Home About Articles Ask the Sheikh
Masuala

Salamu za Pongezi za Amir wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah kwa Wazuruaji wa Kurasa Zake kwa Mnasaba wa Idul Adh'ha 1444 H - 2023 M

June 27, 2023
2271

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na waliomfuata na baada ya hayo...

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, la ilaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, walillahi al-hamd...

Kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla... Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu, unaoamrisha mema na kukataza maovu na kumuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima...

Kwa wabebaji da'wah hasa... Mwenyezi Mungu afungue kheri kupitia mikono yao, na awaididie kwa msaada Wake ili wasimamishe Dola ya Kiislamu; Khilafah Rashida kwa misingi ya Utume...

Kwa wazuruaji wa kurasa watukufu wanaoelekea kwenye kheri inayobebwa... wanaojitahidi kusimama upande wa haki na kuwanusuru watu wake...

Kwa hawa wote... Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Nawapongeza kwa sikukuu tukufu ya Idul Adh'ha... na namuomba Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye utukufu, iwe ni mwanzo wa kheri na baraka kwa Waislamu wote...

Ndugu watukufu... nawasalimia na kuwaombea kheri, na namuomba Mwenye nguvu na utukufu aondoshe dhiki ya majanga na maradhi kwa Waislamu wote, na mwezi huu mtukufu uwe mwezi wa mwisho unaowapitia Waislamu bila ya kuwa na dola inayoutukuza Uislamu na watu wake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.

Mwenyezi Mungu akubali amali zenu na awajalie miongoni mwa wale ambao Yeye Subhaanahu amesema kuwahusu:

رِجَالٌ لَّا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَن ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ ۙ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ * لِيَجْزِيَهُمُ اللَّهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ

"Watu ambao biashara wala kuuza hakuwapotezei kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaogopa siku ambayo nyoyo na macho yatageukageuka. Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yafanya, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu." (QS An-Nur [24]: 37-38)

Ndugu yenu

10 Dhul-Hijjah 1444 H                                               Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Sawia na 28/06/2023 M                                               Amir wa Hizb ut-Tahrir

Share Article

Share this article with your network