Home About Articles Ask the Sheikh
Uchambuzi

Risala kutoka kwa Amir wa Hizb ut-Tahrir kwenda kwa Wabeba Da’wah

March 01, 2018
4724

AlhamduliLLah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, na maswahaba zake na waliomfuata. Baada ya hapo,

Ndugu wapendwa, enyi wabeba da’wah watukufu,

Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Enyi ndugu, huko nyuma nilikuwa nimewaandikia hivi: (Na mimi hapa sitaki kuwazuia ninyi kusoma nyaraka hizo mbaya, wala sikuamrisheni wala sikuwakatazeni, lakini ninachowaamrisha na kukisisitiza ni kwamba msinitumie chochote katika nyaraka hizo mbaya, kwani ninataka nishughulike na uzuri wa mwendo na unyofu wa njia, ili msafara ufikie ukiwa umebeba mwenge wa nuru hadi pale ulipo makao yake, Khilafah Rashidah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu katika muda ambao Mwenyezi Mungu ameuamua na kuukadiria, na kila muda una maandiko yake... Na ninamuomba Mwenyezi Mungu (swt) asiufanye muda huo kuwa mbali):

إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا

"Hakika Mwenyezi Mungu atatiza amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu amekujaalia kila kitu na kipimo chake." (QS At-Talaq [65]: 3).

Na nilipenda msiwe na shughuli ya kuwajibu watu hao, kwani wao ni kama bidhaa duni/chakavu ambazo kila unapozigeuza na kuziangalia unazipa uhai na zinakushughulisha na yale yaliyo kheri... Lakini nilijua kuwa mnakithiri kuwajibu!

Ninajua kuwa mlikuwa mkiwajibu ili kubainisha uzushi na uongo wao, pengine majibu yenu yakawabainishia ukweli kisha wakafaidika na majibu hayo na kuacha upotofu wao. Lakini jambo hili lingewezekana ikiwa wangekuwa wanasema uzushi huo kwa ujinga na si kwa makusudi. Lakini wanasema kwa uongo wa makusudi na kwa kudhamiria, kama walivyofanya wafuasi wao kabla yao kwa kuzua uongo... Na walitaka majibu, tukawaambia wakati huo: (Msemaji wa uzushi huu ni mmoja kati ya wawili: mmoja anayesema kwa uongo wa makusudi na huyu hakusema huku akitaka jibu la kufaidika nalo, na mwingine anayesema huku akiwa amepoteza uoni na ufahamu na huyu haidiki na jibu lolote), basi hawa hali yao ni kama ya wafuasi wao wa awali...

Pia ninajua kuwa mlikuwa mkiwajibu kwa kuchelea athari za uzushi wao ndani ya Hizb wasije wakailetea madhara, au wakaathiri uongozi wa Hizb kwa wale wanaosoma nyaraka zao mbaya. Na jambo hili haliwezi kutokea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu:

  • Ama kuhusu athari yao ndani ya Hizb, walijaribu kufanya hivyo wale waliokuwa na nguvu zaidi kuliko wao na kundi kubwa zaidi... Walijaribu wakoloni makafiri, na wakajaribu vibaraka wao madhalimu, na vyombo vya ujasusi vya hawa na wale vilijaribu, na licha ya hayo yote, wote walishindwa katika kamari yao na kufa kwa chuki zao. Na Hizb bado imesimama kidete juu ya haki, hadhuriki na yule anayeitelekeza wala yule anayeanguka kutoka kwenye msafara wakati msafara huo unashika kasi katika mwendo wake bila ya kudhoofika wala kulegea, bali unakwenda katika mstari ulionyooka usio na upogo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Mwenye Hekima.

  • Ama kuhusu uongozi wa Hizb, uko thabiti juu ya haki kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, azma yake haidhoofiki wala hailegei. Unapanda kutoka kilele kimoja hadi kingine, hauathiriwi na kila aliyeanguka au anayepiga kelele. Bali una uhakika kuwa ushindi unakuja In Shaa Allah, lakini kupitia mikono ya watu wema na watukufu kama maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, kwa sababu ushindi utakuwa ni Khilafah juu ya njia ya Utume, yaani kama Khilafah ya kwanza iliyosimama kupitia mikono ya maswahaba wale watukufu (ra). Na kwa hiyo, kila wanapoanguka katika msafara wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi, basi ushindi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu unakuwa umekaribia...

Hivyo basi, msiihofie Hizb wala uongozi wake kutokana na watu hao; si kutokana na kelele za wakubwa wao wala vilio vya wadogo wao. Kwani kama Alivyosema (swt) kwa Mtume Wake ﷺ:

إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ

"Hakika Sisi tunakutoshelezea dhidi ya wenye kufanya kejeli." (QS Al-Hijr [15]: 95).

Basi sisi tuna uhakika kuwa Mwenyezi Mungu atawatoshelezea waja Wake waumini dhidi ya shari ya wenye kufanya kejeli, wazushi na waongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Mtukufu, na Yeye (swt) ndiye anayewalinda watu wema...

Enyi ndugu wapendwa, enyi wabeba da’wah watukufu,

Kumbukeni daima aya hizi mbili tukufu:

  • إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ "Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walioamini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini anayekanya neema." (QS Al-Hajj [22]: 38). Basi ni ulinzi upi unaoweza kusimama mbele ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu Mlipiza Kisasi na Jabari...?

  • Na kauli Yake (swt): إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ "Hakika Sisi bila shaka tunawanusuru Mitume wetu na walioamini katika uhai wa duniani na siku wataposimama mashahidi." (QS Ghafir [40]: 51). Basi Mwenyezi Mungu hawanusuru Mitume Wake pekee, bali pia "na walioamini". Na ushindi si "siku wataposimama mashahidi" pekee, yaani Akhera kwa radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo ya Firdaus, bali pia "katika uhai wa duniani" kwa utukufu na tamkin (ushindi na mamlaka)... Basi msikate tamaa, enyi ndugu, na rehema ya Mwenyezi Mungu hata dhiki ifikie kiasi gani, bali dhiki ni ishara ya faraji, na giza la usiku ni ishara ya kuchomoza kwa alfajiri:

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا * إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا

"Basi hakika pamoja na dhiki kuna faraji. Hakika pamoja na dhiki kuna faraji." (QS Ash-Sharh [94]: 5-6). Na dhiki moja haishindi faraji mbili.

Kisha kurejea pale nilipoanzia: Kama nilivyowaamuru kuwa (msinitumie chochote katika nyaraka hizo mbaya), basi napenda kwenu msiwe na shughuli ya kuwajibu, kwani wao ni duni mno kwenu kuliko hivyo. Jishughulisheni na mambo ya da’wah na kuinuka kwake na waacheni hao waendelee kupotea katika upotofu wao...

Jazeni kurasa zenu na yale yanayoinua hadhi ya da’wah... Jazeni kurasa zenu na yale yanayopeleka kazi mbele... Jazeni kurasa zenu na yale yanayowafaa watu... Jazeni kurasa zenu kwa kufichua vitimbi vya wakoloni makafiri, vibaraka wao madhalimu, na vyombo vyao vya ujasusi vinavyowasaka waja wa Mwenyezi Mungu waumini... Wala msishughulike na mambo ya bidhaa duni kwani wao ni duni mno kiasi cha kuwashughulisha. Wala msidanganyike na namba zilizo kwenye kurasa zao, kwani wao ni kama yule anayeandika (moja) kisha anaweka baada yake (moja mwingine) akaonekana kama ni kumi na moja au mia na kumi na moja! Vyovyote iwavyo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba miongoni mwao hakuna mwanachama (A’dhu ‘Amil) anayefanya kazi ndani ya Hizb, bali wao ni ama mwanachama aliyevunja ahadi (Nakith), au aliyeacha, au aliyeadhibiwa, au mnafiki anayeonyesha kuipenda Hizb na kuisifu, na wakati huo huo anakula mali ya yatima na kuifanyia vitimbi Hizb, uongozi wake na viongozi wake wote... Katika hayo yote kuna dalili ya usafi wa Hizb na kutakata kwake, na uimara wa msimamo wa uongozi wake katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake ﷺ, na hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.

Katika kuhitimisha, haya ni maneno mawili ambayo mwenye kuyaelewa atatambua mwisho wake utakuwaje:

La kwanza ni kwa wakoloni makafiri, vibaraka wao na vyombo vyao vya ujasusi: wasifurahie fitna hii iliyotokea, nayo haiko mbali na vidole na nyuzi zao, sawa wawe wao ndio washonaji walioifuma na kuishona kwa mikono yao, au hawakuwa hivyo, bali walitega nyavu na nyuzi zao zikanaswa na watu waliopoteza uoni na ufahamu, kukatokea yaliyotokea... Nawaambia wasifurahie fitna yao, kwani Mwenyezi Mungu Mlipiza Kisasi na Jabari yuko macho dhidi ya watu wa shari:

حَتَّى إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُمْ بَغْتَةً فَإِذَا هُمْ مُبْلِسُونَ

"Hata walipofurahia yale waliyopewa, tuliwashika kwa ghafla, na mara hiyo wakawa wenye kukata tamaa." (QS Al-An'am [6]: 44).

Na lau kama waovu hao wangekuwa na akili wangezingatia matukio ya kuvunjwa kwa ahadi ambapo Hizb baada yake iliongezeka nguvu na uungaji mkono, lakini wao hawaelewi.

La pili ni kwa wenye fitna: Katika mazungumzo na baadhi ya wenzangu kuwahusu, ilielezwa kuwa kuna miongoni mwao wanaostahili kufukuzwa (Fasl), na hili ni kweli. Lakini nilipendelea isitokee hivyo, na badala yake kutosheka na adhabu waliyo nayo sasa ya kupuuzwa kikamilifu na kuenezwa kwa jambo hilo, huenda wakajirudi, au wakatubu na kuomba msamaha na kuirejesha mali ya yatima waliyoifanyia khiyana, wairejeshe kwa wenyewe... Hata kama hayo yote ni mambo yaliyo mbali kutarajiwa kutoka kwa watu waliozama kwenye upotovu na fitna, lakini:

مَعْذِرَةً إِلَى رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

"Ili iwe ni udhuru mbele ya Mola wenu Mlezi, na huenda wakacha Mungu." (QS Al-A'raf [7]: 164).

Na mwisho wa hitimisho, ninarudia (napenda msiwe na shughuli ya kuwajibu watu hao, kwani wao ni kama bidhaa duni/chakavu ambazo kila unapozigeuza na kuziangalia unazipa uhai na zinakushughulisha na yale yaliyo kheri...). Na ninamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atuepushe na shari ya Aliyoyahukumu, na atulinde na shari ya viumbe Vyake vyote, na atutukuze kwa utukufu Wake, na atufungulie ufunguzi utakaotuliza nyoyo na kufurahisha vifua, na kuwafurahisha watazamaji, na jambo hilo kwa Mwenyezi Mungu si gumu.

Wassalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

13 Jumada al-Akhirah 1439 H Ndugu yenu, Ata bin Khalil Abu al-Rashtah
1 Machi 2018 M

Share Article

Share this article with your network