Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake, na wanaomfuata, na baada ya hayo...
Kwa wabeba da’wah wapendwa, Mwenyezi Mungu awatukuze kwa utiifu Wake Subhanahu na utiifu wa Mtume Wake Swallallahu Alayhi Wasallam...
Na kwa wageni na watembeleaji wa ukurasa huu watukufu, Mwenyezi Mungu Aliyekwea na Muweza awatukuze kwa Uislamu...
Na kwa Umma mtukufu wa Kiislamu, umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu, unaoamrisha mema na kukataza maovu na kumuamini Mwenyezi Mungu...
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ
"Nyinyi ni umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Mwenyezi Mungu." (QS. Ali Imran [3]: 110)
Kwenu nyote, ninawapongeza kwa Sikukuu ya Idul Fitri, nikimuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu apokee amali njema, saumu na kisimamo cha usiku, na iwe sikukuu hii ni ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu wote, na isifike sikukuu ijayo isipokuwa Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashidah ya Pili, imeshasimama, ambapo kupitia hiyo Waislamu watarejea kuwa watukufu na wenye nguvu kama walivyokuwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu Swallallahu Alayhi Wasallam na zama za Khilafah Rashidah ya kwanza...
Mwenye Nguvu na Mwenye Hikima atawafunika duniani kwa kivuli cha Bendera ya Al-Uqab, bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu Swallallahu Alayhi Wasallam, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na Mwingi wa Rehema na Mwenye kurehemu atawafunika akhera kwa kivuli Chake Subhanahu Siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake... Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Aliye juu ndiye Mlinzi wa watu wema.
Na amani iwe juu yenu na rehma za Mwenyezi Mungu na baraka Zake.
Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah Amir wa Hizb ut-Tahrir