Hotuba ya Amir iliyotolewa katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Hitimisho la kampeni ya Kumbukumbu ya Miaka Mia Moja tangu kuangushwa kwa Khilafah

| Kiarabu | Kiingereza | Kituruki | Kijerumani | Kiurdu |
| Kiswahili | Kirusi | Kiukreni | Kimalaysia |
Sifa zote njema ni za Allah, na swala na salamu zimshukie Mtume wa Allah, jamaa zake, maswahaba wake na waliomfuta, na baada ya hayo...
Kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla, na kwa wabeba da'wah kwa ajili ya kurejesha Khilafah Rashidah hususan, vijana wa kiume na wa kike...
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Katika siku kama hizi miaka mia moja iliyopita, mwishoni mwa Rajab 1342 H, sawia na mwanzoni mwa Machi 1924 M, makafiri wakoloni wakiongozwa na Uingereza wakati huo, kwa ushirikiano na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, walifanikiwa kuingamiza Dola ya Khilafah. Mujirimu wa karne hiyo, Mustafa Kemal, alitangaza kuvunjwa kwa Khilafah, kumzingira Khalifa jijini Istanbul na kumtoa nje alfajiri ya siku hiyo. Hiyo ilikuwa ni bei ambayo Uingereza ilimuamuru ailipe, ili amtawaze mkabala wa hilo kuwa rais dhaifu wa Jamhuri ya Uturuki ya kisekula. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, ambapo kulitokea mtetemeko mkubwa katika nchi za Waislamu kwa kuvunjwa kwa Khilafah, ambayo ndiyo chemchemi ya utukufu wao na radhi za Mola wao.
Mujirimu huyo alitangaza ukafiri wa wazi (kufra buwah) kwa kuifuta Khilafah baada ya kuwa ilikuwepo. Na ilikuwa ni wajibu kwa Umma kumpiga vita kwa upanga kama ilivyokuja katika Hadith ya Mtume ﷺ iliyopokelewa na Ubada bin al-Samit (ra):
وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ
"na tusizozane na wenye mamlaka juu ya jambo lao (uongozi), isipokuwa mkiona ukafiri wa wazi ambao mnao ushahidi kutoka kwa Allah juu yake." (Muttafaq 'alayhi)
Hata hivyo, ukandamizaji wake mkali uliomwaga damu za Umma, hasa wanachuoni—ambapo aliwanyonga wengi, miongoni mwao akiwa Sheikh Said Piran (rahimahullah) na kuwafunga wengine—yote hayo yalikuwa na athari katika kuufanya Umma usitekeleze kile ambacho kingemtetemesha mujirimu huyo na wasaidizi wake na kuwapindua wakiwa wenye hasara. Badala yake, majibu yalikuwa dhaifu, hayakufikia kiwango cha kumseta msaliti huyo wa Allah, Mtume Wake, na Waumini! Hivyo, mhalifu huyo wa kufra buwah "alinusurika" na kitendo chake kiovu bila Umma kumtupa mahali pa mbali sana!
Baada ya hapo, ushawishi wa makafiri wakoloni uliingia katika nchi za Waislamu, wakazigawa nchi na kuzipasua vipande vipande vilivyofikia takriban hamsini na tano. Hiyo ilikuwa ni matokeo ya mtetemeko wa kuanguka kwa Khilafah. Kisha wakaongeza mtetemeko mwingine juu ya huo, wakawapa Mayahudi dola katika ardhi iliyobarikiwa, mahali pa safari ya usiku ya Mtume ﷺ (Isra) na kupaa kwake (Mi’raj), na wakaipa kila sababu ya kuendelea kuwepo. Sababu ya kwanza kabisa ni kulinda usalama wake kupitia watawala vibaraka wanaoizunguka. Si hivyo tu, bali watawala hawa walikuwa wakishindwa mbele ya Mayahudi katika kila vita vilivyozuka hadi wakaipa dola ya Kiyahudi ukubwa zaidi ya ukubwa wake na sura isiyo sura yake. Hawakuishia hapo, bali walitumia kila juhudi kumpiga vita Allah na Mtume Wake ili kuhamisha kadhia kutoka katika kuung'oa umbo la Kiyahudi Palestina hadi kwenye mazungumzo na umbo hilo ili labda lijiondoe katika baadhi ya maeneo iliyoyakalia mwaka 1967! Kisha wakashuka daraja baada ya hapo na kukimbilia katika kuhalalisha mahusiano (at-tatbi’) na umbo la Kiyahudi hata bila hilo kujiondoa katika lolote! Baadhi yao walifanya jinai hiyo ya kuhalalisha mahusiano kisirisiri, na wengine wakaifanya waziwazi usiku na mchana! Baada ya watawala wa Misri kuongoza msafara huu wa unyonge na udhalili, walifuatiwa na Mamlaka ya Palestina (PLO) na watawala wa Jordan, kisha Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco. Watawala wa Saudia wamesimama njiani wakiashiria nchi hizo kuwa wapo nyuma yao na hawataachwa nyuma... Hivyo, wote wanafanya haraka katika jinai hiyo bila kujali udhalili unaowafunika kuanzia utosini hadi nyayo zao:
سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ
"Watafikwa wale waliofanya uhalifu na unyonge mbele ya Allah na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya." (QS. Al-An'am [6]: 124)
Kisha si Palestina pekee iliyochomwa kisu na watawala hawa, bali pia walisalimu amri au kusalimisha maeneo mengine matukufu ya ardhi ya Uislamu. Kashmir ilichukuliwa na washirikina wa Kihindu... Urusi ikachukua Crimea... Kusini mwa Sudan kukatenganishwa na Kaskazini yake... Timor Mashariki ikanyakuliwa kutoka Indonesia... Na Cyprus, na nini kitakujulisha nini hiyo Cyprus, ngome ya Waislamu kwa miaka mingi, leo sehemu yake kubwa inatawaliwa na Ugiriki... Na Waislamu wa Rohingya wanachinjwa huko Myanmar (Burma), na wanapokimbilia Bangladesh, serikali huko inawadhiki na kuwafungia katika kisiwa cha "Bhasan Char," ambacho ni kisiwa hatari kinachokumbwa na mafuriko na hakifai kwa makazi ya binadamu! Kisha Turkestan Mashariki, ambapo China imeanza kuwakandamiza na kuwafanyia unyama ambao hata wanyama huuepuka, ikageuza eneo hilo kuwa gereza kwa wanaume mashujaa na wanawake watukufu. Mauaji makubwa yanafanyika waziwazi mbele ya macho na masikio ya nchi zilizopo katika ardhi za Waislamu, nazo zimenyamaza kimya kama makaburi, na zinapozungumza kuhusu unyama wa China kwa Waislamu, husema kuwa hiyo ni suala la ndani!
كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً
"Ni neno kubwa litokalo vinywani mwao; hawasemi ila uongo." (QS. Al-Kahf [18]: 5)
Ama nchi nyingine za Waislamu, zinatawaliwa na viongozi Ruwaybidhah (viongozi duni) wanaozunguka na makafiri wakoloni popote wanapozunguka. Hawalindi usalama wa nchi wala hawajali haki za waja. Utajiri wao unaporwa na heshima yao inadhulumiwa. Hawana thamani yoyote mbele ya makafiri wakoloni, hasa Marekani. Badala yake, Marekani inawaita vibaraka wake kwa namna inayozidi kuwadhalilisha na kuwafanyia unyonge, ikiwaambia: "Kama si sisi, msingebaki kwenye viti vyenu vilivyopinda kwa siku chache, basi tuliyeni mali muwezavyo, bali hata zaidi ya mnavyoweza." Na hakika, yule anayedhalilika, basi udhalili unakuwa rahisi kwake!
Enyi Waislamu: Hali yenu iko hivi baada ya kutoweka kwa Khilafah, ambapo mataifa yamekushambulieni kutoka kila upande. Je, mlikuwaje mlipokuwa mkifunikwa na kivuli cha Khilafah?
Mlikuwa Umma bora uliotolewa kwa watu, wafuasi wa Muhammad ﷺ, hitimisho la Manabii na imamu wa wapiganaji Jihad... babu zenu walikuwa Makhalifa Waongofu na viongozi washindi... ninyi ni wajukuu wa mshindi Salahuddin, aliyewashinda Wanamsalaba na kuikomboa Baitul Maqdis kutoka katika uchafu wao katika mwezi kama huu mtukufu wa Rajab 583 H... wajukuu wa Qutuz na Baibars, washindi wa Watatari... wajukuu wa Muhammad al-Fatih, kiongozi kijana ambaye hakuzidi umri wa miaka ishirini na mitatu alipoiteka Constantinople mwaka 857 H - 1453 M, na Allah akamtukuza kwa sifa za Mtume ﷺ katika hadith aliyoitoa Ahmad kutoka kwa Bishr al-Khath'ami:
فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ
"Basi ni kiongozi mbora kiongozi wake, na ni jeshi mbora jeshi lile."
Wajukuu wa Khalifa Suleiman al-Qanuni, ambaye Ufaransa iliomba msaada kwake katika karne ya kumi na sita (1525 M) ili kumwachilia mfalme wake aliyekuwa mateka. Lakini leo imesahau au imejisahaulisha kuomba msaada kwake kwa Khalifa wa Waislamu, ikauchokoza Uislamu na Mtume wa Uislamu ﷺ bila ya mlinzi au wa kumuwajibisha kwa sababu ngao ya Uislamu imetoweka... wajukuu wa Khalifa Selim III, ambaye katika zama zake Marekani ililipa kodi ya kila mwaka ili kuruhusu meli za Kimarekani kupita salama kutoka Bahari ya Atlantiki kuelekea Bahari ya Mediterania bila kushambuliwa na jeshi la majini la Kiothmania katika jimbo la Algeria. Na kwa mara ya kwanza Marekani ililazimika kusaini mkataba kwa lugha isiyo yake, bali kwa lugha ya dola nyingine (Dola ya Kiothmania) mwaka 1210 H - 1795 M. Na sasa Marekani inawatawala viongozi wa Waislamu ikisema "lipa, kwani sisi ndio tunaokulinda"... wajukuu wa Khalifa Abdul Hamid, ambaye hakuhadaika na mamilioni ya dhahabu yaliyotolewa na Mayahudi kwa ajili ya hazina ya dola ili kuwaruhusu kufanya makazi Palestina, akasema kauli yake maarufu: (Hakika kufanya upasuaji katika mwili wangu ni rahisi kwangu kuliko kuona Palestina ikikatwa kutoka katika Dola ya Khilafah), kisha akaongeza: (...basi Mayahudi na wabakie na mamilioni yao... na ikiwa Dola ya Khilafah itasambaratika siku moja, basi wakati huo wataweza kuichukua Palestina bila malipo). Na hivi ndivyo ilivyotokea!... wajukuu wa wale waliogundua saa na kumpa zawadi Charlemagne, mfalme mkuu wa Ulaya wakati huo, na wasaidizi wake, ambao walikuwa watu mashuhuri kwake, wakadhani kuwa imejaa majini na mashetani! Hivyo ndivyo tulivyokuwa katika fikra zetu angavu na zilizoangaza, na hivyo ndivyo walivyokuwa katika fikra zao tupu na mbovu!
Hivyo ndivyo mlikivyokuwa enyi Waislamu wakati Khilafah ilipokuwa inawafunika, na hivyo ndivyo mlivyokuwa wakati Khilafah ilipoondoka kwenye vipaji vya nyuso zenu. Basi zingatieni, enyi wenye macho...
Na mwisho, naelekea kwenu enyi watu wa nguvu na ulinzi (Ahl al-Quwwah wal-Man'ah)... Enyi wajukuu wa Khalid, Salahuddin na Muhammad al-Fatih...
Ninyi tu ndio mnaoweza kuponya vifua vya Umma kutokana na maadui zake, maadui wa dini yenu. Ninyi tu ndio mnaoweza kuvunja udhalili uliowafika Waislamu katika nchi zao, nchi za Kiislamu... na mtakuwa na heshima ya kuanza na kutimiza matumaini ya Umma, bali Umma wote utawafuata, na majeshi yake yote yatakuwa mbele yenu na nyuma yenu. Hamtakuwa peke yenu kwa idhini ya Allah Ta'ala. Basi simameni kutekeleza wajibu wenu, Allah awabariki, simameni kutunusuru sisi, kunusuru Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashidah. Kwani hiyo si njia ya ushindi tu kwa mtazamo wa kuelezea uhalisia, bali kwa sababu ni faradhi kubwa kwanza kabisa. Kwani kwayo hukumu zinasimamishwa, na mipaka (hudud) inatekelezwa, na bila hiyo hukumu hazitekelezwi kwa watu wala mipaka haiswihi baina yao... Na yule ambaye hafanyi kazi ya kusimamisha Khilafah na kumpata Khalifa hali ya kuwa ana uwezo, basi dhambi yake ni kubwa, ni kana kwamba amekufa kifo cha kijahilia kuashiria uzito wa dhambi hiyo:
وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً
"...na yule atakayekufa na huku shingoni mwake hamna baia (kiapo cha utii), hufa kifo cha kijahilia." (Muslim)
Na Waislamu walianza na kutoa baia kwa Khalifa kabla hawajajishughulisha na maandalizi ya (mazishi ya) Mtume wa Allah ﷺ na kumzika, pamoja na umuhimu na ukubwa wa jambo hilo. Yote hayo ni kwa ajili ya ukubwa wa Khilafah na umuhimu wake...
Enyi watu wa nguvu na ulinzi... Enyi watu wa nusra... Enyi majeshi ya Waislamu
Je, miongoni mwenu hayupo Mus’ab bin Umair, As’ad bin Zurarah, Usaid bin Hudhair, na Sa’ad bin Muadh ambao walimnusuru Allah (swt) na Mtume Wake ﷺ wakafuzu duniani na Akhera? Hata Kiti cha Enzi (Arshi) cha Allah kilitikisika kwa kifo cha Sa’ad bin Muadh kwa sababu ya kuinusuru dini ya Allah. Al-Bukhari ametoa kutoka kwa Jabir (ra): Nilimsikia Mtume ﷺ akisema:
اهْتَزَّ العَرْشُ لِمَوت سعد بن معاذ
"Kiti cha Enzi (Arshi) kilitikisika kwa kifo cha Sa’ad bin Muadh."
Je, hayupo miongoni mwenu mtu muongofu atakayemnusuru Allah, Mtume Wake, na wabeba da’wah Yake? Hakika Umma unawasubiri ninyi, unasubiri kutoka kwenu mpige Takbir nao wapige Takbir pamoja nanyi, na bendera ipepee mikononi mwenu nao wawalengee tahlili. Na kwa hili pekee Umma utanyanyuka, na kusimamisha Khilafah Rashidah itakayotekeleza Uislamu ndani na kuubeba kwa ulimwengu kwa da’wah na Jihad, na Allah (swt) ataunusuru:
إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ
"Hakika Sisi bila shaka tutawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na siku watakaposimama mashahidi." (QS. Ghafir [40]: 51)
Enyi askari wa Allah: Hakika tunatambua kuwa malaika hawatashuka kutoka mbinguni kutusimamishia Khilafah na kutuongozea jeshi litakalotukuza Uislamu na Waislamu. Bali Allah (swt) anateremsha malaika wa kutusaidia ikiwa tutafanya kazi kwa juhudi, ukweli na ikhlasi kwa ajili ya kuanza tena maisha ya Kiislamu ardhini na kusimamisha Khilafah. Nayo ni ahadi isiyo na shaka katika Kitabu cha Allah (swt) na Hadith ya Mtume wa Allah ﷺ. Na wala isiathiriwe na kauli za wasemaji kuwa kusimamisha Khilafah leo ni aina ya ndoto/khayali; bali ukweli ni kwamba msemaji anayesema kuwa kusimamisha Khilafah ni ndoto ndiye anayekimbilia ndoto. Ama kusimamisha Khilafah ni ukweli ambao lazima utokee kwa idhini ya Allah, ukithibitishwa na mambo manne ya kweli:
Kwanza: Ahadi kutoka kwa Allah:
وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ
"Allah Amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, kwamba kwa yakini Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao." (QS. An-Nur [24]: 55)
Pili: Habari njema kutoka kwa Mtume wa Allah ﷺ kuhusu kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala huu wa mabavu (mulkan jabriyyatan). Anasema ﷺ:
...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ
"...kisha utakuwepo utawala wa mabavu, na utakuwepo kwa muda anaotaka Allah uwepo, kisha Atauondoa Atakapotaka Auondoe, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume." Kisha akanyamaza ﷺ. (Ahmad kutoka kwa Hudhaifah)
Tatu: Umma ulio hai, wenye kutenda, umma bora uliotolewa kwa watu:
كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ
"Mlikuwa Umma bora uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Allah." (QS. Ali 'Imran [3]: 110). Basi hata kama umetulia kutokana na kusimamisha Khilafah kwa siku moja, basi huo ni utulivu wa simba kabla ya mshindo...
Nne: Chama ambacho kwa idhini ya Allah ni chenye ikhlasi kwa ajili Yake (swt), mkweli kwa Mtume Wake ﷺ, kinachoharakisha hatua, kikiunganisha usiku wake na mchana wake ili kutimiza ahadi na habari njema. Ni kana kwamba ni ushahidi wa kauli yake ﷺ:
لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ عَلَى الْحَقِّ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ كَذَلِكَ
"Haitaacha kubakia kundi katika Umma wangu likiwa juu ya haki, hawadhuriki na yule anayewatelekeza mpaka amri ya Allah ije nao wapo hivyo hivyo." (Muslim kutoka kwa Thauban)
Hakika lolote miongoni mwa haya manne linatosha kusema kuwa kazi ya Khilafah si khayali, vipi basi yakiwa yamejumuika yote manne?! Na hivyo ndivyo kusimamishwa kwa Khilafah kulivyo ukweli unaotokea katika wakati usio mbali kwa idhini ya Allah. Na kwamba uthabiti wake na utulivu wake baada ya kusimama kwake ni jambo lenye kuhakikika inshaAllah. Na kwamba majengo ya madola ambayo ni makubwa leo yatasambaratika na madola hayo mahali pa mbali sana. Madola haya ni duni mbele ya Allah na mbele ya waja wa Allah. Na kile ambacho kiumbe kidogo (COVID-19) kilichokuwa hakionekani kimeyafanyia madola hayo na kiongozi wao Marekani kinasema hayo... Na tazameni kile kilichoyapata katika chaguzi zake, upande mmoja unauona kuwa ni wizi na udanganyifu na mwingine unauona kuwa ni ushindi mkubwa! Kisha haikuishia kwenye makombora ya maneno, bali hadi kuvamia taasisi rasmi, na kupoteza roho kwa makombora halisi katika korido za kiongozi wa mfumo wa kirasilimali, na pande zote mbili zinapigania demokrasia iliyoharibika! Huu ndio ulimwengu leo, mkubwa wake kabla ya mdogo wake... Na hautaokolewa isipokuwa kwa kusimamisha Dola ya Uislamu, Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume...
Enyi Ndugu: Hakika tulikuwa tukifanya kazi na kumuomba Allah kusimamishwa kwa Khilafah kuwe kabla ya kumbukumbu ya miaka mia moja. Siku zilikuwa zikipita juu yetu katika kipindi hiki cha miaka sabini ya umri wa Hizb, karibu tunaishika Khilafah kisha inakuwa mbali. Pamoja na hayo, hatukati tamaa na rehema ya Allah. Sisi tunafanya kazi na macho yetu yanatazamia Khilafah, na nyoyo zetu zinadunda kwa ajili yake. Sote tuna utulivu wa kusimama kwake kwani Mtume wa Allah ﷺ alituhubiria hilo na kutupa habari njema:
...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ
"...kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume."
Na yote haya yanafaa kwa ajili ya kuimarisha ari, kuimarisha maazimio, na kuwasha moto upya, na kumfanya mtu kuwa kiumbe kingine; kutoka kwa mwenye kuzimia pindi msiba unapompata hadi kwenye mwenye bishara ya faraja kwa kutokea kwa msiba huo.
Hivyo ndivyo alivyotuhubiria Mjuzi Mwenye Habari:
فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً * إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً
"Basi hakika pamoja na dhiki kuna faraja. Hakika pamoja na dhiki kuna faraja." (QS. Ash-Sharh [94]: 5-6). Na hivyo ndivyo alivyotuhubiria mkweli mwenye kusadikiwa katika hadith madhubuti: "Na kamwe uzito mmoja hautashinda faraja mbili." Na hivyo ndivyo barua ya Umar kwenda kwa Abu Ubaidah ilivyosema: (Kwani hakuna uzito wowote isipokuwa Allah Aujaalia baada yake njia ya kutokea, na kamwe uzito mmoja hautashinda faraja mbili). Basi faraja inakuja kwa idhini ya Allah Mola wa walimwengu, na Khilafah itasimama kwa mikono ya Waumini wa kweli, italingamiza umbo la Kiyahudi na Palestina itarejea katika nyumba ya Uislamu (Dar al-Islam). Na Roma itafunguliwa baada ya dada yake (Constantinople) kufunguliwa. Na sauti tukufu zitapaza sauti kwa neno la Mwenye Nguvu na Mtukufu:
وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وزهق الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً
"Na sema: Kweli imefika na uongo umetoweka; hakika uongo lazima utoweke." (QS. Al-Isra [17]: 81). Na dunia itajaa sauti za Takbir, na ardhi itang’ara kwa nuru ya Uislamu:
لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزّاً يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلّاً يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ
"Hakika jambo hili (Uislamu) litafika kote kule kofikapo usiku na mchana, na Allah hataacha nyumba ya udongo wala ya mahema (ngozi) isipokuwa ataiingiza dini hii ndani yake, kwa utukufu wa mtukufu au unyonge wa mnyonge; utukufu ambao Allah Atautukuza Uislamu kwayo, na unyonge ambao Allah Ataukosesha nguvu ukafiri kwayo." (Ahmad kutoka kwa Tamim ad-Dari)
Hakika tunatambua kuwa maadui wa Uislamu wataona kuwa kufikiwa kwa hilo ni jambo lisilowezekana, na watakariri kauli ya wenzao wa zamani kwa kejeli:
غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ
"Dini yao imewahadaa hawa." (QS. Al-Anfal [8]: 49). Lakini kama vile kauli hiyo ilivyokuwa maangamizi kwa wasemaji wake, na Allah Akaitukuza dini Yake na kuwanusuru watu wake, basi vilevile leo itakuwa maangamizi kwao. Kwani Allah Mwenye Nguvu na Mwenye Hekima yupo pamoja na waja Wake wanaomtegemea, wenye ikhlasi kwa ajili Yake (swt), wakweli kwa Mtume Wake ﷺ, wanaofanya kazi kwa juhudi na bidii, bila nyoyo zao na viungo vyao kuachana na kauli Yake Ta’ala:
إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً
"Hakika Allah Atatimiza amri Yake; Allah Kweli Amekwishajaalia kila kitu na kipimo chake." (QS. At-Talaq [65]: 3). Hawa, kwa kila siku inayopita, wanakaribia "kipimo" hiki:
وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
"Na Allah ndiye Mwenye kushinda katika jambo Lake, lakini watu wengi hawajui." (QS. Yusuf [12]: 21)
Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Jumamosi, 29 Rajab 1442 H Ndugu yenu Sawa na 13 Machi 2021 M Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amir wa Hizb ut Tahrir