika eneo la Kiarabu na Kiislamu ni mafanikio makubwa ya kuimarisha kuwepo kwake na kuifanya kuwa "ya kudumu" kulingana na matamanio yao. Kwa hivyo, serikali zote za dola ya Kiyahudi zinashindana kutafuta upenyo wowote ambao unaweza kuziingiza katika nchi za Kiislamu, haswa za Kiarabu.
Kwa kuwa Saudi Arabia ni moja ya serikali za eneo hilo ambazo hazioni umuhimu wa kupigana na Mayahudi ili kuikomboa Palestina kikamilifu, serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikifanya mawasiliano fulani na kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi kwa muda mrefu lakini kwa siri. Kwa hivyo, Saudi Arabia haipingi kimsingi kuanzisha uhusiano na Mayahudi. Hata mfalme wake wa zamani, Abdullah bin Abdulaziz, ndiye aliyezindua mpango wa khiyana wa Kiarabu mnamo 2002, na Saudi Arabia inatangaza mara kwa mara kushikamana nayo.
Kwa upande wa Marekani, tawala zote za Marekani zimekuwa zikifanya kazi kwa miongo kadhaa kwa ajili ya (amani) kati ya Mayahudi na majirani zao watawala wa Kiarabu ili kuimarisha kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi, kuijumuisha katika eneo hilo, na kuiondolea sifa ya kuwa nchi geni. Hili halina tofauti kati ya vyama viwili vya Marekani (Democratic na Republican).
Pili: Licha ya msingi huu unaoruhusu kuanzisha uhusiano kutoka kwa pande hizi tatu, suala hili lina utata mkubwa wa kisiasa:
Kwa upinzani wake wa wazi dhidi ya makubaliano ya nyuklia na Iran mnamo 2015 na uchochezi wake katika Congress ya Marekani dhidi yake, Netanyahu alichukua msimamo dhidi ya sera ya rais wa Marekani wakati huo, Obama, katika suala la nyuklia ya Iran. Hili lilipelekea kuharibika kwa uhusiano wa dola ya Kiyahudi na chama cha Democratic nchini Marekani. Wakati Rais Trump na utawala wake wa Republican walipoingia madarakani Washington mwanzoni mwa 2017, uhusiano kati ya dola ya Kiyahudi na utawala wa Republican ulipamba moto, ambapo utawala huo uliitambua Quds kuwa mji mkuu wake, ubalozi wa Marekani ukahamishiwa Quds, na pia ukatambua kunyakuliwa kwa milima ya Golan. Wakati utawala mpya wa Democratic chini ya uongozi wa Biden uliporejea madarakani mwanzoni mwa 2021, uhusiano kati ya Tel Aviv na Washington ulirudi kuwa wa baridi. Hata utawala wa Biden ulikataa kumpokea Netanyahu katika Ikulu ya White House hadi hivi karibuni baada ya kupanga upya uhusiano... Moja ya ahadi za uchaguzi za Netanyahu ilikuwa kuanzisha uhusiano na Saudi Arabia, na hivi karibuni imefichuliwa kuwepo kwa mawasiliano halisi kati ya Netanyahu na Ibn Salman (Gazeti la Kiyahudi la "Jerusalem Post" lilisema siku ya Jumatatu, 22/5/2023, kwamba Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu alizungumza kwa simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia mara mbili katika wiki zilizopita... Riyadh iliwasilisha orodha ya madai kwa Israel yanayohusu kadhia ya Palestina... Arabi Post, 23/5/2023)...
Serikali ya sasa ya Saudi Arabia chini ya uongozi wa Ibn Salman inachukuliwa kuwa inayotii zaidi mkononi mwa Marekani baada ya utawala wa Trump kumuondoa kibaraka wa Marekani, Muhammad bin Nayef, mamlakani nchini Saudi Arabia na kumkabidhi mwingine, Muhammad bin Salman. Hii ilikuwa katikati ya mwaka 2017, yaani miezi sita baada ya utawala wa Republican wa Trump kuchukua mamlaka Washington. Kwa hivyo, serikali ya Ibn Salman inatii sana mikononi mwa Marekani, lakini utii wake unategemea zaidi chama cha Republican na kundi la Trump. Kwa sababu hiyo, serikali ya Ibn Salman ilimpa Biden mgongo kwa uchochezi wa siri kutoka kwa kundi la Trump nchini Marekani, na utawala wa Biden ulifanya vivyo hivyo kwake, ambapo Biden alitangaza kuwa hatamsalimia Ibn Salman kwa sababu ya suala la kuuawa kwa Khashoggi.
Utawala wa Biden uliingia madarakani nchini Marekani mwaka 2021 kufuatia mgawanyiko mkubwa nchini humo ambao ulitishia na bado unatishia kupindua maisha yote ya kisiasa nchini Marekani. Vyama viwili vinavyovutana (Democratic na Republican) vimechukua uwanja mpana wa mapambano ya ndani na nje kati yao, kama vile kugawana wafuasi na vibaraka katika uwanja wa kimataifa na kuwatumia kwa maslahi ya upande mmoja dhidi ya mwingine katika mzozo wa ndani wa Marekani. Mfano wa hili ni hatua ya Saudi Arabia kupunguza uzalishaji wa mafuta na Urusi ili kuleta pigo kwa chama cha Democratic nchini Marekani wakati wa uchaguzi wa Congress wa 2022. Pia, matamshi makali yaliyotolewa na dola ya Kiyahudi baada ya Netanyahu kurejea madarakani dhidi ya Marekani kurejea kwenye makubaliano ya nyuklia na Iran ni mambo yanayokinufaisha chama cha Republican na kundi la Trump ili kurejea madarakani tena. Kwa hivyo, utawala wa Biden uling’amua kuwa nyuzi za kuanzisha uhusiano wa Saudi Arabia na dola ya Kiyahudi zimekuwa nje ya mikono yake baada ya Netanyahu kurejea madarakani mwishoni mwa 2022...
Tatu: Marekani imefanya tathmini upya ya uhusiano wake na Saudi Arabia na kuurejesha katika hali ya joto, na pia imeimarisha mawasiliano yake ndani ya kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi lakini kutoka katika kituo cha nguvu. Yote haya yanalenga kushika nyuzi za kuanzisha uhusiano kati ya Saudi Arabia na dola ya Kiyahudi na kuziondoa mikononi mwa chama cha Republican:
Baada ya serikali ya Muhammad bin Salman kukataa ombi la utawala wa Biden mnamo 2022 la kuchelewesha kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mwezi mmoja, utawala wa Biden ulielewa kina cha uhusiano kati ya kundi la Trump na Saudi Arabia. Kwa hivyo, ulianza mara moja kupunguza ukali wa ukosoaji wake dhidi ya Saudi Arabia. Na chama cha Republican nchini Marekani kilikuwa kikimfanyia dhihaka Rais Biden, ambaye msimamo wake wa kutomsalimia Ibn Salman kwa mkono (badala yake alimgonga kwa ngumi), na kukataa mkutano maalum naye (badala yake alikutana naye ndani ya ujumbe wa Saudi Arabia ukiongozwa na Mfalme Salman), ulisababisha ongezeko la bei ya nishati.
Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Jake Sullivan, alitembelea Saudi Arabia na kufanya mkutano wa kirafiki na Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman, na kuanzisha awamu mpya ya uhusiano mzuri wa Marekani na Saudi Arabia baada ya baridi. Hili lilidhihirika kwa kuishukuru nchi hiyo kwa kuwahamisha Wamarekani kutoka Sudan, kushauriana nayo kuhusu maendeleo ya Yemen, na kuipa jukumu kubwa zaidi katika sera ya Marekani na jukumu la kuiunganisha India na ulimwengu... (France 24, 8/5/2023).
Ziara ya Blinken nchini Saudi Arabia (Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, alisisitiza uratibu na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, washirika wa kimkakati. Mawaziri hao wawili walizungumzia wakati wa mkutano huo kurejea kwa Syria katika Jumuiya ya Kiarabu, mgogoro wa Sudan, na faili la kuanzisha uhusiano na Israel... France 24, 9/6/2023).
Kuondoa mivutano kati ya Iran na Saudi Arabia, na maelezo ya hili yalikuja katika jibu la swali (Makubaliano ya Saudi Arabia na Iran) tarehe 1/4/2023. Saudi Arabia inajua kuwa makubaliano haya yana thamani kubwa katika utulivu wa utawala wake, na Marekani ilikuwa ikitangaza kuwa inajua kile ambacho China inafanya na Saudi Arabia na Iran... Pia ilipandisha hadhi ya Saudi Arabia kupitia kuishirikisha katika mazungumzo ya utulivu mjini Jeddah kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) tangu 8/5/2023.
Katika mkutano wa G20 uliofanyika India mnamo 9/9/2023, Saudi Arabia ilijitokeza kama njia ya ardhini kati ya njia za baharini za Mashariki kutoka India na Magharibi kuelekea Ulaya, ikizingatiwa kuwa mhusika mkuu katika ukanda wa kiuchumi wa Biden unaounganisha India na Ulaya kupitia Saudi Arabia na kile kinachoitwa dola ya Kiyahudi. (Saudi Arabia ilikubaliana na India kimsingi kuwekeza takriban dola bilioni 100. Al Jazeera Net, 11/9/2023). Haya yote yanaonyesha kuongezeka kwa ushiriki wa Ibn Salman katika sera za utawala wa Biden ingawa ni utawala wa chama cha Democratic, hata kama hakukata uhusiano na chama cha Republican!
Utawala wa Biden unafanya mazungumzo na serikali ya Ibn Salman kuhusu kuanzisha uhusiano na dola ya Kiyahudi na unazungumzia hilo. Kupitia hilo, unataka kufanya makubaliano yoyote ya amani kati yake na dola ya Kiyahudi yawe mikononi mwake, ili ufaidike nayo katika uchaguzi wa Marekani na usinufaike chama cha Republican na kundi la Trump. Yaani, unabadilisha hasara inayowezekana kuwa nguvu mikononi mwake ili kuitumia mbele ya kundi la ushawishi la Kiyahudi (Jewish Lobby) ili kuwaweka mbali na Trump na chama cha Republican... haswa katika uchaguzi ujao.
Utawala wa Biden unaitia hamu serikali ya Netanyahu kufikia makubaliano ya amani na Saudi Arabia: (Balozi wa Marekani nchini Israel, Thomas Nides, alikuwa amefichua kuwa Marekani inafanya kazi ya kuanzisha uhusiano kati ya Israel na Saudi Arabia. Maafisa wawili wa Marekani waliiambia tovuti ya Axios ya Marekani kuwa Ikulu ya White House inataka kuharakisha kufikia makubaliano kati ya Riyadh na Tel Aviv ndani ya miezi sita hadi saba ijayo, kabla ya Rais Joe Biden kutingwa na kampeni yake ya uchaguzi wa urais. Arabi Post, 23/5/2023). Vyombo vya habari vya Kiyahudi pia vilimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa dola ya Kiyahudi akisema (Israel iko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kufikia makubaliano ya amani na Saudi Arabia. BBC, 22/8/2023).
Lakini Netanyahu anajua kutoka upande wa pili kwamba faili la kuanzisha uhusiano na Saudi Arabia sasa limeshikiliwa kwa kiasi kikubwa na utawala wa Biden, na kwamba hatua katika mwelekeo huu haiwezi kufanywa isipokuwa kupitia utawala wa Biden. Kwa hivyo, Netanyahu alituma ujumbe Washington mnamo 17/8/2023 ukiongozwa na waziri wake anayeaminika zaidi, Waziri wa Masuala ya Kimkakati katika dola ya Kiyahudi, Ron Dermer. Alifanya mazungumzo na maafisa wa Marekani wanaohusika moja kwa moja na faili la Saudi Arabia ambao ni: (Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House, Jake Sullivan, Mshauri Mkuu wa Rais wa Marekani kwa ajili ya Mashariki ya Kati, Brett McGurk, na Mshauri Mkuu wa Rais wa Nishati, Amos Hochstein. Hawa ndio maafisa watatu wa Marekani wanaosimamia juhudi za kidiplomasia zenye lengo la kuanzisha uhusiano kati ya Israel na Ufalme wa Saudi Arabia. BBC, 22/8/2023). Hivyo basi, Netanyahu anaelekea kwa Biden ili kuanzisha uhusiano na Saudi Arabia.
Kisha hatimaye kukawa na tamshi la Ibn Salman lililotajwa katika swali siku ya Jumatano 20/9/2023: (Mwanamfalme wa Saudi Arabia Muhammad bin Salman alitangaza katika mahojiano na mtandao wa Fox News wa Marekani yaliyorushwa sehemu yake siku ya Jumatano kwamba Ufalme huo "unapiga hatua" kuelekea kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel. Mwanamfalme wa Saudi Arabia alisema: "Kila siku tunakaribia zaidi kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel." Mwanamfalme Muhammad bin Salman aliongeza kwa kusema "Kuna uungaji mkono kutoka kwa serikali ya Rais Biden kufikia hatua hiyo. Na kwetu sisi, kadhia ya Palestina ni muhimu sana. Tunahitaji kutatua sehemu hiyo na tuna mazungumzo yanayoendelea hadi sasa. Na lazima tuone yataelekea wapi. Tunatumaini yatafika mahali ambapo yatarahisisha maisha kwa Wapalestina na kuijumuisha Israel katika Mashariki ya Kati"... Kwa upande yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen, alisema siku ya Alhamisi kwamba makubaliano ya mfumo yaliyopatanishwa na Marekani ya kuanzisha uhusiano kati ya Israel na Saudi Arabia yanaweza kuhitimishwa kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao...).
Nne: Inadhihirika kutokana na haya yote kwamba mtawala halisi wa Saudi Arabia, Ibn Salman, hamiliki maamuzi yake mengi. Yeye ni kibaraka anayechezewa kati ya wanachama wa Republican waliomfikisha madarakani Riyadh na wapinzani wao wa Democratic. Anajibu matamanio ya hawa na wale si kwa ajili ya maslahi ya Saudi Arabia, bali kwa ajili ya khiyana na ukibaraka ambao watawala wa Kiarabu na Kiislamu hawajui mipaka yake katika kuwatumikia mabwana zao. Watawala katika nchi za Waislamu wamesahau kuwa Palestina ni ardhi iliyobarikiwa, yenyewe na kile kinachoizunguka:
سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ
"Ametakasika Aliyemchukua mja Wake usiku kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makkah) mpaka Msikiti wa mbali (wa Quds) ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake." (QS. Al-Isra [17]: 1)
Wajibu ni kwa majeshi ya Waislamu kusonga mbele kuikomboa na kuitakasa kutokana na najisi ya Mayahudi, na si Palestina kukabidhiwa kwa Mayahudi katika sinia ya dhahabu ya kuanzisha uhusiano, unyenyekevu, na udhalili! Kwa vyovyote vile, Palestina itarejea ikiwa safi na iliyobarikiwa kama ilivyokuwa kwa panga za majeshi ya Waislamu wa kweli chini ya uongozi wa Khilafah Rashidah. Kundi la Mayahudi na wasaidizi wao litashindwa na watageuza migongo yao, na hofu itajaza mioyo yao hadi mmoja wao ajifiche nyuma ya jiwe ambalo litamfichua zaidi kuliko kumficha!! Na amesema kweli Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ
"Hakika mtapigana na Mayahudi na mtauwaua mpaka jiwe liseme: Ewe Muislamu, huyu hapa ni Myahudi, njoo umuue."
Na katika riwaya nyingine:
هَذَا يَهُودِيٌّ وَرَائِي
"Huyu hapa Myahudi yuko nyuma yangu."
Kwa sanadi hiyo hiyo, imetolewa na Muslim kutoka kwa Ibn Umar... Na huenda ikawa hivi karibuni Mwenyezi Mungu akipenda:
وَيَقُولُونَ مَتَى هُوة قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً
"Na wanasema: Lini hayo? Sema: Huenda yakawa karibu." (QS. Al-Isra [17]: 51)
Na hapo wale waliofanya jinai kwa kuanzisha uhusiano wao na Mayahudi hawatapata chochote isipokuwa udhalili na adhabu kali:
سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ
"Itawasibu wale waliofanya jinai udhalili mbele ya Mwenyezi Mungu na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya." (QS. Al-An'am [6]: 124)
10 Rabi'ul Awwal 1445 H 25/9/2023 M