Kwa wageni wa kurasa zake kwa mnasaba wa kuwadia kwa Idul Adha ya mwaka 1436 H sawia na 2015 M
Alhamdulillah, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Allah, na jamaa zake na masahaba zake na waliomfuata, na baada ya hapo:
Kwa Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimu akasema juu yake:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ
"Mlikuwa bora ya Umma uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Allah..." (Al-Imran [3]: 110)
Kwa wabeba dawa wasafi na wachamungu – wala hatumtakasi yeyote mbele ya Allah – ambao husema yaliyo mazuri na kufanya yaliyo mema, na Allah akamsifu mwenye sifa hizi:
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين
"Na nani mbora wa kusema kuliko yule aliyelingania kwa Allah na akafanya vitendo vyema na akasema hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu." (Fussilat [41]: 33)
Kwa wageni wa ukurasa watukufu wanaoufuatilia kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri inayobebwa na ukurasa huu, Allah awalipe kheri...
Kwa hawa wote, nawapongeza kwa sikukuu ya Idul Adha, na nanamuomba Allah (swt) awakubalie Hija mahujaji na aijaalie iwe Hijjan Mabruran na juhudi zenye kushukuriwa na dhambi zenye kusamehewa, na awafikie Allah (swt) wale ambao hawakuhiji mwaka huu waweze kuhiji mwakani wakiwa na kheri na juu ya kheri, na Allah (swt) ndiye msimamizi wa waja wema.
Vile vile namuomba (swt) kwamba sikukuu hii iwe ni mfunguaji wa kheri na baraka kwa Waislamu, na sikukuu ijayo ifike tukiwa tunajikinga chini ya kivuli cha bendera ya Khilafah Rashidah, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah:
وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
"Na siku hiyo waumini watafurahi * kwa nusra ya Allah, humunusuru amtakaye naye ni Mwenye Nguvu, Mwenye Kurehemu." (Ar-Rum [30]: 4-5)
Mwisho, nakupeeni salamu na nakuombeeni kheri, na Allah atakabali taa (zote).
وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ
"Na ni malipo mazuri yaliyoje ya wafanyaji kazi." (Al-Imran [3]: 136)
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Idul Adha ya Mwaka 1436 H Ndugu yenu Ikiwafikiana na 24/09/2015 M Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah