Kwa umma bora uliotolewa kwa watu... Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimu kwa utiifu Kwake...
Kwa wabebaji Da'wah watukufu ambao biashara wala kuuza hakuwapotezi kutokana na kumdhukuru Allah...
Kwa wageni watukufu wa ukurasa huu wanaoelekea kwenye heri iliyobebwa ndani yake...
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Sifa njema ni za Allah, na swala na salamu zimfikie Mtume wa Allah, familia yake, maswahaba zake na waliomfuata, na baada ya hayo:
Hakika namuomba Yeye (Subhaanahu wa Ta'ala) aukubalie Umma wa Kiislamu funga na kusimama kwao (katika ibada), na Allah atusamehe sisi sote madhambi yetu yaliyotangulia kama alivyosema ﷺ katika hadithi iliyopokelewa na Bukhari na Muslim, kutoka kwa Abu Hurairah amesema: Amesema Mtume wa Allah ﷺ:
مَنْ صَامَ رَمَضَانَ، إِيمَاناً وَاحْتِسَاباً، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ
"Mwenye kufunga Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo (kutoka kwa Allah), atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia."
Na katika upokezi mwingine kutoka kwa Abu Hurairah (radhi za Allah ziwe juu yake): Kwamba Mtume wa Allah ﷺ amesema:
مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَاناً وَاحْتِسَاباً، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ
"Mwenye kusimama (kufanya ibada usiku) katika Ramadhani kwa imani na kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia."
Ndugu watukufu: Hakika Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) alifaradhiwa katika mwezi wa Sha’ban mwaka wa pili wa Hijra funga ya mwezi wa Ramadhani, nao ni mwezi ambao Allah ameteremsha ndani yake Qur’an:
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ
"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake Qur’ani kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi." (QS. Al-Baqarah [2]: 185)
Vilevile ni mwezi ambao Allah ameuheshimu Umma huu kwa nusra na ushindi ulio wazi. Vita vya Badr vilitokea mnamo tarehe kumi na saba ya Ramadhani ambapo washirikina wa Makka walishindwa vibaya sana... Kisha kulikuwa na vita vingine muhimu katika mwezi huu mtukufu kuanzia Fath Makkah (Ukombozi wa Makka) tarehe ishirini ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka wa nane wa Hijra, hadi vita vya Al-Buwaib (karibu na mji wa Kufa hivi sasa) ambavyo ni Yarmouk ya Uajemi ambapo Waislamu walishinda chini ya uongozi wa Al-Muthanna mnamo tarehe kumi na nne ya Ramadhani mwaka wa 31 Hijriya. Kisha ukombozi wa Amorium (Amuriya) chini ya uongozi wa Al-Mu'tasim tarehe kumi na saba ya Ramadhani mwaka wa 223 Hijriya, na vita vya Ain Jalut ambapo Waislamu waliwashinda Watartari mnamo tarehe ishirini na tano ya Ramadhani mwaka wa 658 Hijriya, pamoja na ushindi mwingine mwingi katika mwezi huu mtukufu...
Hivyo basi, funga imeambatana na Qur'an Tukufu ambayo haifikiwi na batili mbele yake wala nyuma yake... na funga imeambatana na ukombozi na nusra... funga imeambatana na Jihad... funga imeambatana na utekelezaji wa hukumu za Allah... Na kila mwenye macho na busara amejua kuwa hukumu za Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) hazitengani, ziwe ni ibada, Jihad, muamala, maadili na tabia, au mipaka ya kisheria (hudud) na jinai... zote zinatoka katika chimbuko moja. Na mwenye kuzitafakari aya za Kitabu Kitukufu na maandiko ya hadithi tukufu ataliona hilo liko wazi kabisa. Muislamu husoma katika aya za Dhikri Hakim:
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ
"Na simamisheni Swala." (QS. Al-Baqarah [2]: 43)
Kama anavyosoma:
وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللهُ
"Na wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Allah." (QS. Al-Ma'idah [5]: 49)
Na anasoma:
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ
"Mmefaradhiwa kufunga." (QS. Al-Baqarah [2]: 183)
Kama anavyosoma pia:
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ
"Mmefaradhiwa kupigana vita." (QS. Al-Baqarah [2]: 216)
Kadhalika, anasoma kuhusu Hajj katika hadithi za Mtume wa Allah ﷺ:
خُذُوا عَنِّي مَنَاسِكَكُمْ
"Chukueni kutoka kwangu namna ya kutekeleza ibada zenu (za Hajj)." (Imepokelewa na Al-Bayhaqi katika Sunan al-Kubra kutoka kwa Jabir)
Vilevile anasoma kuhusu Hudud:
خُذُوا عَنِّي، خُذُوا عَنِّي، قَدْ جَعَلَ اللهُ لَهُنَّ سَبِيلاً، الْبِكْرُ بِالْبِكْرِ جَلْدُ مِائَةٍ وَنَفْيُ سَنَةٍ، وَالثَّيِّبُ بِالثَّيِّبِ جَلْدُ مِائَةٍ، وَالرَّجْمُ
"Chukueni kutoka kwangu, chukueni kutoka kwangu, hakika Allah ameshawawekea njia; bikira kwa bikira (akizini) ni kupigwa mijeledi mia na kuhamishwa mwaka mmoja, na aliyewahi kuoa/kuolewa kwa aliyewahi kuoa/kuolewa ni kupigwa mijeledi mia na kupigwa mawe (hadi kufa)." (Imepokelewa na Muslim kutoka kwa 'Ubada bin as-Samit)
Na anasoma katika Muamala:
البَيِّعَانِ بِالخِيَارِ مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا - أو قال حتى يتفرقا -
"Wauzaji wawili wana hiyari (ya kuvunja mkataba) maadamu hawajatengana – au alisema mpaka watengane." (Imepokelewa na Bukhari kutoka kwa Hakim bin Hizam)
Pia anasoma kuhusu Bay'ah ya Khalifah:
وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً
"Na yeyote atakayekufa na huku hana Bay'ah (ahadi ya utiifu kwa Khalifah) shingoni mwake, basi amekufa kifo cha kijahilia." (Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Abdullah bin Umar)
Kwa hiyo, Uislamu ni mfumo mmoja usiogawanyika, na ulinganizi (Da'wah) kwake ni mmoja kwa ajili ya kuutekeleza katika dola, maisha, na jamii. Hivyo basi, mwenye kutofautisha kati ya aya za Allah, na akadai kutenganisha dini na maisha, au kutenganisha dini na siasa, amefanya dhambi kubwa na jinai nzito inayompeleka mhusika wake kwenye fedheha duniani na adhabu kali Akhera.
Enyi Waislamu: Nakumbusheni haya yote katika siku hizi ambapo mashambulizi ya kinyama ya kiyahudi yamepamba moto dhidi ya watu wa Gaza. Wameshtushwa na ushujaa wa watu wa Gaza; miezi mingi imepita bila chombo cha kiyahudi kufikia mafanikio yoyote iliyokuwa ikidai dhidi ya watu wa Gaza. Kimepoteza fahamu na badala ya kupigana uso kwa uso na kundi lile la waumini lenye silaha duni wakati chenyewe kimesheheni silaha za Marekani na Magharibi, kimegeukia kuua wanawake na watoto ili kijitafutie "mafanikio" ya kuzungumzia! Hakika chombo cha kiyahudi kinachora kufeli kwake kwa mikono yake chenyewe, kwani wao si watu wa vita isipokuwa kwa "kamba kutoka kwa watu" kama alivyosema Mwenye Nguvu, Mtukufu:
ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ
"Wamepigiwa dhalili popote wanapokutikana, isipokuwa (wakishika) kamba ya Allah na kamba ya watu." (QS. Ali 'Imran [3]: 112)
Na wao wameshakata kamba ya Allah tangu zama za Manabii wao, na imebaki kwao kamba ya watu kutoka Marekani, Ulaya, na vibaraka wao miongoni mwa watawala wasaliti katika nchi za Waislamu ambao hawachukui hatua yoyote huku wakiona unyama wa kiyahudi dhidi ya watoto na wanawake. Bali, walio bora miongoni mwao ni yule anayesimama kuhesabu idadi ya mashahidi na majeruhi:
قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ
"Allah awaangamize! Ni vipi wanageuzwa?" (QS. At-Tawbah [9]: 30)
Pamoja na hayo enyi Waislamu, kupigana na mayahudi, kuwaua, na kukiondoa chombo chao ni jambo ambalo hapana shaka linakuja chini ya uongozi wa Khalifah muadilifu (Rashid) na mpiganaji (mujahid) baada ya utawala huu wa kidikteta (mulkan jabriyan) na watawala vibaraka. Bishara ya Mtume wa Allah ﷺ haitachelewa wakati wake kwa idhini ya Allah, ikiwa ni uthibitisho wa hadithi aliyoitoa Ahmad kutoka kwa Mtume wa Allah ﷺ:
ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ
"Kisha utakuwepo utawala wa kidikteta, utakuwepo kwa muda anaotaka Allah uwepo, kisha Allah atauondoa anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza."
Vilevile kusadikisha hadithi ya Mtume wa Allah iliyopokelewa na Muslim:
لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...
"Hakika mtapigana na Mayahudi na mtawaua..."
Mwisho, kama tunavyopaswa kuwa na pupa ya kufunga ili Allah aturidhie na atusamehe madhambi yetu yaliyotangulia, tunapaswa pia kuwa na pupa ya kufanya kazi ya kurejesha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah ya Rashidah. Hili ni ili tuwe miongoni mwa washindi duniani kwa kutekeleza hukumu za Allah, tukivuliwa chini ya bendera ya Mtume wa Allah ﷺ, bendera ya Al-Uqab, bendera ya La ilaha illallah Muhammad Rasulullah. Na tuwe miongoni mwa washindi Akhera pia kwa idhini Yake (Subhaanahu wa Ta'ala), tukivuliwa katika kivuli Chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake; hapo tutakuwa tumeshinda katika nyumba zote mbili, na huo ndio ushindi mkuu.
Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.