Home About Articles Ask the Sheikh
Siasa

Salamu za Pongezi za Ameer wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashta kwa Mnasaba wa Kuwadia kwa Idul Adh'ha ya Mwaka 1439 H sawia na 2018 M

August 20, 2018
5082
استمع للمقال

Salamu za Pongezi za Ameer wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashta Kwa mnasaba wa kuwadia kwa Idul Adh'ha ya mwaka 1439 H sawia na 2018 M Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La ilaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, wa lillahi al-hamd

Ameer

Kwa Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu ameuakifu kwa kusema:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

"Mlikuwa bora ya Umma waliofanyiwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu..." (QS. Al-Imran [3]: 110)

Kwa wabeba dawah, vijana wa kiume na kike wa Hizb ut Tahrir, watu wasafi na wacha Mungu – na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu – wale ambao husema kauli nzuri na kufanya vitendo vyema, na Mwenyezi Mungu akawasifu wenye sifa hizi:

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين

"Na ni nani mbora wa kusema kuliko anayemlingania Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu?" (QS. Fussilat [41]: 33)

Kwa wageni watukufu wa ukurasa huu, wanaoufuatilia kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri iliyobeba ndani yake, Mwenyezi Mungu awalipe kheri...

Kwa hawa wote: Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh, Nawapongeza kwa Idul Adh'ha njema na yenye baraka, na Mwenyezi Mungu apokee amali zenu... Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) apokee Hija za mahujaji na aijaalie kuwa ni Hija yenye kukubaliwa (Hajjan Mabruran), juhudi zenye kushukuriwa, na madhambi yenye kusamehewa. Na Mwenyezi Mungu awawafikishe wale ambao hawakuhiji mwaka huu waweze kuhiji mwaka ujao kwa kheri na katika hali ya kheri, na Mwenyezi Mungu ndiye Msimamizi wa watu wema.

Enyi ndugu, Idd inakuja mwaka huu huku Khilafah yetu bado haijakuwepo, hivyo makafiri wakoloni na vibaraka wao wametuandama kwa kuanzisha mauaji na kumwaga damu katika nchi zetu. Jinai zao za kikatili zimetofautiana, kuanzia mabomu ya mapipa hadi makombora yenye kuharibu na silaha za kemikali... Yote hayo ni kwa mikono yao mara nyingine na kwa mikono ya vibaraka wao mara nyingine. Kila unapotazama, unakuta damu za Waislamu zikimwagwa kwa dhuluma na uadui... Mashariki kuna Burma, na nani akwambiaye Burma ni nini, hali ya Waislamu huko inahuzunisha moyo kutokana na jinai za Mabudha na ukatili wao ambao hata wanyama wa mwituni hawaufanyi... Kisha unaona Kashmir na jinai za India huko... Ukipanda kaskazini unaona Chechnya, Caucasus, na kisha Crimea zikiangamizwa na mikono ya Urusi iliyozama katika jinai na damu... Ukielekea mashariki kuelekea Turkestan Mashariki, utaiona China ikiwafanyia kila aina ya uadui... Na ukielekea kusini na kugusa pwani ya bahari, utakuta moyo wa nchi za Waislamu, Ardhi Iliyobarikiwa, Palestina, Kibla cha kwanza, na utawaona Mayahudi wakiikalia kwa nguvu na kufanya humo jinai na mauaji, na kusikia kilio cha msikiti wake (Al-Aqsa) ukipiga kite kutokana na kidonda kirefu kinachokaribia kuufanya uwe katika pumzi za mwisho... Kisha Ash-Sham, na nani akwambiaye Ash-Sham ni nini, damu inatiririka humo kila upande, mauaji ya kikatili yamesambaa mitaani na vichochoroni kwa mkono wa mtawala dhalimu wa Sham, na nyuma yake na mbele yake kuna Amerika, na wafuasi na washirika kutoka Urusi hadi Iran kisha makundi ya wanamgambo (militias)... Na hawa wote wanawasha moto huu wa mauaji na umwagaji damu kwa kutumia kila aina ya silaha za maangamizi... Na hapa kuna mauaji ya Idlib yanachungulia kupitia mashambulizi ya kikatili pande zote, na mkusanyiko wa madhalimu wanaoelekea huko, ukichanganywa na mikataba ya usaliti pembezoni mwake... Kisha Iraq, dada wa Sham katika majanga na misiba... Ukielekea kusini hadi Yemen ambayo ilikuwa na furaha, utaiona imekuwa na huzuni ikiangamizwa na majanga ya mapigano, ikichochewa na nchi kafiri za kikoloni ambazo zimeifanya Yemen kuwa uwanja wa ushindani kati yao juu ya mafuvu na damu zetu... Na ukielekea upande wa machweo ya jua, utaikuta Libya ambako Waislamu wanauana wao kwa wao... Kisha ukipitia Afrika ya Kati, utaona Waislamu huko wamepatwa na maumivu, madhara, kumwagwa kwa damu takatifu, na kuvunjiwa heshima kwa kiwango ambacho maelezo hayawezi kukielezea... Kisha jirani yake Sudan, ambayo kusini yake imetenganishwa na kaskazini yake, na kidonda chake kuachwa kikitiririka damu... Kisha Somalia inayolia kwa maumivu makali na mapigano ya kikatili tangu miaka mingi...

Majanga hayo yote yako katika nchi za Waislamu ambazo zilikuwa na utukufu katika miaka ya nyuma kupitia Uislamu, bendera ya Uislamu, Adhana ya Uislamu, na uadilifu wa Uislamu... Lakini baada ya kuondoka kwa Khilafah na kuondoka kwa Imam ambaye ni ngao (Junnah), hali imebadilika na Umma umeonja machungu ambapo makafiri wakoloni na vibaraka wao watawala madhalimu wamevamia... Isitoshe majanga ya Waislamu katika nchi za kikafiri ni makubwa zaidi, kwani mataifa hayo yanataka Waislamu waache utambulisho wao; mavazi ya wanawake wao wanayawekea vizuizi, sauti ya adhana yao wanajitahidi kuinyamazisha, na wanaeneza chuki dhidi yao katika jamii zao na nyanja za maisha hata barabarani... Haya ni majanga tangu kutoweka kwa Khilafah, moja likifuatiwa na jingine, misiba iliyorundikana inayomfanya hata mwenye hekima abaki na mshangao...

Enyi ndugu, majanga haya lau yangelipata umma mwingine wowote, ungelisambaratika au kukaribia kusambaratika, na ungelikata tamaa na kuendelea kwa maisha... Lakini Umma wa Kiislamu unao mwongozo katika Kitabu cha Mola wake, Sunnah za Mtume wake, na hata katika alama za uumbaji kama usiku na mchana, mambo ambayo yanaufanya usitikisike katika dhiki wala azma yake isilegee katika migogoro, bali huongezeka nguvu juu ya nguvu na azma juu ya azma... Unatekeleza kazi yake kwa nguvu na ubora na kuelekea kwa Mola wake kwa kumtegemea kwa ukweli:

  • Ama katika Kitabu cha Mola wake, Aya za Mwenyezi Mungu zinasema hivyo:

فإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا * إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا

"...Basi kwa hakika pamoja na uzito kuna wepesi. Hakika pamoja na uzito kuna wepesi." (QS. Ash-Sharh [94]: 5-6)

حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ

"Hata Mitume walipokata tamaa na wakaona kuwa walikadhibishwa, msaada Wetu uliwafikia, tukaokoa tuliowataka. Na adhabu Yetu haitarudishwa kutoka kwa watu wahalifu." (QS. Yusuf [12]: 110)

أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُمْ مَثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلِكُمْ مَسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ نَصْرُ اللَّهِ قَرِيبٌ

"Je, mnadhani kuwa mtaingia Peponi, na bado hayajakufikieni kama yaliyowafikia wale waliopita kabla yenu? Walipatwa na dhiki na madhara na wakatikiswa mpaka Mtume na wale walioamini pamoja naye wakasema: Ni lini msaada wa Mwenyezi Mungu (utafika)? Jueni kuwa msaada wa Mwenyezi Mungu uko karibu." (QS. Al-Baqarah [2]: 214)

  • Na ama katika sira ya Mtume wake, ni yale yaliyomfika Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambapo ulikuwa Mwaka wa Huzuni, akafariki Khadija Mama wa Waumini (ra), kisha kufuatiwa na kifo cha Abu Talib aliyekuwa akimsaidia Mtume (saw), na baada ya hapo upinzani mkali kutoka kwa watu wa Taif uliomfanya Mtume (saw) avuje damu... Kisha hali ikawa ngumu zaidi, wakakubaliana kumuua Mtume (saw), kisha wakamfuata (saw) hadi katika pango la Thawr, akiwa amejificha humo na rafiki yake Abu Bakr as-Siddiq (ra). Walisimama mbele ya mlango wa pango na hapakuwa kati yao na Mtume (saw) isipokuwa dhiraa moja au sehemu ya dhiraa... Hiyo ilikuwa jioni ya siku hiyo, na baada ya hapo kwa siku moja au mbili Mtume (saw) alikuwa akisimamisha Dola mjini Madina na kuinua jengo lake, dunia ikang'ara na akatangaza ukweli...

  • Na ama katika alama za uumbaji kama usiku na mchana, hakika kuzidi kwa kiza cha usiku hufuatiwa na kuchomoza kwa alfajiri ya kweli, na hiyo ni ishara kwa wenye akili...

Hivyo basi, Umma wa Kiislamu haukati tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, na unatambua kuwa wepesi unakuja baada ya uzito, na faraja baada ya dhiki, na kuchomoza kwa alfajiri baada ya kiza cha usiku... Hivyo haushitushwi na misukosuko bali unafanya kazi na unaendelea kufanya kazi kwa ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu na ukweli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu... Wala haudhuriwi na yule anayegeuka miongoni mwao au kupotea, kwani wengi wao hawakuridhii mbadala wa Uislamu...

Enyi ndugu, makafiri hao wamepata nafuu baada ya kutoweka kwa Khilafah, hivyo wakafanya jinai zao hizo wakiwa salama, hakuna anayesimama mbele yao, wala anayewazuia jinai zao, wala anayewarudisha katika makazi yao... Wanaelewa kuwa ngao ya Waislamu imetoweka, na hivyo wanafanya kila juhudi ili ngao hiyo isirudi. Na kwa sababu wanatambua kuwa mtengenezaji wa ngao hii ni Khilafah ambapo ndipo penye utukufu wa Waislamu na kinga yao, ndiyo maana wanawawinda wanaofanya kazi ya kurejesha Khilafah... Hivyo, Hizb ut Tahrir imekuwa lengo la mishale ya makafiri wakoloni na vibaraka wao watawala katika nchi za Waislamu. Kutokana na hilo, Hizb imekumbana na kila aina ya bughudha na mateso yanayopelekea ushahidi kutokana na hila za makafiri, majasusi wa madhalimu, na chuki za wenye chuki... Hizb imepigwa marufuku na kuzuiwa katika nchi za ulimwengu wa Kiislamu, hata katika nchi zile zilizofunguliwa kwa vyama vya kila namna kama Indonesia, Hizb imezuiwa! Na pia katika nchi zile ambazo milango yake iko wazi kwa vyama vya aina zote hata vile dhaifu kama Tunisia, pia Hizb imezuiwa... Ama vijana wa Hizb, magereza ya matwaghuti yanazungumza hali yao; katika magereza yao finyu wanateswa, na katika magereza mapana (nje ya jela) wanawindwa. Na sababu ya yote haya ni neno la haki ambalo Hizb inalitangaza, ambalo linawashitua zaidi ya mapigo ya panga, kwani hawana hoja inayoweza kusimama mbele ya neno la haki. Mwenyezi Mungu awaangamize, vipi wanageuzwa?

Enyi ndugu: Hakika majanga haya yanayousibu Umma na wale wanaofanya kazi kwa ajili ya Khilafah ni makali sana. Lau si kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ameifanya Idd kuwa ni chanzo cha furaha, na kuingiza katika nyoyo za Waislamu mchangamko na furaha, na kuunga vyema udugu, na Umma ueneze kati yake salamu na pongezi njema... Na lau si kwamba ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ya utukufu na tamkin inakuja kwa Umma huu... Na lau si kwamba kuna bishara kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ya kurejea kwa Khilafah Rashidah... Na lau si kwamba kuna chama chenye ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu (swt), kikweli kwa Mtume wake (saw), kikifanya kazi usiku na mchana kikiomba kwa Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu akifungulie kwa mikono yake kusimamisha Khilafah na kurejesha utukufu wa Uislamu na Waislamu... Lau si kwa haya manne, tabasamu lingeacha kuonekana nyusoni, kwani moyoni kuna kidonda, na kooni kuna uchungu, kutokana na wingi wa majanga yanayowazunguka Waislamu mbele na nyuma, kulia na kushoto... Kwani Khilafah haipo kwa takriban karne moja, hivyo Waislamu wamekuwa vipande vilivyofarakana, wakitawaliwa na watawala ruwaibidhah madhalimu... Isitoshe uadui wa makafiri wakoloni na washirika wao dhidi ya nchi na watu, kana kwamba nchi za Waislamu ni uwanja wa mapambano wa kumwaga damu zetu na kuvunja heshima zetu...

Lakini, pamoja na ukali wa majanga haya, Hizb ut Tahrir ina utulivu na ushindi wa Mwenyezi Mungu na utimilifu wa ahadi Yake (swt) na bishara ya Mtume Wake (saw). Hivyo Hizb haikati tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu maadamu inaboresha kazi yake kwa idhini ya Mola wake. Hizb inatambua kuwa wakati wa kurejea kwa Khilafah umeandikwa katika Kitabu, na kila siku inayopita tunakaribia wakati huo kwa siku moja. Na chama chenye sifa hii hakiruhusu kukata tamaa kuingia moyoni mwake, wala azma yake hailegei wala nguvu yake haidhoofiki kwa idhini ya Mwenye Nguvu, Mwenye Hekima. Bali misukosuko huizidisha nguvu, kwani misukosuko ndiyo kipimo cha wanaume, na vijana wa Hizb ni wanaume kwelikweli ambao wanamuomba Mwenyezi Mungu (swt) wawe miongoni mwa wale ambao Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu:

رِجَالٌ لَا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ

"Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Swala, na kutoa Zaka. Wanaiogopa siku ambayo nyoyo na macho yatageuka." (QS. An-Nur [24]: 37)

Wanabeba dawah kwa mikono yao ya kulia kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, na dawah hii itanyanyuka kupitia mikono yao InshaAllah, na kisha ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara ya Mtume Wake (saw) itatimia katika sehemu zake tatu kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu na msaada Wake:

- Ya kwanza: Katika kurejesha Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala huu wa mabavu (mulkan jabriyan): Imam Ahmad na Al-Tayalisi katika Musnad yake wamepokea kutoka katika hadith ya Hudhayfah, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: "...kisha utakuwepo utawala wa mabavu, utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo, kisha Atauondoa Atapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume."

- Ya pili: Katika kuung'oa utawala wa Mayahudi kutoka katika mizizi yake. Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: "Haitafika Saa mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, Waislamu watawaua...", na katika tamko jingine (saw) amesema: "Mayahudi watapigana nanyi, na nanyi mtapewa mamlaka juu yao."

- Ya tatu: Katika kufunguliwa kwa Roma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Ahmad amepokea katika Musnad yake na Al-Hakim na akaisahihisha na kumpandisha daraja Al-Dhahabi kutoka kwa Abu Qabil, amesema: Tulikuwa kwa Abdullah bin Amr bin al-Aas, akasema: Wakati tukiwa tumemzunguka Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) tukiandika, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akaulizwa: Ni mji gani kati ya miji miwili utafunguliwa kwanza: Constantinople au Roma? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: "Mji wa Herakulu utafunguliwa kwanza, yaani Constantinople." Na Constantinople ilishafunguliwa, na Roma itafunguliwa InshaAllah...

Enyi ndugu, katika kutafakari yaliyoandikwa hapo juu kwa akili timamu na ufahamu wa busara, kuna matumaini baada ya maumivu, na bishara ya furaha baada ya uhalisia wa huzuni, na wepesi baada ya uzito, na raha iliyokaribia baada ya mashaka yaliyochukua muda mrefu, na kuteremka kwa rehema za Mwenyezi Mungu baada ya Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un... Kisha kheri na ushindi... Kheri na ushindi... Kheri na ushindi.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّ الرحيمُ

"Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu; Humsaidia Amtakaye, Naye ni Mwenye Nguvu, Mwenye kurehemu." (QS. Ar-Rum [30]: 4-5)

Mwisho, namuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuwa Idd hii njema na yenye baraka irejee huku Umma wa Kiislamu ukijivuli kwa bendera ya Khilafah Rashidah, bendera ya al-Uqab, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah... Kadhalika namuomba Yeye Aliyekweka juu, vijana wa Hizb wawe mstari wa mbele wa Umma huu wakijivuli pamoja nao katika kivuli cha Khilafah Rashidah... Na ama kijana ambaye Mwenyezi Mungu atamfanyia muda wake ufike kabla ya kurejea kwa Idd hii, basi namuomba Mwenyezi Mungu (swt) apate kivuli Chake siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Na hatima ya mwisho, nakupeeni salamu na nakuombeeni kheri.

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh

Ndugu yenu Katika usiku wa tarehe kumi ya Dhul-Hijjah 1439 H Ata Bin Khalil Abu al-Rashta Sawia na 21/08/2018 M Ameer wa Hizb ut Tahrir

Share Article

Share this article with your network