Home About Articles Ask the Sheikh
Siasa

Salaam za Pongezi za Amiri wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wazuruaji wa Kurasa Zake kwa Mnasaba wa Eid al-Fitr ya Baraka

June 03, 2019
3298

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na familia yake, maswahaba wake, na waliomfuata, na baada ya hayo:

Kwa Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu ameuheshimu na kusema juu yake:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

"Mlikuwa bora ya Umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu..." (QS. Ali 'Imran [3]: 110)

Kwa wabebaji wa da’wah, watakasifu na wacha Mungu – na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu – wale ambao wanalingania kwa Mwenyezi Mungu na kufanya vitendo vyema:

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين

"Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu, na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu?" (QS. Fussilat [41]: 33)

Kwa wazuruaji watukufu wa ukurasa huu, wanaouendea kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri iliyobeba ndani yake, basi Mwenyezi Mungu awalipe kheri...

Kwa hawa wote, nawapongeza kwa Eid al-Fitr, na nawaomba Mwenyezi Mungu (swt) akubali saumu zao na visimamo vyao, na awajalie kuwa miongoni mwa walioachwa huru na moto katika mwezi huu mtukufu. Kadhalika, nawaomba Kwake (swt) kwamba Eid hii iwe ni mwanzo wa kheri na baraka kwa Waislamu, na Eid ijayo ifike tukiwa chini ya kivuli cha bendera ya Khilafah Rashidah, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na hilo si jambo gumu kwa Mwenyezi Mungu...

Mwisho, nawapa salamu na kuwaombea kheri, na Mwenyezi Mungu akubali amali zenu, na awahifadhi na kila baya, na awalinde na kila shari.

فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ

"Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kuhifadhi, Naye ndiye Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanaorehemu." (QS. Yusuf [12]: 64)

Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Usiku wa Eid al-Fitr, 1 Shawwal 1440 H Sawia na 04/06/2019 M

Ndugu yenu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network