Home About Articles Ask the Sheikh
Masuala

Tangazo la Msiba na Rambirambi kutoka kwa Amir wa Hizb ut-Tahrir na Mkuu wa Diwan al-Mazhalim kufuatia kifo cha Dkt. Abdul Halim Muhammad al-Ramhi (Abu Imad)

April 02, 2023
2053

**Bismillahir Rahmanir Rahim**

وَمَن يُطِعِ اللّهَ وَالرَّسُولَ فَأُوْلَـئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاء وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَـئِكَ رَفِيقًا

"Na wanaomtii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao watakuwa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao!" (QS An-Nisa [4]: 69)

Amir wa Hizb ut-Tahrir na Mkuu wa Diwan al-Mazhalim (Ofisi ya Malalamiko), kwa imani kamili juu ya qadhwa na qadar ya Allah, wanatangaza kifo cha:

**Dkt. Abdul Halim Muhammad al-Ramhi (Abu Imad)**

Aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84, naye alikuwa mmoja wa wanachama wema na waadilifu wa Diwan (idara), kwa idhini ya Allah. Ameondoka katika dunia hii inayopita na kuhamia katika nyumba ya akhera yenye kubaki, usiku wa Jumapili, tarehe 11 Ramadhani Tukufu 1444 Hijiria, sawia na tarehe 02/04/2023 Miladi.

Allah amrehemu, alikuwa mtu mwenye kusimama imara kwenye haki na hakuivuka, bila kuogopa lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Allah, na hatumtakasi yeyote mbele ya Allah. Alikuwa na uzoefu wa muda mrefu katika kuchunguza kwa kina kila kesi iliyowasilishwa mbele ya Diwan, ambapo yeye na ndugu zake walikuwa wakisimamia uhalisia wa jambo, kuliweka mahali pake, na kulihukumu pamoja na ndugu zake kwa njia ya hukumu ya haki, huku jicho lake likitazama kule, kwenye Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi iliyoandaliwa kwa ajili ya wachamungu. Hakika jicho linatoa machozi na moyo unahuzunika, na hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu, na hakika sisi kwa kuondokewa nawe, ewe mpendwa wetu, tunahuzunika.

Sisi ndani ya Chama, uongozi na vijana, tunamuomba Allah (swt) atupe sisi na familia yake tukufu subira na tulizo, na tuwe kama alivyosema Allah (swt):

الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ

"Wale ambao unapo wafika msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye hakika tutarejea." (QS Al-Baqarah [2]: 156)

Allah akurehemu ewe ndugu mpendwa kwa rehema pana na akwingize katika Pepo zake pana:

فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِنْدَ مَلِيكٍ مُقْتَدِرٍ

"Katika makazi ya ukweli kwa Mfalme Mwenye uweza." (QS Al-Qamar [54]: 55)

Hakika sisi ni wa Allah na kwake Yeye tutarejea.

11 Ramadhani 1444 H Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah Sawia na 02/04/2023 M Amir wa Hizb ut-Tahrir

Share Article

Share this article with your network