Alhamdu Lillahi wa Salaatu wa Salaamu 'ala Rasoolillahi wa 'ala Aalihi wa Sahbihi wa Man Waalah, wa Ba'd:
Kwa Ummah wa Kiislamu kwa ujumla... na kwa wabeba da’wah wa kurejesha Khilafah Rashidah hususan...
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh
Katika siku kama ya leo, tarehe 28 Rajab mwaka 1342 Hijiria, sawia na tarehe 3 Machi 1924 Miladi, yaani miaka mia moja na miwili ya Hijiria iliyopita, makafiri wakoloni wakiongozwa na Uingereza wakati huo, na kwa ushirikiano na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, walifanikiwa kuivunja Dola ya Khilafah. Mustafa Kemal alifanya jinai ya ukafiri wa wazi (kufr bawwah) kwa kuifuta Khilafah mjini Istanbul, kumzingira Khalifa na kumfukuza alfajiri ya siku hiyo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, ambapo msiba huu mchungu ulitokea katika nchi za Waislamu kwa kuvunjwa kwa Khilafah... Ilikuwa ni wajibu kwa Ummah kupambana na mfanyaji wa ukafiri huo wa wazi kwa upanga, kama ilivyokuja katika hadithi ya Mtume ﷺ iliyopokelewa na ‘Ubadah bin al-Samit (ra):
وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ
"Na kwamba tusigombee madaraka na wenye nayo, isipokuwa mkiona ukafiri wa wazi (kufr bawwah) ambao mnao ushahidi kutoka kwa Allah juu yake." (Bukhari na Muslim)
Lakini Ummah haukusimama kwa namna ambayo ingemtetemesha mhalifu huyo na wasaidizi wake na kuwafanya washindwa, badala yake radiamali ilikuwa dhaifu na haikufikia kiwango hicho!
Tangu hapo, historia ya Ummah ikawa giza. Baada ya Khilafah kuwa dola yake ya haki na uadilifu, nchi zake sasa zimekuwa vipande zaidi ya hamsini, na uhasama kati ya watawala wake ni mkubwa. Hata tetemeko la ardhi la Syria na Uturuki, pamoja na ukali wake katikati ya mwezi huu, halikuweza kuondoa mifarakano yao na kurejesha umoja wao katika dola moja, bali waliendelea katika mgawanyiko wao kabla na baada ya tetemeko hilo, bila kukumbuka!
أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُون
"Je, hawaoni kwamba wanatiwa mtihani kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu wala hawakumbuki." (QS. At-Tawbah [9]: 126)
Pamoja na hayo, tetemeko hilo limefichua kuwa Uislamu umekita mizizi ndani ya nyoyo za Waislamu wa kawaida. Walikuwa wakikumbusha ukuu wa Allah (wakipiga Takbir) huku wakiwaokoa ndugu zao kutoka chini ya vifusi, hususan walipokuwa wakimwokoa mtoto aliyezaliwa na mama yake aliyefariki chini ya vifusi... au yule aliyefunikwa na vifusi huku mkono wake ukionekana ukiwa umeshika tasbihi aliyokuwa akimdhukuru kwayo Allah... au walipokuwa wakijaribu kumtoa mwanamke chini ya jengo lililobomoka, naye akaomba kabla ya kutolewa kwanza apewe vazi la kichwa (hijabu) ili nywele zake zisifunuke... au yule waliyekuwa wakimwita kutoka chini ya magofu ili wamtoe, naye akaomba kwanza maji kwa ajili ya udhu na swala ili asipitwe na wakati... kisha yule wanayejaribu kumwokoa kati ya mabaki ya jengo wakimkuta akisoma Qur'ani kutoka Surat al-Baqarah... au yule binti ambaye wakati wakijaribu kumtoa alionyesha huzuni yake kwa sababu hakuweza kuswali swala ya siku hiyo... na wakati wa yote hayo, Takbir zinasikika... Allahu Akbar... Hawa ndio Waislamu. Allah amrehemu kila Mwislamu aliyefariki wakati wa tetemeko hilo na tunamuomba Allah awe miongoni mwa mashahidi wa Akhera, na Allah awashifu majeruhi shifaa isiyoacha ugonjwa... Na Allah amsaidie kila Mwislamu aliyenusurika, na amwandikie maisha mema atakayoyatumia katika kumtii Allah (swt) na kumtii Mtume Wake ﷺ.
Hawa ndio Waislamu na wale ndio watawala katika nchi za Waislamu, na kati yao kuna umbali mkubwa. Tofauti hii yote imetokea katika miaka hii mia moja na miwili tangu msiba mkuu wa kuvunjwa kwa Khilafah! Baadaye, makafiri wakoloni wakitumia kutoweka kwa Khilafah, waliongeza msiba mwingine mchungu: waliwapa mayahudi dola katika Ardhi Iliyobarikiwa, mahali pa safari ya usiku ya Mtume ﷺ (Isra) na kupaa kwake (Mi’raj), na wakawapa nyenzo za kubaki. Sababu ya kwanza ya nyenzo hizo ni kulinda usalama wake kupitia watawala vibaraka wanaoizunguka. Walikuwa wakishindwa mbele ya mayahudi katika kila vita vilivyozuka hadi wakaipa dola ya mayahudi sura tofauti na ile aliyowaelezea kwayo Allah:
وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَة
"Na wakapigwa (wakagubikwa) na udhalili na unyonge." (QS. Al-Baqarah [2]: 61)
Watawala hawakuishia hapo, bali walitumia kila juhudi kuhamisha kadhia hii kutoka kwenye kuondoa chombo cha mayahudi hadi kwenye mazungumzo nacho, labda kitajiondoa katika sehemu ya kile kilichokikalia kwa mabavu mwaka 1967!
Isitoshe, dola ya mayahudi ilikuwa na inaendelea kufanya jinai mbaya zaidi nchini Palestina. Mauaji ya kinyama, bali simulizi ya kishujaa ya Jenin mnamo 26/01/2023 ni ushahidi wa hilo. Jeshi la chombo cha mayahudi likiwa na vikosi vikubwa vilivyojaa silaha lilivamia kambi ya Jenin na kutekeleza mauaji ambapo mashahidi tisa waliuawa. Wakati huo, walifanya jinai mbaya zaidi kwa kuua, kubomoa kuta juu ya majeruhi, na kuwakanyaga kwa tingatinga (bulldozers). Kisha likaendelea na uchokozi wake huko Nablus, na kuvamia kambi ya Aqbat Jabr likaua na kujeruhi... Yote haya yanatokea bila watawala katika nchi za Waislamu kuchukua hatua ya kuwaokoa, bali mbora wao alikuwa yule aliyetangaza upatanishi wake kati ya mhalifu na aliyefanyiwa jinai; Allah awalaani, wanageuzwa wapi! Na watafanyaje zaidi ya hapo wakati wanakimbilia kufanya jinai ya kurejesha uhusiano wa kawaida (normalization) na mayahudi? Baada ya watawala wa Misri kuongoza msafara huu wa udhalili na unyonge, walifuatiwa na Mamlaka (PLO) na watawala wa Jordan, kisha Imarati, Bahrain, na Morocco... Na sasa huyu Sudan anajiunga nao katika jinai hiyo, kwani Al-Burhan, rais wa Sudan, alimpokea waziri wa mambo ya nje wa mayahudi Eli Cohen huko Khartoum mnamo 02/02/2023 ili kujadili kurejesha uhusiano!! Na wote hawa hawajali udhalili unaowazunguka:
سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ
"Itawafika wale waliofanya jinai udhalili mbele ya Allah na adhabu kali kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyapanga." (QS. Al-An'am [6]: 124)
Cha ajabu ni kwamba, pamoja na kila uchokozi au kila jinai inayofanywa na chombo cha mayahudi, viongozi wake huwa, katika siku zilizopita au siku hiyo hiyo, wako vifuani mwa watawala wa Kiarabu au katika ziara kwao. Netanyahu alikuwa mgeni katika kasri ya utawala wa Jordan muda mfupi kabla ya jinai ya Jenin! Wakati wa jinai ya Jenin, Mamlaka ya Palestina ilikuwa ikishirikiana kiusalama na mayahudi, na kwa kukiri kwao wenyewe kwa sababu walidai kuwa watasitisha ushirikiano wa kiusalama baada ya jinai hiyo; hivyo basi ushirikiano ulikuwepo! Lakini la kustaajabisha na la ajabu zaidi ni kwamba pindi shujaa miongoni mwa mashujaa wa Palestina anaposimama kuitetea nchi yake na watu wake na kuua mayahudi saba katika operesheni ya Al-Quds baada ya mauaji yale, watawala katika nchi za Waislamu wanakimbilia kulaani! Wizara za mambo ya nje huko Uturuki, Imarati, Jordan na Misri zililaani operesheni hiyo ya Al-Quds katika taarifa zao kwa vyombo vya habari!!
Vilevile, si Palestina pekee iliyochomwa kisu na watawala hawa, bali pia walisalimisha au kutoa maeneo mengine matukufu ya ardhi ya Uislamu. Kashmir imenyakuliwa na washirikina wa Kihindu na kuunganishwa na dola yao huku watawala wa Pakistan wakiwa kimya... Waislamu wa Rohingya wanachinjwa huko Myanmar (Burma) na watawala wa Bangladesh ni kama wamelala hawaoni... kisha Turkestan Mashariki ambako Uchina inafanya mauaji ya kimbari, na nchi zilizopo katika ardhi za Waislamu ziko kimya kama makaburi, na pindi zinapozungumza husema kuhusu mauaji hayo kuwa ni suala la ndani la Uchina!
كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً
"Ni neno kuu hilo linalotoka vinywani mwao; hawasemi ila uongo tu." (QS. Al-Kahf [18]: 5)
Kisha makafiri wakoloni hawakutosheka na udhalili waliouingiza kwa Ummah, bali walithubutu kushambulia itikadi yake. Mwenye msimamo mkali Paludan alichoma nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya jengo la ubalozi wa Uturuki huko Stockholm mnamo Jumamosi 21/01/2023, baada ya mamlaka ya Sweden kuruhusu hilo... Kisha jinai zao zikaendelea kwa kuchoma Qur'ani huko The Hague na huko Copenhagen mnamo Ijumaa 27/01/2023. Baada ya hapo, Al-Azhar kupitia kitengo chake cha ufuatiliaji ilitoa taarifa kali ikilaani na kutaka kusimama dhidi ya majaribio ya kuchezea matukufu ya kidini... Hapana shaka kuwa wanachuoni wa Al-Azhar wanajua kuwa radiamali ya kuchomwa kwa Qur'ani haiwi kwa kulaani kwa maneno tu, bali ni lazima majeshi yachukue hatua kunusuru Kitabu cha Allah na dini Yake. Kuchomwa kwa Qur'ani ni kutangaza vita dhidi ya Ummah wa Kiislamu na itikadi yake, hivyo radiamali yake iwe ni vita vitakavyowatawanya wale walio nyuma yao:
فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُون
"Basi ukiwakuta vitani, watishe kwa (kuwaadhibu) wale walio nyuma yao ili wapate kukumbuka." (QS. Al-Anfal [8]: 57)
Enyi Waislamu: Uchokozi dhidi ya Waislamu haukabiliwi na maneno yenye nakshi kwa nje lakini matupu kwa ndani ambayo hayanenepeshi wala kutosheleza dhidi ya njaa. Badala yake, uchokozi unajibiwa kwa ukali wa upanga, kwa mapigo yanayomfanya adui asahau wasiwasi wa shetani... Hivyo ndivyo walivyokuwa Waislamu walipokuwa na Khilafah, na matukio ya kihistoria katika zama zao yanashuhudia hilo... Mifano yake iko wazi katika historia ya Waislamu iliyopokelewa na vitabu kama (Al-Bidaya wa al-Nihaya cha Ibn Kathir, Futuh al-Buldan cha al-Baladhuri, Tarikh Ibn Khaldun, Tarikh al-Islam cha al-Dhahabi, na vyanzo vinginevyo). Nitawanukulu baadhi yayo:
(- Kisha ukaingia mwaka 87 Hijiria... Ambapo Qutayba bin Muslim alivamia Baikand, miongoni mwa vitongoji vya Bukhara... Na kabla ya nusu ya mchana Allah aliwateremshia ushindi... Na aliyekuwa akiwachochea watu dhidi ya Waislamu alikuwa ni mtu mmoja chongo miongoni mwao, alipotekwa akasema: Mimi nitajikomboa kwa nguo elfu tano za Kichina zenye thamani ya milioni moja (dirham). Makamanda wakamshauri Qutayba akubali hilo, lakini Qutayba akasema: "La wallahi, hutamtia hofu Mwislamu yeyote kwa mara ya pili," na akaamuru akatwe kichwa chake.)
(- Kisha ukaingia mwaka 90 Hijiria... Ambapo Dahir, mtawala wa Sindh, alishambulia meli iliyokuwa na wanawake wa Kiislamu na kuwachukua kama mateka. Khalifa akamtuma liwali wake kulipiza kisasi kwa dhalimu huyo. Muhammad bin Qasim akaongoza jeshi, akawaokoa wanawake wa Kiislamu na kumlipiza kisasi mtawala huyo mtwaguti na kuifungua nchi ya Sindh.)
(- Kisha ukaingia mwaka 223 Hijiria, mfalme wa Kirumi akatoka kuelekea nchi za Waislamu na kuua na kuteka watu wa Zibatra... Mwanamke mmoja akapiga ukelele akisema "Wa Mu'tasimah" (Ewe Mu'tasim nisaidie). Habari hiyo ikamfikia Khalifa al-Mu'tasim naye akajibu "Labbaiki" (Nimeitika mwito wako), akaongoza jeshi na kumfanyia kisasi mwanamke huyo... Akauliza: Ni mji gani wa Kirumi ulio mkuu zaidi? Akaambiwa ni Amorium (karibu na Ankara) naye akaifungua.)
(- Kisha ukaingia mwaka 582 Hijiria... Ambapo Arnat (Raynald wa Châtillon), bwana wa Karak, alifanya usaliti kwa kuvizia msafara mkubwa (wa mahujaji) uliokuwa ukitoka Misri, akaua na kuteka. Sultan Salahuddin akajiandaa kwa vita dhidi yake, akaitisha wanajeshi kutoka nchi mbalimbali, na akaapa kuwa akimshinda atamuua kwa mkono wake mwenyewe. Allah akampa ushindi dhidi yake mwaka 583 Hijiria katika vita vya Hattin katikati ya mwezi wa Rabi' al-Akhir, na Salahuddin akamuua kwa mkono wake mwenyewe kama malipo ya usaliti wake na kuvizia misafara. Kisha ukafuatia ukombozi wa Al-Aqsa mnamo 27 Rajab 583 Hijiria.)
(- Kisha mnamo 1307 Hijiria (1890 Miladi), mtunzi wa riwaya moja alimzulia uongo Mtume wa Allah ﷺ na kujaribu kuionyesha katika moja ya kumbi za maonyesho mjini Paris. Khalifa Abdul Hamid alipopata habari hiyo, alimwita balozi wa Ufaransa huko Istanbul na akakusudia kumpokea akiwa amevaa vazi la kijeshi. Kisha akamtishia kuwa ikiwa itaonyeshwa, Dola ya Osmania itatangaza kuvunja uhusiano na Ufaransa kama hali ya vita, na akamhutubia kwa sauti kali: "Mimi ni Khalifa wa Waislamu... Nitaupindua ulimwengu juu ya vichwa vyenu ikiwa hamtasitisha mchezo huo". Ufaransa ikaitikia na kupiga marufuku maonyesho hayo...)
Makafiri wakoloni walikuwa wakitambua wakati huo kuwa uvunjaji wowote wa heshima ya Uislamu na Waislamu utakabiliwa na kukatwa ndimi na kuvunjwa miguu... Lakini leo Qur'ani Tukufu inashambuliwa, Mtume ﷺ anashambuliwa, na nchi za Waislamu zinavamiwa na uchokozi huo haujibiwi! Na yote hayo ni kwa sababu ya kukosekana kwa Imamu, Khalifa Rashid anayelinda Ummah dhidi ya shari ya maadui... Imekuja katika hadithi sahihi iliyokubaliwa:
إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ، يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ، وَيُتَّقَى بِهِ
"Hakika Imamu ni ngao, hupigwa vita nyuma yake na hulindwa kwayo." (Bukhari na Muslim)
Mwishoni, ninarudia kuelekeza mwito kwenu enyi watu wa nguvu na ulinzi (Ahlu al-Quwwah wa al-Man'ah)... Ni nyinyi pekee mnaoweza kuponya vifua vya Ummah dhidi ya maadui zake, ambao ni maadui wa dini yenu. Ni nyinyi pekee mnaoweza kuvunja udhalili ambao Waislamu wameufikia katika nchi zao... Basi simameni kutekeleza wajibu wenu, Allah awabariki. Simameni kutunusuru, kunusuru Hizb ut-Tahrir kusimamisha Khilafah Rashidah. Kwani hiyo siyo tu njia ya ushindi kwa mtazamo wa kuelezea uhalisia, bali kwa daraja ya kwanza ni faradhi kuu. Na yeyote asiyefanya kazi huku akiwa na uwezo wa kusimamisha Khilafah na kumpata Khalifa anayestahiki kupewa bay'ah, basi dhambi yake ni kubwa kana kwamba amekufa kifo cha kijahilia kama kielelezo cha ukali wa dhambi hiyo, kama alivyosema ﷺ:
وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً
"Na yeyote atakayekufa na huku shingoni mwake hamna kiapo cha utii (bay’ah), basi amekufa kifo cha kijahilia." (Muslim)
Pili, Waislamu walianza kwa kutoa bay'ah kwa Khalifa kabla hawajaanza kumwandaa Mtume wa Allah ﷺ na kutekeleza faradhi ya kumzika, na yote hayo ni kwa sababu ya umuhimu wa Khilafah... Na tatu, Umar (ra) siku ya kufa kwake aliweka muda wa kumchagua Khalifa kutoka kwa wale sita waliobashiriwa pepo kuwa ni siku tatu zisizozidi, na ikiwa hawataafikiana kwa Khalifa ndani yake basi anayepinga auawe. Hilo lilikuwa mbele ya masahaba na hapakuripotiwa yeyote aliyepinga, hivyo ikawa ni ijma’ (mwafaka) wa masahaba. Na sisi tayari zimepita kwetu "nyingi ya hizo siku tatu"! Hivyo basi, kusimamisha Khilafah ni jambo kuu sana.
Enyi Wanajeshi wa Allah: Tunatambua kuwa hawatashuka malaika kutoka mbinguni kutusimamishia Khilafah, bali Allah huteremsha malaika kutusaidia ikiwa tutafanya kazi kwa bidii kusimamisha Khilafah. Nayo ni ahadi ya kweli katika Kitabu cha Allah:
وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ
"Allah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao." (QS. Al-Nur [24]: 55)
Na ni bishara ya utukufu katika hadithi ya Mtume wa Allah ﷺ baada ya utawala huu wa kidikteta (mulkan jabriyyah), anasema ﷺ:
...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ
"...kisha utakuwepo utawala wa kidikteta (mulkan jabriyyah) utakaodumu mpaka pale Allah atakapopenda uishe, kisha Allah atauondoa anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume (Khilafah ‘ala Minhaj al-Nubuwwah)." (Ahmad)
Kisha akanyamaza ﷺ. Na tunatambua pia kuwa maadui wa Uislamu wataona kuwa kusimamisha Khilafah upya ni jambo lisilowezekana, na wanakariri kauli ya wafuasi wao wa zamani kwa kejeli:
غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ
"Dini yao imewahadaa hawa." (QS. Al-Anfal [8]: 49)
Lakini kama vile kauli hiyo ilivyokuwa maangamizi kwa wataji wake, na Allah akaipa nguvu dini Yake na kuwanusuru watu Wake, vivyo hivyo leo itakuwa maangamizi kwao. Kwani Allah, Mwenye Nguvu na Mwenye Hekima, yuko pamoja na waja Wake wenye ikhlasi wanaofanya kazi kwa bidii, bila ya nyoyo na viungo vyao kuachana na kauli Yake Ta'ala:
إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً
"Hakika Allah anatimiza jambo Lake. Hakika Allah amejalia kwa kila kitu kipimo chake." (QS. Al-Talaq [65]: 3)
Hawa, kwa kila siku inayopita, wanakaribia "kipimo" hiki kwa idhini ya Allah...
وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً
"Na watasema: Lini hayo? Sema: Huenda yakawa karibu." (QS. Al-Isra [17]: 51)
Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh
28 Rajab 1444 H Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu al-Rashtah 19/02/2023 M Amiri wa Hizb ut-Tahrir