Sifa zote njema ni za Allah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Allah, jamaa zake, masahaba zake na waliomfuata, na baada ya hayo:
Kwa Umma wa Kiislamu, umma bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللهِ
"Mlikuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu." (QS. Al-Imran [3]: 110)
Kwa wabebaji da'wah, safi na wacha Mungu "na hatumtakasi yeyote mbele ya Allah" ambao husema kauli njema na kufanya vitendo vyema, na Allah amewasifu wale wenye sifa hizi:
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين
"Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?" (QS. Fussilat [41]: 33)
Kwa wageni waheshimiwa wa ukurasa huu wanaoufuatilia kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri iliyobebwa ndani yake, Allah awalipe kheri.
Nawapongeza nyote kwa Eid al-Fitr tukufu.. Na Allah akubali ibada zenu.. Na Allah ndiye Mlinzi wa waja wema...
Ndugu waheshimiwa:
Eid hii inakuja huku dola haramu ya Kiyahudi ikifanya madhambi makubwa dhidi ya binadamu, miti na mawe huko Gaza na Palestina yote, nayo inafanya hivyo kwa msaada wa Amerika inayoisambazia mabomu, makombora na ndege.. Na ingawa si jambo la kushangaza kwa chombo cha Kiyahudi kufanya hivyo kwa msaada wa Amerika, kwani wao ni maadui wa Uislamu na Waislamu, lakini cha kushangaza ni kuwa hakuna hata mmoja wa watawala katika nchi za Kiislamu, hasa wale walio jirani na Palestina, anayeanzisha hatua ya kulisogeza jeshi lake kunusuru Gaza, watu wake, Al-Aqsa na maeneo yanayoizunguka, na kuing’oa dola ya Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake, na kisha kuirejesha Palestina yote kwa watu wake.. Je, si ni kwamba yule aliyeteka ardhi ya Waislamu na kuwafukuza watu wake anastahili kupigwa vita na majeshi ya Waislamu na kumfukuza kama alivyowafukuza watu wake?
وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ
"Na waueni popote mnapowakuta, na wafukuzeni popote walipokufukuzeni." (QS. Al-Baqarah [2]: 191)
Je, watawala hawawezi kulielewa hilo?! Lakini uovu wao umewatawala, kwani wako chini ya utiifu wa makafiri wakoloni hasa Amerika, hawakatai ombi lake ili kulinda viti vyao vya enzi vilivyopinda.
قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُون
"Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa wapi hawa?" (QS. At-Tawbah [9]: 30)
Haya basi enyi majeshi ya Kiislamu, nusueni ndugu zenu huko Gaza, na ikiwa mifumo ya utawala wa kidikteta iliyopo katika nchi za Kiislamu itasimama mbele yenu, basi wapeni adhabu kali.. na simamisheni utawala wa Allah badala yao, Khilafah kwa Njia ya Utume, ili kutimiza bishara ya Mtume wa Allah ﷺ:
ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ
"Kisha utakuwepo utawala wa kidikteta, utakuwepo kwa muda anaopenda Allah uwepo, kisha Allah atauondoa anapotaka kuiondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha (Mtume) akanyamaza." (Musnad ya Imam Ahmad)
Na hapo ndipo Khalifa, wasaidizi wake na wanajeshi wa Kiislamu kuanzia wa cheo cha juu kabisa hadi cha chini watakapokuwa wakihama kutoka ushindi mmoja hadi mwingine, wakipiga takbira na Umma ukipiga takbira pamoja nao, wakiwa wenye nguvu kupitia kwa Mola wao na wenye utukufu kupitia dini yao, kiasi kwamba hakuna adui atakayethubutu kuwa na chombo chake katika ardhi ya Uislamu..
وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
"Na siku hiyo waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu; hunusuru amtakaye, Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS. Ar-Rum [30]: 4-5)
Mwishoni, enyi ndugu, nawabariki kwa Eid al-Fitr, nikimuomba Allah Mtukufu tuwe tumetekeleza saumu ya mwezi huu mtukufu na visimamo vyake kwa namna inayomridhisha Allah Mtukufu na Mtume wake ﷺ ... Kadhalika namuomba Yeye Aliyetukuka kuwa Eid hii iwe ni mwanzo wa kheri, baraka na utukufu kwa Uislamu na Waislamu,
وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُون
"Na Mwenyezi Mungu ana nguvu juu ya jambo lake, lakini watu wengi hawajui." (QS. Yusuf [12]: 21)
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
1 Shawwal 1446 H Ndugu yenu inayowiana na 30/03/2025 M Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah