Home About Articles Ask the Sheikh
Siasa

Ujumbe wa Mwanachuoni Mtajika Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Hafla ya Kuingia kwa Eid Al-Adha ya Baraka kwa Mwaka 1439 AH sawia na 2018 CE

August 21, 2018
49

بسم الله الرحمن الرحيم

Allah Akbar, Allah Akbar, Allah Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allah Akbar, Allah Akbar, Wa lilah Alhamd

Kwa Umma wa Kiislamu ambao Allah ameuheshimisha na kuusifu kuwa:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

"Nyinyi ndio Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Allah." (QS. Al-i-Imran [3]: 110)

Kwa wabebaji dawa, Shabab kwa wavulana na wasichana wa Hizb ut Tahrir, wabebaji dawa walio safi na wacha Mungu—na hatumtakasi yeyote mbele ya Allah—wale wanaosema kauli njema na kufanya vitendo vya uadilifu, na matokeo yake Allah akawasifu wenye sifa hizi:

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين

"Na ni nani mbora wa kusema kuliko yule anayelingania kwa Allah na akatenda mema na akasema: 'Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu'." (QS. Fussilat [41]: 33)

Kwa wageni watukufu wa ukurasa wa Facebook ambao wanautembelea kwa ukweli na uaminifu, wakitafuta heri iliyobebwa humo, basi Allah awalipe heri…

Kwao wote,

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Nawapongeza kwa mnasaba wa Eid ul-Adha na Allah ayatakabali matendo yao mema. Namuomba Allah Subhaanahu autakabali Hijja ya wale wanaoitekeleza na kuijaalia iwe Hijja yenye kutakabalika, juhudi inayopokelewa vyema na dhambi zenye kusamehewa. Na pia namuomba Allah Subhaanahu awape tawfiki wale ambao hawakutekeleza Hijja mwaka huu ili waitekeleze mwaka ujao kwa kheri juu ya kheri, na Allah Subhaanahu ndiye Mlinzi wa waadilifu.

Ndugu zangu wapendwa, Eid inakuja mwaka huu kukiwa na kutokuwepo kwa Khilafah yetu. Hivyo wakoloni makafiri na vibaraka wao wametuonea na kuanzisha mauaji na umwagaji damu katika nchi zetu. Jinai zao za kinyama zimeenea kuanzia mapipa ya milipuko hadi makombora yenye uharibifu na silaha za kemikali... yote haya yakifanywa kwa mikono yao wakati mwingine na kwa mikono ya vibaraka wao wakati mwingine. Popote unapotazama unakuta damu ya Waislamu inamwagika kidhulma na kwa uadui... Mashariki kuna Burma, na nini unajua kuhusu Burma, hali ya Waislamu kule inahuzunisha, kutokana na jinai za Mabudha na unyama wao ambao hata wanyama wa mwituni wanaukataa... Kisha unaona Kashmir na jinai za India huko... Kaskazini unaona Chechnya na Caucasus kisha Crimea ambayo inaharibiwa kwa mikono ya Urusi, iliyoizamisha katika jinai na damu... Ukitembea kutoka huko kuelekea mashariki hadi Turkestan Mashariki, utaona Uchina na aina zake mbalimbali za uchokozi... Ukitembea kusini na kugusa pwani ya bahari, utapata moyo wa ardhi za Kiislamu, Ardhi Iliyobarikiwa, Palestina, Kibla cha kwanza kati ya viwili. Utawaona Mayahudi wakiipora na kufanya jinai na mauaji, na kusikia mayowe ya Masjid yake ikilia kutokana na jeraha zito linaloifanya ionekane kama inapumua pumzi yake ya mwisho.

Kisha Ash-Sham na nini unajua kuhusu Ash-Sham, damu inamwagika huko kutoka kila upande, mauaji ya kinyama karibu yameenea katika vichochoro na vitongoji na dhalimu wa Ash-Sham, na nyuma yake na mbele yake Amerika na wafuasi na waungaji mkono kutoka Urusi hadi Iran na kisha wanamgambo... Hawa wote wanawasha moto, mauaji na umwagaji damu kwa njia zote za kuua zenye uharibifu... Na hapa mauaji ya Idlib yanazidi kupamba moto kupitia mashambulizi ya kinyama kutoka pande zote, na makundi ya madhalimu yakielekea huko, yakichanganyika na mikataba ya usaliti inayoizunguka... Kisha Iraq, dada wa Ash-Sham katika majanga na maafa... Ukienda kusini kuelekea Yemen, ambayo zamani ilikuwa na furaha, utaona imekuwa na huzuni kwa majanga ya vita yanayochochewa na nchi za kikoloni za kikafiri, ambazo zimeifanya kuwa uwanja wa ushindani kati yao juu ya mafuvu na damu yetu... Ukielekea upande wa jua linapozama, utapata Libya na mapigano ya ndani kati ya Waislamu. Kisha ukielekea Afrika ya Kati, utaona kwamba Waislamu wamepata madhara na uharibifu na kumwagwa kwa damu isiyo na hatia; ukiukaji wa matukufu huko hauelezeki... Kisha jirani yake Sudan, ambayo kusini yake imetenganishwa na kaskazini, na kuacha jeraha lake likivuja damu. Kisha Somalia inayolia kwa maumivu makali na mapigano ya kutisha kwa miaka mingi.

Majanga haya yote yako katika ardhi za Waislamu, ambazo katika miaka yao ya nyuma ziliheshimika kwa Uislamu, bendera ya Uislamu, Adhana ya Uislamu, na uadilifu wa Uislamu... Lakini baada ya kuvunjwa kwa Khilafah na kuondoka kwa Imam, ambaye ni ngao (al-Junnah), hali ilibadilika, Umma uliteseka na wakoloni makafiri na vibaraka wao watawala madhalimu wameshuka na kushirikiana dhidi yake. Bila kusahau majanga ya Waislamu katika nchi za makafiri, ni mengi, mataifa hayo yanataka kuwatoa Waislamu katika ngozi yao (utambulisho), hivyo wanashambulia mavazi ya wanawake wa Kiislamu, na wanataka kuziba sauti ya Adhana yao, na wanaeneza chuki dhidi yao katika jamii zao, vifaa vyao vya maisha na hata kwenye barabara zao... Ni janga tangu kutokuwepo kwa Khilafah, kila moja likipelekea jingine, maafa yaliyolimbikizwa ambayo yanamwacha mwenye subira akiwa amechanganyikiwa.

Ndugu zangu wapendwa, majanga haya kama yangekipata taifa lingine lolote yangekuwa yameshasambaratika au karibu yangekuwa, na yangekuwa yamekata tamaa juu ya kuendelea kwa maisha, kama kuna maisha yaliyobaki... Ama kwa Umma wa Kiislamu, unao katika Kitabu cha Mola wake na Sunnah za Mtume wake na hata katika hali za uumbaji wa usiku na mchana, ambazo huufanya kuwa imara wakati wa shida na azma yake hailegei katika migogoro, bali huongezeka nguvu juu ya nguvu yake na huongeza azma yake juu ya uamuzi wake na kufanya kazi yake kwa nguvu na kwa njia bora na kumtegemea Mola wake kwa dhati:

  • Kutoka katika Kitabu cha Mola wake, aya ziko wazi juu ya hili:

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا * إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا

"Basi hakika pamoja na dhiki kuna wepesi. Hakika pamoja na dhiki kuna wepesi." (QS. Ash-Sharh [94]: 5-6)

حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ

"[Waliendelea] mpaka, wakati Mitume walipokata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, uliwafikia ushindi Wetu, na akaokolewa Tuliyemtaka. Na adhabu Yetu haiwezi kurudishwa kutoka kwa watu ambao ni wahalifu." (QS. Yusuf [12]: 110)

أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُمْ مَثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلِكُمْ مَسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ نَصْرُ اللَّهِ قَرِيبٌ

"Au mnadhani kwamba mtaingia Peponi na ilhali hamjafikiwa na mfano wa wale waliopita kabla yenu? Waliguswa na ufukara na dhiki na wakatikiswa mpaka [hata] Mtume na wale walioamini pamoja naye wakasema: 'Lini utakuja ushindi wa Allah?' Fahamuni kuwa ushindi wa Allah uko karibu." (QS. Al-Baqara [2]: 214)

  • Katika Seerah ya Mtume wake: yaliyompata Mtume wa Allah (saw) wakati wa mwaka wa huzuni, wakati Khadija (ra), Mama wa Waumini alipofariki, na kisha kifo cha Abu Talib, aliyekuwa akimsaidia Mtume wa Allah (saw). Kisha itikio la kikatili kutoka kwa watu wa Taif, ambalo lilimfanya Mtume wa Allah (saw) kuvuja damu. Na kisha mgogoro ulizidi na wakakubaliana kumuua Mtume wa Allah (saw). Kisha wao (Maquraishi) wakamfuata (saw) mpaka kwenye Pango la Thor, ambapo alikuwa amejificha na rafiki yake Abu Bakr, Allah awe radhi naye. Wao (Maquraishi) walisimama mbele ya mlango wa pango wakiwa wametenganishwa tu na Mtume wa Allah kwa umbali wa mkono mmoja au kidogo zaidi... Hii ilikuwa usiku wa siku hiyo, na siku moja au mbili baadaye Mtume (saw) alianzisha dola huko Madina na kuinua jengo lake ili kuujaza ulimwengu nuru na kutangaza Ukweli...

  • Kuhusu hali ya uumbaji wa usiku na mchana, kuongezeka kwa giza la usiku hufuatiwa na nuru ya alfajiri ya kweli, na hiyo ni ishara kwa watu wenye akili.

Hivyo, Umma wa Kiislamu haukati tamaa na rehema za Allah, na unatambua kuwa baada ya dhiki huja wepesi, baada ya ugumu huja ufumbuzi, na nuru ya alfajiri hufuata giza la usiku... Hivyo hauyumbishwi na mitikisiko, bali hufanya kazi na hufanya kazi kwa dhati kwa ajili ya Allah na ni mkweli kwa Mtume wa Allah... Haudhuriwi na wale wanaokengeuka nao au wanaopotea; wengi hawakubali kingine isipokuwa Uislamu kama mbadala...

Ndugu zangu wapendwa, makafiri hao wamevuta pumzi ya unafuu baada ya Khilafah kuvunjwa, hivyo wamefanya jinai zao wakiwa salama, hakuna anayesimama njiani mwao au kuwazuia jinai zao au kuwarudisha makwao... Wanaelewa kuwa ngao ya Waislamu imeondolewa, na wanatumia juhudi zao zote kuizuia isirejee. Hii ni kwa sababu wanajua kuwa mtengenezaji wa ngao hii ni Khilafah, hapa ndipo ulinzi na heshima ya Waislamu vilipo. Hii ndiyo sababu wanawafuatilia wafanyakazi wanaofanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah.

Hivyo, Hizb ut Tahrir imekuwa shabaha ya mishale ya makafiri wakoloni na vibaraka wao watawala katika nchi za Kiislamu. Hizb imekumbwa na manyanyaso mbalimbali na mateso yaliyopelekea ushahidi kutokana na njama za makafiri na majasusi wa madhalimu na chuki ya wale wenye kinyongo. Hizb imepigwa marufuku na kusimamishwa katika ulimwengu wa Kiislamu hata katika nchi zile ambazo ziko wazi kwa vyama katika mifumo tofauti kama Indonesia; chama kimepigwa marufuku huko! Vilevile katika nchi zile zinazofungua milango yao kwa vyama vya kila aina, hata kwa vile vyenye ufisadi, kama Tunisia, chama pia kilipigwa marufuku! Kuhusu wanachama wa chama, wafungwa wa madhalimu wanazungumzia mateso yao. Wanateswa katika magereza yao finyu, na katika gereza lao pana wanadhulumiwa. Hivyo hii ni kwa ajili ya nini? Ni kwa ajili ya kusema neno la Ukweli, ambalo chama hulitangaza, na linawachoma zaidi kuliko upanga, kwa sababu hawana hoja ya kusimama mbele ya neno la ukweli, Allah awaangamize, jinsi gani wanavyodanganywa?

Ndugu zangu wapendwa: Majanga haya yanayousibu Umma na wafanyakazi wa Khilafah ni makubwa sana, na kama Allah asingeliifanya Eid kuwa chanzo cha furaha na lango katika nyoyo za Waislamu kwa ajili ya furaha na kheri ya mahusiano ya kifamilia, na Umma kueneza salamu na pongezi ndani yake. Lau kama isingekuwa kuwepo kwa ahadi ya Allah (swt) kwamba kuwezeshwa na heshima kunakuja kwa Umma huu... Na lau kama isingekuwa kuwepo kwa bishara kutoka kwa Mtume (saw) za kurejea kwa Khilafah... Na lau kama isingekuwa kuwepo kwa chama chenye ikhlasi kwa Allah (swt), mkweli kwa Mtume wa Allah, kikifanya kazi usiku na mchana, kikiomba na kumsihi Allah afungue kupitia mikono yao na kiwe ndicho chenye kusimamisha Khilafah na kurejesha utukufu wa Uislamu na Waislamu... bila mambo haya manne; ingekuwa vigumu kutabasamu, kwa sababu kuna jeraha moyoni, na donge kooni, kutokana na majanga mengi yanayozunguka Waislamu mbele na nyuma, na kulia na kushoto; Khilafah haipo kwa takriban karne moja. Waislamu wamesambaratika na kugawanyika wakitawaliwa na madhalimu Ruwaybiddah (watu duni/wajinga). Bila kusahau uchokozi wa makafiri wakoloni na washirika wao katika nchi na watu, kana kwamba nchi za Kiislamu ni uwanja wa migogoro wa kumwaga damu yetu na kukiuka matukufu yetu.

Hata hivyo, pamoja na ukali wa majanga haya, Hizb ut Tahrir ina uhakika na ushindi wa Allah na kutimia kwa ahadi Yake na bishara za Mtume Wake (saw). Haikati tamaa na rehema za Allah mradi tu inafanya kazi nzuri kwa idhini ya Mola wake. Chama kinatambua kuwa wakati wa Khilafah umeandikwa katika Kitabu. Kila siku inayopita inaifanya siku hii kuwa karibu zaidi. Chama kama hiki ambacho hakiruhusu kukata tamaa kuingia moyoni mwake na azma yake haidhoofiki na uamuzi wake hauvunjiki, kwa idhini ya Al-Aziz Al-Hakim, bali dhiki huongeza nguvu zake, kwani dhiki ni mtihani wa wanaume, na wanachama wa chama ni wanaume wa kweli wanaomuomba Allah (swt) awafanye miongoni mwa wale ambao Allah (swt) alisema juu yao:

رِجَالٌ لَا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ

"[Wapo] watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Allah na kusimamisha sala na kutoa zakat. Wanaiogopa Siku ambayo nyoyo na macho yatageuzwa [kwa hofu]." (QS. An-Nur [24]: 37)

Wabeba ulinganizi (dawa) kwa imani yao kwa baraka kutoka kwa Allah, na ulinganizi huu utainuka juu ya mikono yao, Allah akipenda, na kisha ahadi ya Allah (swt) na bishara za Mtume wake zitatimia katika sehemu tatu kwa tawfiki ya Allah na msaada wake:

  • Kwanza: kurejeshwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala huu wa kidhalimu: Imam Ahmad, na At-Taylasi katika Musnad yake kutokana na Hadith ya Hudhayfah, amesema: "Mtume wa Allah (saw) amesema:

«... ثُمَّ تَكُونُ جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“...Kisha kutakuwepo utawala wa kidikteta kwa muda anaotaka Allah uwepo, kisha Atauondoa Atakapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

  • Pili: kwa kung'olewa kwa dola ya Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake. Muslim amepokea katika Saheeh yake kwa mamlaka ya Abu Hurayrah, Allah awe radhi naye: Mtume wa Allah (saw) amesema:

«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ، فَيَقْتُلُهُمُ الْمُسْلِمُونَ...»

“Qiyama haitafika mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu watawaua…”. Katika riwaya nyingine, amesema (saw):

«تُقَاتِلُكُمُ يَهُودُ، فَتُسَلَّطُونَ عَلَيْهِمْ»

“Mayahudi watapigana nanyi, na ninyi mtawashinda.”

  • Tatu: Katika kufunguliwa kwa Roma, kwa idhini ya Allah.

Ahmad amepokea katika Musnad yake na Al-Hakim, na ilisahihishwa na kuidhinishwa na Az-Zhahabi kutoka kwa Abi Qabeel, amesema: Tulikuwa na Abdullah bin Amr ibn al-Aas: Amesema: Wakati tukiwa tumemzunguka Mtume wa Allah (saw) tukiandika, Mtume wa Allah (saw) aliulizwa: “Ni mji gani kati ya miji miwili utafunguliwa kwanza: Constantinople au Roma?” Mtume wa Allah (saw) akasema:

«مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلًا، يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ»

“Mji wa Heraclius utafunguliwa kwanza, yaani Constantinople.”

Constantinople ilifunguliwa, na Roma itafunguliwa, Allah akipenda.

Ndugu zangu wapendwa, kutafakari juu ya yaliyotajwa hapo juu kwa akili timamu na ufahamu wa busara ni matumaini baada ya maumivu, na furaha na bishara baada ya hali ya kusikitisha, na wepesi baada ya dhiki, na furaha baada ya mateso marefu sana, na kushuka kwa dua na rehema za Allah baada ya "hakika sisi ni wa Allah na Kwake tutarejea"... Kisha kheri na ushindi... kheri na ushindi... kisha kheri na ushindi.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo waumini watafurahi. Kwa ushindi wa Allah. Humvusha ampendaye, naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS. Ar-Rum [30]: 4-5)

Kwa kuhitimisha, namuomba Subhaanahu kwamba Eid hii ya kheri na baraka irejee wakati Umma wa Kiislamu ukiwa chini ya kivuli cha Raayah (bendera) ya Khilafah Rashidah, Raayah ya Laa Ilaaha Illallah Muhammadur Rasoolullah.

Na namuomba Allah (swt) kwamba wanachama wa Hizb ut Tahrir wawe mstari wa mbele katika Umma huu, wakisimama nao chini ya kivuli cha Khilafah Rashidah… Ama kwa wanachama waliofariki kabla ya kurejea kwa Eid hii, namuomba Allah (swt) awape nafasi chini ya kivuli Chake katika siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa Chake (swt). Allah ni Ar-Rahman Ar-Rahim.

Katika tamati yangu ya mwisho, nawapelekea Salamu zangu, na nawaombea Dua ya kheri kwenu.

Wasalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuhu.

Ndugu yenu,

Usiku wa 10 Dhul Hijjah 1439 AH Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Sawia na 21/08/2018 CE Ameer wa Hizb ut Tahrir

Share Article

Share this article with your network