Home About Articles Ask the Sheikh
Siasa

Salamu za Pongezi za Amir wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah kwa Wazuruaji wa Kurasa Zake kwa Mnasaba wa Eid al-Fitr ya Mwaka 1441 H Unaoafikiana na 2020 M

May 23, 2020
3598

Kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla... Mwenyezi Mungu awape ushindi dhidi ya adui zao, na awawajibishe kwa neno la ucha-Mungu, kwani wao ndio wanaostahili zaidi na wenye sifa nalo...

Kwa wabebaji da'wah mahususi... Mwenyezi Mungu afungue kupitia mikono yao, na awaayidi kwa msaada Wake ili wasimamishe Dola ya Kiislamu; Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume...

Kwa wazuruaji wa ukurasa watukufu wanaoelekea kwenye kheri unayobeba... wanaotumia jitihada zote kusimama kwenye haki na kuwanusuru watu wake...

Kwa hawa wote... Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Nawapongeza kwa Eid al-Fitr, na nakuomba Mwenyezi Mungu (swt) iwe ni mwanzo wa kheri na baraka kwa Waislamu wote, ili Umma wao urejee kuwa umma bora uliotolewa kwa watu, na hilo ni kwa kusimamisha dola yao, Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, ili Mwenyezi Mungu aondoe dhiki zao, na awarejeshee utukufu wao.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo waumini watafurahi, kwa nusura ya Mwenyezi Mungu. Humunusuru amtakaye, Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS. Ar-Rum [30]: 4-5)

Kadhalika nakuomba Yeye (swt) aondoe dhiki ya balaa na janga la maradhi kwa Waislamu wote, na iwe ni utangulizi wa ushindi na ufunguzi ulio wazi, na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu.

Na mwisho, nawasalimia na nawaombea kheri, na nakuomba Mwenye Nguvu, Mtukufu, kwamba mwezi huu mtukufu uwe ndio mwezi wa mwisho wenye baraka kupita kwa Waislamu pasina kuwa na dola inayoutukuza Uislamu na watu wake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikma.

Na Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Siku ya Eid al-Fitr, 1 Shawwal 1441 H                                          Ndugu yenu

Unaoafikiana na 23/05/2020 M                                                   Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network