"Miongoni mwa waumini wapo watu waliotimiza waliyoahidiana na Allah; miongoni mwao wapo waliokamilisha nadhiri zao (wamekufa), na miongoni mwao wapo wanaongoja, wala hawakubadilisha (ahadi yao) hata kidogo." (QS. Al-Ahzab [33]: 23)
Ameer wa Hizb ut-Tahrir anatangaza kwa Waislamu kwa ujumla na kwa shabab wa Hizb ut-Tahrir hususan, kifo cha ndugu mtukufu ambaye tulimpoteza alfajiri ya Alhamisi, tarehe 18/05/2023 nchini Australia...
Marehemu (Mwenyezi Mungu amrehemu) alikuwa miongoni mwa nguzo za Hizb, alikuwa mjumbe katika Ofisi ya Ameer, mwenye uzoefu wa muda mrefu katika kupinga dhuluma na msimamo thabiti juu ya haki, bila kutikiswa na matatizo, mitihani, wala jela za mataghuti na kuteswa kwao, badala yake alizidi kuongezeka nguvu juu ya nguvu, akifanya kazi kwa ukweli na ikhlasi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu...
Macho yake hapa duniani yalikuwa yakitazama bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ ikipaa juu kutoka kilele kimoja hadi kilele kingine... Na huko Akhera kama Alivyosema Yeye (Mwenyezi Mungu) Subhanahu:
"Hakika wachamungu watakuwa katika Bustani na mito. Katika makao ya kweli kwa Mfalme Mwenye uweza." (QS. Al-Qamar [54]: 54-55)
Mwenyezi Mungu amrehemu ndugu yetu na amuingize katika Pepo Yake pana, na amfufue pamoja na Mitume, Masiddiqi, Mashahidi na Waja wema, na hao ndio marafiki bora kabisa... Tunamuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu, kwa ajili yetu na familia yake na Waislamu wote, tuwe kama alivyosema Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu:
"(Wale) ambao unapo wafika msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema, na hao ndio wenye kuongoka." (QS. Al-Baqarah [2]: 156-157)
Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Abu Anas, rehema pana... na wala hatusemi ila yale aliyoyasema (Mtume ﷺ) Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alipompoteza mwanawe na kipenzi cha jicho lake, Ibrahim (Amani iwe juu yake):
"Hakika jicho linatoa machozi, na moyo unahuzunika, na wala hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu, na hakika sisi kwa kutengana nawe, ee Ibrahim, tuna huzuni."
Mwenyezi Mungu akurehemu ewe Abu Anas.. Ewe rafiki yetu na mwenza wetu wa njiani.. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea.
Ndugu yako na rafiki wa njia yako, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah
Ameer wa Hizb ut-Tahrir
28 Shawwal 1444 H Inayoendana na 18/05/2023 M