Home About Articles Ask the Sheikh
Uchambuzi

HOTUBA YA AMIR WA HIZB UT-TAHRIR, MWANACHUONI MTUKUFU ATA BIN KHALIL ABU AL-RASHTAH KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 99 YA KUANGUKA KWA DOLA YA KHILAFAH

March 22, 2020
6469
استمع للمقال

Alhamdullilah, na swala na salamu zimwendee Mtume wa Allah, jamaa zake na maswahaba wake na waliomfuata. Baada ya hayo:

Kwa Ummah wa Kiislamu kwa ujumla ambao Allah ameujaalia kuwa Ummah bora uliotolewa kwa watu... na kwa vijana wa Hizb ut-Tahrir hasa ambao Allah amewakirimu kwa kubeba da’wah yake kwa ukweli na ikhlasi... na kwa wageni wa ukurasa huu wanaoufuata kwa mapenzi ya kile ubebacho katika kheri na nuru... kwa hawa wote: Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh,

Katika siku kama hii miaka tisini na tisa iliyopita, mhalifu wa zama hizi, Mustafa Kemal, aliifuta Khilafah. Licha ya kwamba jambo hili lilikuwa wazi kweupe na limethibitika kwa ushahidi—tena kwa zaidi ya ushahidi mmoja—kuwa ni kufuru ya waziwazi (kufr bawwah) na kufutwa kwa hukumu ya Uislamu, jambo ambalo mtekelezaji wake anastahili kupingwa kwa upanga kwa mujibu wa hadithi ya Mtume wa Allah ﷺ iliyopokelewa na Bukhari na Muslim kutoka kwa Junada bin Abi Umayyah, amesema: Tuliingia kwa Ubaid bin as-Samit akiwa mgonjwa, tukasema: Allah akuzidishie kheri, tuhadithie hadithi ambayo Allah atakunufaisha kwayo uliyoisikia kutoka kwa Mtume ﷺ. Akasema: Mtume ﷺ alituita, tukampa baia, na miongoni mwa mambo aliyochukua kwetu ni:

أَنْ بَايَعَنَا عَلَى السَّمْعِ وَالطَّاعَةِ فِي مَنْشَطِنَا وَمَكْرَهِنَا وَعُسْرِنَا وَيُسْرِنَا وَأَثَرَةً عَلَيْنَا وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ

"Tupe baia ya kusikia na kutii katika hali ya wepesi na uzito, ya kupenda na kukuchukia, na hata kama tutadhulumiwa haki zetu, na tusiwanasue wenye mamlaka na uongozi wao, isipokuwa mtafapoona kufuru ya waziwazi (kufr bawwah) ambayo mna ushahidi kwayo kutoka kwa Allah."

Basi wajibu ulikuwa ni kupigana naye na kujitolea kila kilicho na thamani bila kujali gharama. Hata hivyo, mtawala huyu muovu hakukabiliwa na Ummah kwa yale aliyostahili ya kung’olewa mizizi yake! Kutokana na hilo, historia ya Ummah ambao ulikuwa Ummah bora uliotolewa kwa watu ikawa giza; ambapo awali ulikuwa na dola moja ya Khilafah yenye kuheshimika na kuogopewa kwa haki na uadilifu, lakini sasa umegawanyika katika vipande zaidi ya hamsini, uadui miongoni mwao ni mkubwa, wakitawaliwa na watu wasio na huruma nao wala wasiochunga mambo yao. Na si hayo tu, bali mambo yao yanashikiliwa na viongozi wapuuzi (ruwaybidhat) walio duni mbele ya makafiri na wanyenyekevu kwa wakoloni. Utajiri wao unaendesha uchumi wa maadui hao wa dini ya Allah, huku uchumi wa nchi na raia ukiwa umeporwa na kutaabika, watu wake hawanufaiki nao. Hali yao ni kama usemi usemavyo: (Kama ngamia jangwani wanaouawa na kiu huku maji yakiwa yamebebwa migongoni mwao). Haya yote yanatokea mbele ya macho na masikio ya hawa viongozi wapuuzi... Umaskini unasambaa miongoni mwa watu isipokuwa kundi la watawala na wafuasi wao ambao hupata ujira wao uliojaa udhalili kutokana na kuwatumikia mabwana zao wakoloni, ikiwa ni usaliti kwa Allah, Mtume Wake, na waumini, na kuzuia njia ya Allah, Mwenye nguvu na Mwenye hekima.

Enyi Waislamu, hakika Khilafah ni suala la kimsingi la kufa na kupona (qadhiyyah masiiriyyah) kwa Waislamu; kupitia kwayo mipaka ya kisheria husimamishwa, heshima hulindwa, ushindi na ukombozi hupatikana, na Uislamu na Waislamu hupata utukufu. Haya yote yameandikwa katika Kitabu cha Allah Mwenye nguvu na Mwenye hekima, Sunnah za Mtume Wake ﷺ, na Ijma’ ya Maswahaba wake (ra). Inamtosha Mwislamu kutafakari mambo matatu yafuatayo ili atambue jinsi faradhi ya Khilafah ilivyo kuu mno. Mambo hayo matatu ni haya yafuatayo:

Kwanza: Kauli yake (swala na salamu zimwendee) katika yale yaliyopokelewa na At-Tabarani katika Al-Mu’jam al-Kabir kutoka kwa Asim, kutoka kwa Abu Salih, kutoka kwa Muawiyah, amesema: Nilimsikia Mtume wa Allah ﷺ akisema:

مَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مَيْتَةً جَاهِلِيَّةً

"Mwenye kufa na hali hana baia (ahadi ya utii) shingoni mwake, amekufa kifo cha kijahilia."

Huu ni ushahidi wa ukubwa wa dhambi inayomwangukia Mwislamu mwenye uwezo ambaye hafanyi kazi kwa ajili ya kupatikana kwa Khalifah ambaye atakuwa na baia shingoni mwake. Yaani, ni ushahidi wa kuwepo kwa Khalifah ambaye anastahili kuwa na baia shingoni mwa kila Mwislamu kwa kuwepo kwake.

Pili: Ni kushughulika kwa Maswahaba wa Mtume wa Allah ﷺ katika kusimamisha Khilafah na kutoa baia kwa Khalifah kabla ya kushughulika na mazishi ya Mtume wa Allah ﷺ, licha ya kuwa kuharakisha mazishi ni jambo lililoamriwa kisheria. Imeelezwa katika Ma’rifat al-Sunan wa al-Athar ya Al-Bayhaqi: (Na Shafi’i amesema katika upokezi wa Abu Said: "Napenda kuharakisha mazishi ya maiti pindi kifo chake kinapothibitika"). Hii ni kwa maiti yeyote, basi itakuwaje ikiwa maiti huyo ni Mtume wa Allah ﷺ? Pamoja na hayo, Maswahaba walitanguliza kumpa baia Khalifah kabla ya kumzika Mtume wa Allah ﷺ. Hivyo, kumedhihiri msisitizo wa Ijma’ ya Maswahaba juu ya kusimamisha Khalifah kupitia kuchelewesha kwao mazishi ya Mtume ﷺ mara tu baada ya kifo chake na kushughulika kwao na kumteua Khalifah.

Tatu: Kwamba Umar (ra) siku ya kifo chake aliweka muda wa kumchagua Khalifah kutoka miongoni mwa wale sita waliobashiriwa pepo usiozidi siku tatu... Kisha akausia kwamba ikiwa hawatakubaliana juu ya Khalifah ndani ya siku tatu, basi yule atakayepinga auaye baada ya siku hizo tatu. Akawakabidhi wanaume hamsini miongoni mwa Waislamu kutekeleza hilo, yaani kumuua mpinzani, licha ya kuwa wao ni miongoni mwa waliobashiriwa pepo, ni watu wa Shura, na ni miongoni mwa Maswahaba wakubwa. Hilo lilitokea mbele ya macho na masikio ya Maswahaba, na hakuna yeyote aliyeripotiwa kupinga au kukataa jambo hilo. Hivyo, ikawa ni Ijma’ ya Maswahaba kwamba haijuzu kwa Waislamu kukaa bila Khalifah kwa zaidi ya siku tatu na mchana wake. Na sisi tayari tumepitiwa na "mfululizo mrefu wa siku tatu", wala hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa Allah... Hivyo basi, enyi Waislamu, Khilafah ni jambo kuu mno, na ni suala la kufa na kupona kwa Waislamu tena suala la kweli kweli.

Enyi Waislamu, pamoja na hayo, hatukati tamaa na rehema ya Allah:

إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِنْ رَوْحِ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ

"Hakika hawakati tamaa na rehema ya Allah isipokuwa watu makafiri." (QS Yusuf [12]: 87)

Hususan kwa kuwa Allah (swt) amewaahidi wale walioamini na kutenda mema kuwapa mamlaka (ukhalifa) katika ardhi:

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ

"Allah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, kwamba atawafanya makhalifa (watawala) katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale wa kabla yao." (QS An-Nur [24]: 55)

Vilevile, Mtume wa Allah ﷺ ametoa bishara ya kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala wa kidikteta ambao tuko nao sasa:

ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ

"Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume." (HR Ahmad kutoka kwa Hudhayfah bin al-Yaman (ra)).

Lakini tunasisitiza na kurudia yale tuliyoyasema hapo awali kuwa Allah Mwenye nguvu na Utukufu atatunusuru ikiwa tutainusuru dini Yake kwa kuwa miongoni mwa wafanyaji kazi wakweli na wenye ikhlasi. Kwani kanuni ya Allah imeelekeza kwamba hatoshusha malaika watakaofanya kazi kwa niaba yetu na kutusimamishia Khilafah hali ya kuwa tumekaa na kuegemea makochi! Bali Allah akipenda atashusha malaika wa kutusaidia tukiwa tunafanya kazi. Na hivi ndivyo Allah alivyoahidi katika kila ushindi, iwe ni katika kusimamisha Khilafah kwa uzuri wa kazi na ufanisi wake, au iwe ni katika ukombozi na nusra kutoka kwa Allah kwa kupigana katika njia Yake (swt).

Nasi tunamshukuru Allah kwa kuukirimu Ummah huu kwa kusimama kwa Hizb ut-Tahrir iliyojitolea kwa kazi nzito na ya ikhlasi, kwa idhini ya Allah, kwa ajili ya kuanza tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah. Nayo kwa haki ni kiongozi asiyewaambia uongo watu wake, na ni chama ambacho harufu yake nzuri inazidi kung’aa, na anayeanguka kutoka kwayo ni yule tu asiyeweza kuvumilia uzuri wake... Hivyo ndivyo tunavyokidhania na kuwadhania vijana wake wote wanaofanya kazi ndani yake kuwa ni wenye jitihada na bidii, wafanyaji kazi wenye ikhlasi, wanaotazamia Akhera kwa idhini ya Allah zaidi kuliko wanavyotazamia dunia. Wanaunganisha usiku na mchana wakitaraji rehema ya Allah ili ahadi Yake (swt) na bishara ya Mtume Wake ﷺ itimie kupitia mikono yao, na jambo hilo kwa Allah si gumu.

Na mwisho, faradhi ya kusimamisha Khilafah, enyi Waislamu, si kwa vijana wa Hizb pekee, bali ni kwa kila Mwislamu mwenye uwezo. Basi tuungeni mkono enyi Waislamu, na tunusuruni enyi majeshi ya Waislamu, na murejeshe mwenendo wa Answar walipoinusuru dini ya Allah, Allah (swt) akawafanya kuwa sawa na Muhajirina, akawasifu na kuridhika nao katika Kitabu Chake bila sharti, lakini akaweka sharti hilo kwa Tabi’ina kwa kuwafuata kwa wema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَداً ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

"Na wale waliotangulia mbele (katika Uislamu), miongoni mwa Wahajiri na Maansari, na wale waliowafuata kwa wema, Allah ameridhika nao na wao wameridhika Naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufanikiwa kukubwa." (QS At-Tawbah [9]: 100)

Hayo ni kutokana na kile ambacho nusra kwa dini ya Allah na kusimamisha Khilafah kuna ujira mkubwa na fadhila adhimu, kiasi kwamba malaika walibeba jeneza la Saad bin Muadh, kiongozi wa Maansari (ra) kama ilivyokuja katika Mustadrak ala al-Sahihayn ya Al-Hakim kutokana na ukubwa wa fadhila za kunusuru dini ya Allah.

Mwisho wa mwisho, hakika mwenye kunusuru kazi ya kusimamisha Khilafah kabla haijasimama, ujira wake ni mkubwa na adhimu zaidi kuliko kunusuru Khilafah baada ya kusimama kwake:

لَا يَسْتَوِي مِنْكُمْ مَنْ أَنْفَقَ مِنْ قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ أُولَئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِنَ الَّذِينَ أَنْفَقُوا مِنْ بَعْدُ وَقَاتَلُوا وَكُلّاً وَعَدَ اللَّهُ الْحُسْنَى وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

"Hawalingani miongoni mwenu wale waliofanya matumizi kabla ya ushindi (wa Makka) na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale waliofanya matumizi baada ya hapo na wakapigana vita. Na wote Allah amewaahidi wema. Na Allah anajua vyema yote mnayoyatenda." (QS Al-Hadid [57]: 10)

Na sisi tunamuomba Allah (swt) kwamba maadhimisho haya ya tisini na tisa yawe ni tangulizi la nusra adhimu ya Allah kabla ya maadhimisho ya karne moja ya kuvunjwa kwa Khilafah, na kisha Khilafah Rashidah iangaze ulimwenguni upya:

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo waumini watafurahi * Kwa nusra ya Allah; Hunusuru amtakaye, Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu." (QS Ar-Rum [30]: 4-5)

Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Jumatatu, 28 Rajab 1441 H / 23 Machi 2020 M

Ndugu yenu Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah
Amir wa Hizb ut-Tahrir

Share Article

Share this article with your network