Home About Articles Ask the Sheikh
Masuala

Salamu za Pongezi za Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wageni wa Kurasa Zake kwa Mnasaba wa Eid Al-Fitr ya Mwaka 1444 H / 2023 M

April 20, 2023
1696

Alhamdu lillahi, swala na salamu zimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake na waliofuata uongofu wake, na baada ya hayo:

Kwa Umma wa Kiislamu, Umma bora uliotolewa kwa watu:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

"Nyinyi mmekuwa Umma bora uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Mwenyezi Mungu..." (QS. Ali 'Imran [3]: 110)

Kwa wabebaji da'wah walio safi na wacha Mungu, na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu...

Kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa huu...

Nawapongeza kwa Eid al-Fitr, nikimuomba Mwenyezi Mungu (swt) akubali swaumu, visimamo, na amali zote njema, na atujalie sisi na nyinyi miongoni mwa watakaowachwa huru na moto katika mwezi huu mtukufu... At-Tirmidhi amepokea katika Sunan yake kutoka kwa Abu Hurairah kuhusu masiku ya Ramadhani akisema:

قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «وَلِلَّهِ عُتَقَاءُ مِنَ النَّارِ وَذَلكَ كُلَّ لَيْلَةٍ»

"Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: 'Na Mwenyezi Mungu ana watu anaowaacha huru kutokana na moto, na hilo ni kila usiku.'" (Imepokewa na At-Tirmidhi na Al-Hakim)

Vilevile namuomba Yeye Aliyetakasika kuwa Eid hii iwe ni mwanzo wa kheri na baraka kwa Waislamu, ili Eid ijayo ifike tukiwa chini ya kivuli cha utukufu, ushindi na tamkini, tukijikinga chini ya bendera ya Khilafah Rashidah, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu... Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Hudhayfah bin al-Yaman:

قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» ثُمَّ سَكَتَ

"Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: '...kisha utakuwepo utawala wa kidikteta (wa kulazimisha), utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo, kisha Atauondoa Atakapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume,' kisha akanyamaza." (Imepokewa na Ahmad na At-Tayalisi)

Mwishowe, nawatumia salamu na nawaombea kheri, na Mwenyezi Mungu akubali utii wenu...

Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Usiku wa Eid al-Fitr, 1 Shawwal 1444 H Ndugu yenu,

Sawia na 21/04/2023 M Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network