Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu
Sifa njema ni za Allah, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Allah, na familia yake, maswahaba zake, na waliomfuata, ama baada ya hayo:
Kwa Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimu akisema juu yake:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ
"Mlikuwa bora ya Umma waliofanyiwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu..." (QS Al-Imran [3]: 110)
Kwa wabebaji da’wah watakasifu na wachamungu – na hatumtakasi yeyote mbele ya Allah – ambao husema kauli nzuri na kufanya vitendo vyema, hivyo Allah akawasifu wenye sifa hizi:
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين
"Na ni nani mbora wa kauli kuliko yule anayelingania kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu?" (QS Fussilat [41]: 33)
Kwa wageni watukufu wa ukurasa huu wanaoufuatilia kwa haki na ukweli, na wanaotafuta kheri iliyobebwa ndani yake, Allah awalipe kheri...
Kwa hawa wote, nawapongeza kwa Eid al-Fitr, na nakuombeni kwa Allah Aliyetakasika aikubali saumu yenu na awajalie kuwa miongoni mwa walioachwa huru na moto katika mwezi huu mtukufu. Pia nakuombeni Kwake Aliyetakasika kuwa Eid hii iwe ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu, ili Eid ijayo iwadie huku tukijifunika kwa kivuli cha bendera ya Khilafah Iliyoongoka, bendera ya La ilaha illa Allah Muhammad Rasulullah, na hilo kwa Allah si jambo gumu...
Na mwisho, nawapelekeeni salamu na nakuombeeni kheri, Allah ayatakabali matendo yenu ya taa, na awalinde na kila ubaya, na awaepushe na kila shari:
فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ
"Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wanaorehemu." (QS Yusuf [12]: 64)
Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh
Ndugu yenu, Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah