Home About Articles Ask the Sheikh
Siasa

Pongezi za Amir wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah kwa Wazuruaji wa Kurasa Zake kwa Mnasaba wa Kuingia kwa Eid al-Fitr Iliyobarikiwa ya Mwaka 1439 H - 2018 M

June 14, 2018
3167

Alhamdu Lillahi, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Allah, na jamaa zake na maswahaba wake na waliomfuata, na baada ya hayo:

Kwa Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimu na akasema kuuhusu:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

"Nyinyi mmekuwa bora ya Umma waliofanyiwa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu." (QS. Al-Imran [3]: 110)...

Kwa wabebaji da'wah wasafi na wacha-Mungu - wala hatumtakasi yeyote mbele ya Allah - wale wanaolingania kwa Allah na kufanya vitendo vyema:

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين

"Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu, na akatenda mema, na akasema: 'Hakika mimi ni katika Waislamu'?" (QS. Fussilat [41]: 33)...

Kwa wazuruaji wa ukurasa huu watukufu wanaouelekea kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri iliyobebwa ndani yake, basi Allah awalipe kheri...

Kwa hawa wote, nawapongeza kwa Eid al-Fitr, na namuomba Allah (swt) akubali saumu zao na awajalie kuwa miongoni mwa walioachwa huru na moto katika mwezi huu mtukufu. Kadhalika namuomba (swt) kwamba Eid hii iwe ni ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu, na Eid ijayo ije tukiwa tunajivuli chini ya bendera ya Khilafah Rashidah, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na hilo si gumu kwa Allah...

Mwishoni, ninawatolea salamu na kuwaombea kheri, na Allah akubali amali zenu, na Allah awalinde na kila ubaya, na awahifadhi na kila shari,

فَاللَّه خيرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ

"Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kuhifadhi, naye ndiye Mwenye kurehemu kuliko wote wanaorehemu." (QS. Yusuf [12]: 64).

Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Usiku wa Eid al-Fitr, 1 Shawwal 1439 H Sawia na 15/06/2018 M

Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network