Takriban miaka miwili iliyopita, mtu mmoja aliniambia kuwa kuna mtu anayefanya kazi na mashetani wa kijini ambao walimwambia kuwa Amir wa Hizb ut-Tahrir, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, ataondolewa madarakani hivi karibuni... Baada ya kupita takriban miaka miwili tangu kauli hiyo na Amir hajaondolewa, huyo mwenye majini akaona aunganishe pia mashetani wa kibinadamu ili mashetani wa pande zote mbili washirikiane kutimiza kazi hiyo... Hapo ndipo wafuasi na mashabiki miongoni mwa wanaovunja ahadi (nakithin), waachaji, na wale ambao nyoyo zao zina maradhi, walianza kuandika kwenye mtandao wa intaneti kwa majina ya bandia hapa na pale. Mara wanaandika kwa jina la Al-Amin, mara nyingine Al-Mansur, kisha Al-Muntasir, kisha wanamalizia kwa jina la sheikh wao wanayemdai "Al-Jawwal"... n.k., ili waonekane kana kwamba ni kundi lenye idadi kubwa inayozingatiwa... nao ni kama yule aliyesemwa hivi kumhusu:
Kama ungekuwa miongoni mwa watu wanaostahili kudhihakiwa, ningekudhihaki, Ewe mwana wa Riqaa, lakini wewe si lolote.
Walikuwa wakimhutubia Ata bin Khalil Abu al-Rashtah katika barua zao tatu za kwanza kama Amir wa Hizb ut-Tahrir... Inaonekana huyo mwenye majini hakuweza kusubiri zaidi, akataka kumwondoa Amir mara moja... Kwa hivyo, barua ya nne ilitoka ikiwa na kichwa cha habari "Kwa Ata bin Khalil Abu al-Rashtah, Amir wa zamani wa Hizb ut-Tahrir"... Kisha akaongeza kuwa mashetani wa kijini walimbeba hadi nyumbani kwangu ambako nimejificha, na huko, kama alivyosema, alinikuta nikiwa "donge la nyama na mifupa lililotupwa sakafuni, nisiyezungumza neno lolote isipokuwa mtetemo mkali uliokuwa ukinipata ukiashiria hofu na kihoro changu kikubwa, na sikuweza kuzungumza kwa sababu sikuwa na nguvu tena ya kusema...". Hivyo ndivyo alivyodai!!
Hakika haya yote si geni kusemwa na watu duni, lakini nimesimama kwenye masuala mawili:
Kwanza: Ni vipi huyo mwenye majini hakuanguka akiwa amebebwa mgongoni mwa shetani wake kwa umbali mrefu hadi akafika nyumbani kwangu kule mbali... nchini Lebanon kama walivyosema...?!
Pili: Anasema kuwa alinijia nyumbani kwangu ambako nimejificha... na mafunuo yake ni kwamba nyumba hiyo iko katika handaki (sardab) inayofaa kwa kujificha, sasa ni vipi alishuka ngazi za handaki hiyo akiwa mgongoni mwa shetani wake na kichwa chake kisigongane na ukuta wa ngazi za handaki hilo?!
Na hivi ndivyo inavyosemwa, "Ishi Rajab uone maajabu", na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada...
Na kwa kuhitimisha, hakika huyo mwenye majini atakuja kugundua kuwa mashetani wake hawakumsaidia na hawatamsaidia, na hawatamtimizia anayoyatamani. Mashetani hao watamzidishia majuto tu, kwa sababu shetani wao mkuu hakunufaisha wale waliohadaika naye, na hakuwatimizia walioyatamani, bali aliwazidishia majuto:
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
"Na shetani atasema mambo yatakapo kwisha: 'Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nilikuahidini, lakini nikakuvunjieni ahadi yangu. Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu, isipokuwa niliwaiteni nanyi mkanitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa msaidizi wenu, wala ninyi hamwezi kuwa wasaidizi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha kwenu na Mwenyezi Mungu.' Hakika madhalimu wana adhabu kali." (QS Ibrahim [14]: 22)
Na Amir wa Hizbi atabaki, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kama mti wa miiba katika koo la huyo mwenye majini na mashetani wake wa kibinadamu na wa kijini, na Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Mtukufu ndiye mlinzi wa waja wema...
- Na tamati ya mwisho kwa Shabab wa Hizbi wacha-Mungu walio safi – na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu – na kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa huu:
Msishughulishwe na barua hizo chafu na duni, zikanyageni kwa miguu yenu, na zitupeni mbali kama mnavyotupa kokwa ya tende. Wala msiniletee tena kuanzia leo kitu chochote katika maandishi kama hayo, kwani ni duni mno kudhuru da'wah au viongozi wake au watu wake. Kuweni na yakini na jueni kuwa:
إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ
"Hakika Mwenyezi Mungu huwalinda walioamini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini anayekufuru." (QS Al-Hajj [22]: 38)
Tisa ya Dhu al-Qi'dah 1438 H Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah 01/08/2017 M Amir wa Hizb ut-Tahrir