Jibu la Swali
Swali: (Ikulu ya Marekani ilisema katika taarifa yake kwamba Rais wa Marekani Trump alimwambia Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan katika mazungumzo ya simu siku ya Ijumaa, kwamba ni muhimu kwa India na Pakistan kujaribu kupunguza mvutano huko Jammu na Kashmir kupitia mazungumzo ya nchi mbili. Hespress - Reuters mnamo 17/08/2019) mwisho... Trump anasema hayo wakati ambapo Modi anajivunia kunyakua Kashmir rasmi na kwamba haipingwi tena kati ya India na Pakistan (Modi, Waziri Mkuu wa India, alisema mnamo 15/08/2019 katika hotuba yake kwenye hafla ya Siku ya Uhuru wa India "Kwamba serikali yake imeweza kufanikisha kile ambacho serikali zote za awali za India zilishindwa..." Al-Sharq Al-Awsat mnamo 16/08/2019)! Swali ni: Kuna faida gani ya mazungumzo wakati India imeshuanyakua Kashmir rasmi? Na kwa nini Pakistan haikuchukua hatua sahihi ya kukomboa Kashmir kwa Jihad, haswa ikiwa ina uwezo wa kufanya hivyo kupitia jeshi lake? Kisha, je, Marekani ina mchango wowote katika hili? Mwenyezi Mungu akujazi heri.
Jibu: Ili jibu liwe wazi, tunatathmini mambo yafuatayo:
1- Kati ya maeneo yote duniani, eneo la Eurasia ndilo muhimu zaidi kwa wapangaji wa sera za kigeni wa Marekani, na Marekani inafanya kila juhudi ili kuzuia mshindani yeyote asijitokeze katika eneo hilo. Kuna washindani wanne wanaotarajiwa: Urusi, China, Ujerumani, na Khilafah... Lakini inaona kuwa mshindani halisi sasa ni China. Tangu kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti, wanaistratejia wa Marekani wamekuwa wakiitazama China kama tishio kubwa kwa maslahi ya Marekani. Kiutendaji, wanaistratejia wa Marekani wametumia nchi za Asia-Pasifiki kuhujumu kuinuka kwa China kama nguvu ya majini, na wameitumia rasi ya India kukabiliana na kuinuka kwa China kama nguvu inayotawala Eurasia... Wakati Marekani ilikuwa ikiimarisha uwezo wake katika eneo la Asia-Pasifiki kupitia idadi kubwa ya miungano na Taiwan, Thailand, Vietnam, Philippines, Japan, Indonesia, na Australia, hakukuwa na muungano wowote mkubwa katika rasi ya India - haswa India - hadi Vajpayee alipoingia madarakani na kuongoza serikali mwishoni mnamo miaka ya tisini. Kilele cha kuitumia India kilikuja baada ya ziara ya Rais Clinton mnamo mwaka 2000, na muda mfupi baada ya matukio ya Septemba 11, 2001, utawala wa Bush ulielekeza nguvu zake kwa India. Sehemu kubwa ya hatua za Marekani zilielekezwa katika kuziba pengo la kijeshi kati ya India na China kulingana na programu za Marekani... Miongoni mwa hatua hizi ni makubaliano ya nyuklia ya Marekani na India...
2- Marekani iliona kuwa mvutano kuhusu Kashmir kati ya India na Pakistan unadhoofisha uwezo wa rasi ya India kukabiliana na China... Ili kushinda mvutano huu, Marekani ilianza mchakato wa kurekebisha mahusiano (normalization) kati ya India na Pakistan. Lengo la marekebisho haya lilikuwa kuzuia vikosi vya India na Pakistan kupigana vyenyewe kwa vyenyewe kwa sababu ya Kashmir, na kuelekeza juhudi zao kwenye ushirikiano na Marekani hatimaye kudhibiti kuinuka kwa China. Marekani ilidhani kuwa kuunganishwa kwa Kashmir na India na shinikizo la Marekani kwa utawala wa Pakistan kuuzuia kuirejesha kijeshi na kuhamishia suala hilo kwenye mazungumzo kutaifanya kadhia hiyo kufa na kuzuia mzozo wa kijeshi kati yao, kama ilivyo hali ya mamlaka ya Abbas huko Palestina na nchi za Kiarabu zinazoizunguka bila mzozo wa kijeshi na Dola ya Mayahudi, wakati wao wananyakua na kuunganisha sehemu yoyote ya Palestina wanayotaka! Hivyo basi, Modi alianza mpango wa kunyakua Jammu na Kashmir na kubadilisha muundo wa idadi ya watu humo, na kisha akachukua uamuzi mnamo 05/08/2019 wa kufuta Ibara ya 370 ya katiba yao inayohusiana na Kashmir. Ibara hii ilikuwa ikilipa eneo hilo kiwango kikubwa cha utawala wa ndani, kwani iliruhusu Kashmir kuwa na katiba yake, bendera tofauti, na uhuru katika mambo mengi isipokuwa mambo ya nje, ulinzi, na mawasiliano. Uamuzi wa kufuta ulitolewa chini ya jina la sheria ya "Uundaji Upya", ambayo inagawa Kashmir inayokaliwa kwa mabavu katika maeneo mawili: eneo la Jammu na Kashmir na eneo la Ladakh, na inaunganisha usimamizi wa maeneo haya mawili na serikali kuu ya New Delhi. Baraza la juu la Bunge la India "Baraza la Majimbo" liliidhinisha mswada huo siku iliyofuata 06/08/2019 kwa kura 125 dhidi ya 61. Pia ilifutwa Ibara ya 35A ambayo inawazuia watu wasio wa Kashmir kununua mali na ardhi huko Kashmir, hatua ambayo itawapa fursa Wahindi wengine kutoka majimbo mengine kuja Kashmir kununua mali na ardhi na kuomba kazi za serikali humo, jambo litakalosababisha mabadiliko ya idadi ya watu na utamaduni katika eneo hilo lenye Waislamu wengi... Yaani, hatua inayofanana na hatua za Dola ya Mayahudi katika kunyakua ardhi huko Palestina! Kama vile anachofanya Netanyahu kinavyofanywa kwa idhini ya Marekani na baraka zake, vivyo hivyo Modi anafanya kwa idhini ya Marekani na baraka zake... Hii ina maana kwamba Modi amekarabati mbinu ya Netanyahu huko Palestina kwa idhini na uungaji mkono wa Marekani.
3- Wakati India ilipotangaza uamuzi wake wa mwisho wa kufuta hadhi maalum ya Kashmir, msimamo wa Pakistan pia ulikuwa wa kusuasua na haukuzidi kulaani ili tu kutimiza wajibu. Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilitoa taarifa ikisema: "Pakistan inalaani vikali na kukataa tangazo lililotolewa siku ya Jumatatu (05/08/2019) kutoka New Delhi, na kwamba hakuna hatua yoyote ya upande mmoja ya serikali ya India inayoweza kubadilisha hali ya mzozo huo, na kama sehemu ya mzozo huu wa kimataifa, Pakistan itafanya kila iwezalo kukabiliana na hatua hizo haramu." (AFP 05/08/2019). Balozi wa Pakistan mjini Moscow, Qazi Khalilullah, alisema "Mamlaka za Pakistan kwa sasa zinajielekeza katika kuandaa majibu ya kidiplomasia, kisiasa, na kisheria dhidi ya hatua za hivi karibuni za India huko Kashmir, na kamati maalum imeundwa itakayotoa mapendekezo kwa serikali kuhusu suala hili." Hii ni sawasawa na kile anachofanya mamlaka ya Abbas na nchi za Kiarabu zinazoizunguka, ambapo wanalaani na kulalamika dhidi ya ukiukaji wa Dola ya Mayahudi katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina bila kuhamasisha majeshi kwa ajili ya vita. Pakistan inakariri jukumu lile lile kwa kulaani bila kuhamasisha jeshi kupigana! Zaidi ya hayo, wanakimbilia Umoja wa Mataifa na Marekani kutatua masuala yao, ilhali hao ndio adui, basi jihadhari nao!
4- Kinachothibitisha hili ni hatua ya Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan mnamo 11/08/2019 kutuma jumbe kwenye Twitter akielezea hatua ya India kuwa itasababisha "kukandamizwa kwa Waislamu nchini India na baadaye kuilenga Pakistan, na ni jaribio la kubadilisha muundo wa idadi ya watu huko Kashmir kupitia mauaji ya kikabila" na akaiomba ile inayoitwa jumuia ya kimataifa kuingilia kati na kwamba jumuia hiyo ina nguvu ya kuidhibiti India! Pakistan inasahau kwamba yenyewe ina nguvu ya kuidhibiti India... Na hili ni jambo lililoshuhudiwa kwani India ilitangaza mnamo 26/02/2019 kutekeleza mashambulizi ya anga kwenye kambi za vikundi vya Kashmir na kwamba "iliua idadi kubwa katika kambi hizi." Hii ilitokea baada ya kutangazwa kuwa vikundi vya Kashmir vilitekeleza operesheni dhidi ya jeshi la India linalokalia Kashmir na kuua wanajeshi 41 wa India mnamo 14/02/2019. Pakistan ilitangaza siku iliyofuata baada ya shambulio hilo la India kuwa imetungua ndege mbili za India, ikamteka rubani mmoja na kuua wawili... Hii inaashiria uwezo wa jeshi katika kuidhibiti India na kuishinda, lakini utawala wa Pakistan hauko makini katika kuchukua hatua zozote za kuidhibiti India, bali unatii amri za Marekani iliyoagiza kutoeneza mzozo (de-escalation) katika tukio la kutunguliwa kwa ndege hizo mbili. Habari ziliripoti kuwa ("Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Pompeo alizungumza kwa simu na wenzake wa India na Pakistan kufuatia shambulio la India kwenye kambi ya kundi la Jaish-e-Mohammed na kutoa taarifa akizitaka pande zote mbili kuwa watulivu, na kuepuka hatua yoyote ambayo ingeweza kuongeza hatari. Hata hivyo alisimama upande wa India alipoongeza kwa kusema kuwa "mashambulizi ya anga ya India yalikuwa hatua za kupambana na ugaidi, na akaihimiza Pakistan kuchukua hatua kali dhidi ya makundi ya kigaidi yanayofanya kazi katika ardhi yake"... AFP, Reuters 28/02/2019). Inaonekana kutokana na tamko hili kiasi cha upendeleo wa Marekani upande wa India na uungaji mkono wake kwa kile inachokifanya kama inavyofanya huko Palestina ambapo daima inapendelea upande wa chombo cha Mayahudi na kukiunga mkono katika kila kitu kinachokifanya dhidi ya Waislamu wanaotetea nchi yao na kufanya kazi kuikomboa... Pamoja na hayo, Pakistan kama mamlaka ya Abbas na tawala za Kiarabu haijaacha tabia yake ya kuikimbilia Marekani na kusubiri iingilie kati ili kuitatulia tatizo lake, huku ikitambua kuwa Marekani inasimama upande wa India. Balozi wa Pakistan mjini Washington, Majeed Khan, alisema mnamo 27/02/2019 kwamba (Taarifa "taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani" ilitafsiriwa na kueleweka kama uungaji mkono kwa msimamo wa India na hili ndilo lililowatia moyo zaidi "Wahindi") na akasema: "Pengine hakuna nchi nyingine iliyo katika nafasi nzuri kuliko Marekani kufanya jukumu fulani"... AFP 28/02/2019). Yaani, pamoja na kukiri kwamba taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ni uungaji mkono wa msimamo wa India, bado anaona kuwa Marekani ndiyo inayofaa kutekeleza jukumu hilo! Na kama ilivyo tabia ya Marekani ni kuwashughulisha na Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa... Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa utawala wa Pakistan ulipotangaza kuwa hautaki mvutano na kuenea mzozo na India, na kwamba utawasilisha malalamiko rasmi kwa Umoja wa Mataifa dhidi ya New Delhi tu, wala si zaidi ya hapo. Hata utawala ulitangaza kuwa utamkabidhi yule rubani muuaji wa India kwa nchi ya India na ukamkabidhi kweli kama ishara ya amani kulingana na madai yake... Na hivyo ndivyo ilivyokuwa baadaye wakati wa kunyakuliwa kwa Kashmir, Pakistan iliitisha (kikao maalum cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali katika eneo la Kashmir kikiwa kimefungwa baada ya uamuzi wa India wa kufuta utawala wa ndani wa eneo hilo... Mwakilishi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa Maleeha Lodhi alikaribisha uamuzi wa Baraza la Usalama wa kujadili suala la Kashmir wakati wa kikao maalum, akisema kuwa suala la Kashmir limeanza kuibuliwa kimataifa na kwamba liko tayari kwa ufumbuzi na India kupitia mazungumzo. Al-Araby Al-Jadeed mnamo 16/08/2019)!
5- Msimamo huu unaashiria kuwa utawala wa Pakistan hautachukua hatua za kijeshi kuidhibiti India na hautafanya kazi yoyote makini dhidi yake, jambo linaloimarisha uamuzi wa India wa kufuta hadhi maalum ya Kashmir na kuimarisha uvamizi. Ikumbukwe kwamba Imran Khan katika ziara yake nchini Marekani mnamo 21/07/2019 akiandamana na Mkuu wa Jeshi la Pakistan Javed Bajwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ujasusi na Usalama wa Ndani Faiz Hameed, wakati wa mkutano wake na Trump alimuomba acheze jukumu kwa maslahi ya Marekani huko Afghanistan kwa kusema "Anatumai kuwa Pakistan itasaidia kupatanisha ili kufikia makubaliano ya kisiasa kumaliza vita vya miaka 18 huko Afghanistan", kisha Imran Khan akatii mara moja amri za Trump akisema: ("Nitakutana na Taliban na nitafanya kila niwezalo kuwashawishi waingie kwenye mazungumzo na serikali ya Afghanistan." Kisha akajivunia usaliti wa utawala wa Pakistan na kutoa huduma kwa Marekani akisema: "Kwamba ujasusi wa Pakistan ulitoa taarifa zilizoruhusu "Wamarekani" kubaini mahali alipo Osama bin Laden"... Reuters 22/07/2019), yote haya anayatoa kwa Wamarekani wakati ambapo wao wanaiunga mkono India kwa gharama ya Pakistan! Wakati tangazo la India la kufuta hadhi maalum ya Kashmir lilipokuja, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa taarifa iliyosema: "Tunaendelea kuunga mkono mazungumzo ya moja kwa moja kati ya India na Pakistan kuhusu Kashmir na masuala mengine yanayoleta wasiwasi"... (Reuters 07/08/2019). Marekani haikulaani hatua ya India wala kusema kuwa inakiuka maamuzi ya kimataifa kuhusu Kashmir, bali ilisema "kupitia mazungumzo" kama dharau kwa Imran na utawala wake. Mazungumzo gani wakati India inatangaza kunyakua Kashmir rasmi?! Hii inaonyesha idhini ya Marekani kwa hatua hii, bali inaonyesha elimu ya Marekani ya awali kuhusu hilo kwa sababu India haiwezi kuchukua hatua kama hiyo kabla ya kushauriana na Marekani na kupata baraka zake...
6- Imewahi kuandikwa katika kitabu chetu "Qadhaya Siyasiyyah - Biladu al-Muslimin al-Muhtallah" kilichotolewa mnamo 21/05/2004 kuhusu kadhia ya Kashmir yafuatayo: (Na kwa sababu hiyo, Marekani - wakati nchi mbili hizi India na Pakistan zimekuwa chini ya ushawishi wake - imekuwa ikijitahidi kuleta maelewano kati yao kuhusu Kashmir. Na ilibadilisha mtazamo wake wa kimsingi wa kutatua kadhia hiyo kwani mwanzoni ilikuwa ikitaka kadhia hiyo iwe ya kimataifa na sasa inazihimiza pande hizo mbili kuisuluhisha kati yao wenyewe. Na maoni ya Marekani katika suluhu hii sasa yanajumuisha kuigawa Kashmir, ili Kashmir iliyokombolewa iwe ya Pakistan, na Kashmir iliyo chini ya udhibiti wa India iwe ya India"). Kwa hivyo yanayotokea sasa yanalingana na yaliyoandikwa katika kitabu chetu. India imechukua hatua hii na kutengeneza uhalisia mpya unaosisitiza uvamizi wa India huko Kashmir.
7- China ililaani hatua ya India, kwani uamuzi wa kufutwa kwa Ibara ya 370 ulitolewa chini ya jina la sheria ya "Uundaji Upya" ukagawa Kashmir inayokaliwa kwa mabavu katika maeneo mawili: eneo la Jammu na Kashmir, na eneo la Ladakh, na kuunganisha usimamizi wa maeneo hayo mawili na serikali kuu ya New Delhi... Hasa kwa vile Ladakh iliyoko katika eneo la Kashmir iko kwenye nyanda za juu za Tibet karibu na China, na India haikushauriana na China kabla ya sheria hii. Kwa hiyo, Hua Chunying, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, alisema "Kwamba upande wa India hivi karibuni umeendelea kudhoofisha sera ya kikanda ya China kupitia mabadiliko ya sheria zake za ndani zinazohusiana na mipaka bila kurejea Beijing na kwamba China haiwezi kukubali vitendo hivi... Matamko ya Ying yalikuja kama jibu la uamuzi wa New Delhi Jumatatu iliyopita wa kutangaza kuwa Ladakh ni eneo la muungano ambalo linajumuisha sehemu ya magharibi ya mpaka wa China na India, na Chunying alisisitiza kuwa China siku zote inapinga India kujumuisha ardhi za China katika sehemu ya magharibi ya mpaka chini ya jina la jimbo la utawala la India..." (Al-Bayan mnamo 08/08/2019).
8- Tunahitimisha kutokana na yaliyotangulia mambo yafuatayo:
a- Kufutwa kwa Ibara ya 370 na kisha hatua za unyakuzi alizozifanya na anazoendelea kuzifanya Modi ni kwa baraka za Marekani na uungaji mkono wake, ikidhani kuwa unyakuzi huo utawafanya Waislamu waisahau Kashmir na India na Pakistan ziwe bila matatizo kati yao kwa kuzingatia kuwa tawala zote mbili sasa zinafuata mrengo wa Marekani... Marekani ilisahau au ilijisahaulisha, yenyewe na India, kwamba Kashmir iko ndani ya nyoyo za Waislamu huko Pakistan na kila mahali, sawa na nchi yoyote ya Kiislamu inayokaliwa kwa mabavu...
b- Kwamba ridhaa ya utawala nchini Pakistan au ukimya wake kuhusu unyakuzi wa India kwa Kashmir haumaanishi hata kidogo ukimya wa Waislamu huko Pakistan wala ukimya wa majeshi yao... Na mashambulizi ya jeshi hili India inayafahamu, na tukio la kutunguliwa kwa ndege mbili haliko mbali na India... Na mashambulizi haya ya jeshi yanafanyika wakati utawala wa Imran unalizuia jeshi kushambulia ili kukomboa Kashmir, bali linaruhusiwa tu kujihami na hata hivyo kwa vikwazo! Sasa ingekuwaje kama wangehamasishwa kupigana? Basi bila shaka adui angeona kutoka kwao yale yaliyo na maangamizi yake!
c- China ililaani hatua ya India, ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitoa taarifa ikisema: "Kwamba uamuzi wa India ni wa upande mmoja na una athari hasi kwa mamlaka ya kikanda ya China na unakiuka makubaliano ya kimataifa. Beijing haitakubali uamuzi wa upande mmoja wa India unaohusiana na mabadiliko ya hali ya kisheria ya eneo la Kashmir na kwamba uamuzi huo haukubaliki" (Anadolu 06/08/2019). China inatambua kuwa hilo linaimarisha msimamo wa India katika eneo hilo, na kuifanya India ishindane na China na kuwa nguvu ya kikanda inayolingana nayo, na hili ndilo Marekani inalolenga kukabiliana na nguvu ya kikanda ya China... Hasa kwa vile Ladakh iliyoko katika eneo la Kashmir iko kwenye nyanda za juu za Tibet karibu na China, na ingawa idadi ya watu wake ni ndogo (karibu watu 270,000) lakini kutatua kadhia ya Kashmir kwa namna hii na kuingilia eneo la Ladakh kwenye mpaka wa China na India bila kushauriana na China kumezua ukosoaji kutoka kwa China. Na ikiwa China itaweza kudhibiti hatua zake na kukuza ufahamu wake wa kisiasa ili kutumia hali ya Ladakh kwa faida yake, basi inaweza kupindua mipango ya Marekani, kwani badala ya Ladakh kuwa kituo cha operesheni za mbele kwa majeshi ya Marekani dhidi ya China kama Marekani inavyopanga, inaweza kuwa mtego kwa majeshi hayo watakamoingia na wasitoke!
9- Mwishowe, msiba wetu uko kwa watawala katika nchi za Waislamu. Hakika wenzo za nguvu tulizonazo zinatosha, bali ziko juu ya kutosha kurejesha haki zetu kwa izza na kumpa adui somo litakaloambatana naye hadi kaburini kwake! Lakini watawala waliofanya hiana kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Waumini wanawasujudia mabwana zao miongoni mwa makafiri wakoloni zaidi ya wanavyomsujudia Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote, hivyo wanayazuia majeshi yasipigane na maadui zao ili kukomboa nchi zao zinazokaliwa kwa mabavu... Kisha watawala hawa wanaomba kwa unyonge na fedheha makombo fulani katika vichochoro vya Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama... Hiyo ni kama watayapata makombo hayo!... Lakini pamoja na majanga haya yote, nchi za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu kuanzia Palestina hadi Kashmir, hadi Burma ardhi ya Warohingya, kisha Turkestan Mashariki, Caucasus, Chechnya na maeneo ya pembezoni mwake, Crimea na kila ardhi ambayo mwadhini alipiga takbira humo na ikakaliwa na maadui wa Uislamu... zote zitarejea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu katika Darul Islam ikipepea juu yake bendera ya Uislamu... Atazirejesha Imamu ambaye ni kinga... Atazirejesha Khalifah Mwongofu... Atazirejesha jeshi la Uislamu la Mujahidina... Basi yule anayependa izza duniani na Pepo ya juu kabisa (Al-Firdaws) Akhera, basi ajifunge kibwebwe na afanye kazi pamoja na wafanyao kazi kusimamisha Khilafah, na kazi hii iingie katika damu yake, moyo wake, na viungo vyake kwa ukweli na ikhlasi...
إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ
"Hakika huku ndiko kufanikiwa kukubwa. Kwa mfano wa haya, hebu wafanye kazi wafanyao kazi." (QS. As-Saffat [37]: 60-61)
17 Dhul-Hijjah 1440 H 18/08/2019 M