Kwa Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu... Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimisha kwa kumtii Yeye...
Kwa wabebaji da'wah watukufu ambao biashara wala kuuza hakuwapotezei kumdhukuru Allah...
Kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa huu wanaoelekea kwenye kheri iliyobebwa ndani yake...
Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Nawapongeza kwa mwezi huu mtukufu,
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ
"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi." (QS Al-Baqarah [2]: 185)
Na ni mwezi ambao Allah سبحانه amewaheshimisha Waislamu ndani yake kwa msamaha kama alivyosema Mtume wa Allah ﷺ:
مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ
"Mwenye kusimama (kufanya ibada) Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia." (Imepokelewa na Al-Bukhari kutoka kwa Abu Hurairah)...
Ndani yake iliteremshwa Qur'ani Tukufu, na ndani yake kulikuwa na ushindi na ufunguzi ulio wazi... mwezi wa kazi, bidii na juhudi, na mwezi wa ibada, subira na jihadi... Basi pigeni mbio enyi Waislamu, na shindaneni katika kheri, ambapo thawabu na mema huongezwa maradufu...
Na namuomba Allah سبحانه awakubalie Waislamu wote saumu zao na visimamo vyao, na uwe mwezi huu mtukufu ni ufunguzi wa kheri na baraka, na tangulizi ya ushindi kwa kusimamisha Khilafah Rashidah, ili Umma ujikinge chini ya kivuli cha bendera ya Al-Uqab, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, uree kama ulivyokuwa, Umma mtukufu, wenye nguvu kupitia kwa Mola wake, na wenye izza kupitia dini yake.
وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
"Na siku hiyo waumini watafurahi. Kwa nusura ya Allah; Humnusuru amtakaye, naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS Ar-Rum [30]: 4-5)
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Usiku wa tarehe mosi Ramadhani 1443 H Sawia na 01/04/2022 M
Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah