Home About Articles Ask the Sheikh
Siasa

Salaam za Pongezi za Ameer wa Hizb ut-Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, kwa Wageni wa Kurasa Zake kwa Mnasaba wa Kuwadia kwa Eid al-Fitr ya Baraka kwa Mwaka wa 1442 H sawia na 2021 M

May 14, 2021
2230

Alhamdullilah, swala na salamu zimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba zake, na wale wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kwa Umma wa Kiislamu, umma bora uliotolewa kwa watu:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

"Nyinyi mmekuwa umma bora uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu..." (QS. Ali-Imran [3]: 110)

Kwa wabeba da’wah walio safi na wachamungu, na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu...

Kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa huu...

Nawapongeza kwa Eid al-Fitr, nikimuomba Mwenyezi Mungu (swt) akubali saumu, kisimamo cha usiku, na matendo yote mema, na atujalie sisi na nyinyi miongoni mwa watakaokombolewa kutokana na moto katika mwezi huu mtukufu...

At-Tirmidhi amepokea katika Sunan yake kutoka kwa Abu Hurairah kuhusu masiku ya Ramadhani akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

وَلِلَّهِ عُتَقَاءُ مِنْ النَّارِ وَذَلكَ كُلُّ لَيْلَةٍ

"Na Mwenyezi Mungu ana watu wanaokombolewa kutoka Motoni, na hayo ni kila usiku." (Imepokelewa na At-Tirmidhi na Al-Hakim katika Mustadrak yake).

Pia namuomba Yeye (swt) kwamba Eid hii iwe mwanzo wa kheri na baraka kwa Waislamu baada ya utawala huu wa kidikteta (mulkan jabriyyatan) ambao tumeishi ndani yake kwa muda wa miaka mia moja, na ifike Eid ijayo huku tukiwa tumetulia chini ya kivuli cha bendera ya Khilafah ya Rashidah, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu... Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Hudhayfah bin al-Yaman kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ

"...Kisha utakuwepo utawala wa kidikteta, utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo, kisha Atauondoa atakapotaka Kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume." Kisha akanyamaza. (Pia imepokelewa na At-Tayalisi katika Musnad yake).

Mwisho, nawasalimu na kuwaombea kheri, na Mwenyezi Mungu akubali matendo ya utiifu...

Wasalaam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Siku ya Eid al-Fitr, 1 Shawwal 1442 H Ndugu yenu

Sawia na 13/05/2021 M Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah

Share Article

Share this article with your network