Home About Articles Ask the Sheikh
Uchambuzi

Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mtukufu Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah Katika Maadhimisho ya Miaka Mia Moja Tangu Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah Mwaka 1342 H - 1924 M

March 13, 2021
74

Alhamdu Lillahi was-Salaatu was-Salaamu 'alaa Rasoolillahi wa 'alaa Aalihi wa Sahbihi wa man waalaahu, wa ba'du...

Kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla, na kwa wabeba da’wah wa kurejesha Khilafah Rashidah mahususi, vijana wa kiume na kike...

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Katika siku kama hizi miaka mia moja iliyopita, mwishoni mwa Rajab 1342 H, sawia na mwanzoni mwa Machi 1924 M, makafiri wakoloni wakiongozwa na Uingereza wakati huo, kwa ushirikiano na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, walifanikiwa kuivunja Dola ya Khilafah. Mhalifu wa karne hiyo, Mustafa Kemal, alitangaza kufutwa kwa Khilafah, kumzingira Khalifah kule Istanbul na kumfukuza alfajiri ya siku hiyo. Hiyo ilikuwa ni gharama ambayo Uingereza ilimwamuru ailipe ili amikishwe kuwa rais dhaifu wa Jamhuri ya Uturuki ya kisekular. Hivyo ndivyo ilivyotokea, ambapo mtetemeko mkubwa ulitokea katika nchi za Waislamu kwa kuvunjwa kwa Khilafah – chemchemi ya utukufu wao na njia ya kupata radhi za Mola wao.

Mhalifu huyo alitangaza kufanya kufuru ya wazi kwa kuifuta Khilafah baada ya kuwepo kwake. Ilikuwa ni wajibu kwa Umma kumpiga kwa upanga kama ilivyokuja katika Hadith ya Mtume ﷺ iliyopokelewa na ‘Ubadah bin as-Samit (ra):

وَأَنْ لَا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أَهْلَهُ إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِنْدَكُمْ مِنْ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ

“...na kwamba tusizozane na wenye mamlaka juu ya jambo hilo (uongozi), isipokuwa mkieona kufuru ya wazi ambayo mna ushahidi kwayo kutoka kwa Allah.” (Muttafaqun ‘alayhi)

Hata hivyo, ukandamizaji wake mkali uliomwaga damu za Umma, hasa wanachuoni – ambapo aliwanyonga wengi, akiwemo Sheikh Said Piran (rehema za Allah ziwe juu yake), na kuwafunga wengine – yote hayo yalikuwa na athari katika kuufanya Umma ushindwe kutekeleza wajibu wake. Hivyo, haukuweza kumsambaratisha mhalifu huyo na wasaidizi wake ili wawe wenye kushindwa. Badala yake, jibu lilikuwa dhaifu ambalo halikufikia kiwango cha kumpondaponda msaliti huyo wa Allah, Mtume Wake, na Waumini! Hivyo ndivyo mtendaji huyo wa kufuru ya wazi “alivyookoka” na kitendo chake kiovu bila ya Umma kumtumbukiza kwenye shimo la uharibifu!

Baada ya hapo, ushawishi wa makafiri wakoloni ulienea katika nchi za Waislamu. Walizigawa nchi hizo na kuzisambaratisha katika vipande vipande vilivyofikia karibu hamsini na tano, kama matokeo ya mtetemeko wa kuvunjwa kwa Khilafah. Kisha, waliongeza mtetemeko mwingine juu ya mtetemeko huo kwa kuwapa Mayahudi dola katika Ardhi Iliyobarikiwa, mahali pa safari ya usiku ya Mtume ﷺ (Israa) na kupaa kwake mbinguni (Mi’raaj), na kuwapa njia zote za kuendelea kuwepo. Njia ya kwanza kabisa kati ya hizo ilikuwa ni kulinda usalama wa dola hiyo kupitia watawala vibaraka wanaoizunguka. Si hivyo tu, bali watawala hawa walikuwa wakishindwa mbele ya Mayahudi katika kila vita vilivyozuka hadi wakaipa dola ya Kiyahudi ukubwa zaidi ya ilivyo na taswira isiyo ya kweli.

Hawakuishia hapo, bali walifanya kila juhudi kumpiga vita Allah na Mtume Wake ili kuhamisha kadhia hiyo kutoka kwenye kuung’oa upandikizaji wa Kiyahudi katika Palestina hadi kwenye mazungumzo na upandikizaji huo ili labda ujitoe katika sehemu ya ardhi iliyoikalia mwaka 1967! Kisha walishuka viwango zaidi baada ya hapo na kukimbilia katika kuanzisha uhusiano wa kawaida (normalization) na dola ya Kiyahudi hata bila ya hiyo kujiondoa kwenye sehemu yoyote!! Baadhi yao walifanya jinai ya kuanzisha uhusiano huo kwa siri, na wengine wakafanya waziwazi usiku na mchana! Baada ya watawala wa Misri kuongoza mkondo huu wa udhalili na unyonge, walifuatiwa na Mamlaka ya Palestina na watawala wa Jordan, kisha Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco. Watawala wa Saudia nao wamesimama njiani wakiashiria nchi hizo kuwa wapo nyuma yao na hawatachelewa kufuata msafara huo... Hivyo, wote wanafanya haraka katika jinai hiyo bila ya kujali udhalili unaowazunguka kuanzia utosini mwao hadi nyayoni mwao.

سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ

“Itawafika wale waliofanya jinai udhalili mbele ya Allah na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.” (Al-An'am [6]: 124)

Kisha si Palestina pekee ndiyo waliyoichoma kisu watawala hawa, bali pia walisalimisha maeneo mengine matukufu ya ardhi ya Uislamu. Kashmir ilinyakuliwa na washirikina wa Kihindu na kuunganishwa na dola yao... Urusi iliichukua Crimea... Kusini mwa Sudan ilitenganishwa na Kaskazini yake... Timor Mashariki ilichukuliwa kutoka Indonesia... Na Cyprus, na nini kitakujulisha nini hiyo Cyprus? Ngome ya Waislamu kwa miaka mingi, leo hii sehemu yake kubwa inadhibitiwa na Wayunani... Waislamu wa Rohingya wanachinjwa nchini Myanmar (Burma), na wanapokimbilia Bangladesh, utawala unawabana na kuwafungia katika kisiwa cha Bhasan Char, ambacho ni kisiwa hatari kinachokumbwa na mafuriko na hakifai kwa makazi ya binadamu! Kisha Turkestan Mashariki ambayo Uchina imeanza kuishambulia na kuifanyia vitendo vya kinyama, kiasi kwamba hata wanyama wakali wanaona haya; imeigeuza kuwa gereza la wanaume na wanawake huru. Mauaji makubwa yanafanyika waziwazi mbele ya macho na masikio ya nchi zilizopo katika ardhi za Waislamu, ambazo zimenyamaza kimya kama makaburi, na zinapozungumza, zinasema kuhusu ukatili wa Uchina kwa Waislamu kuwa ni "suala la ndani"!

كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً

“Ni neno kubwa litokalo vinywani mwao, hawasemi ila uongo.” (Al-Kahf [18]: 5)

Ama nchi nyingine za Waislamu zinatawaliwa na viongozi wapuuzi (ruwaibidhah) wanaozunguka na makafiri wakoloni popote wanapoelekea. Hawalindi usalama wa nchi wala hawachungi haki za waja. Utajiri wao unaporwa na heshima yao inachukuliwa. Hawana thamani yoyote mbele ya makafiri wakoloni, hasa Marekani, bali Marekani inawaita vibaraka wake kwa namna inayozidisha udhalili na unyonge, ikiwaambia: "Bila sisi, msingebaki kwenye viti vyenu vilivyopinda kwa siku chache, basi tulipeeni fedha kadiri mwezavyo, hata zaidi ya mwezavyo." Na hakika, anayekubali kudhalilika, udhalili unakuwa rahisi kwake!!

Enyi Waislamu: Hii ndiyo hali yenu baada ya kuondoka kwa Khilafah, ambapo mataifa yamekuvamieni kutoka kila upande. Lakini mlikuwa vipi mlipokuwa chini ya kivuli cha Khilafah?

Mlikuwa Umma bora uliotolewa kwa watu, wafuasi wa Muhammad ﷺ, hitimisho la Manabii na imamu wa Mujahidina... Babu zenu walikuwa Makhalifa Waongofu na viongozi washindi... Nyinyi ni wajukuu wa mshindi Salahuddin, aliyewashinda Wanamsalaba na kuikomboa Baitul Maqdis kutoka kwenye uchafu wao katika mwezi kama huu mtukufu wa Rajab mwaka 583 H... Wajukuu wa Qutuz na Baibars, washindi wa Watatar... Wajukuu wa Muhammad al-Fatih, amiri kijana ambaye hakuzidi umri wa miaka ishirini na tatu alipoiteka Constantinople mwaka 857 H - 1453 M, na Allah akamsherehesha kwa sifa za Mtume ﷺ katika Hadith iliyopokelewa na Ahmad kutoka kwa Bishr al-Khath’ami:

فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ

“Hakika amiri (kiongozi) bora ni amiri wake, na jeshi bora ni jeshi hilo.” (HR Ahmad)

...Wajukuu wa Khalifah Suleiman al-Qanuni, ambaye Ufaransa iliomba msaada wake katika karne ya kumi na sita (1525 M) ili kumwachilia mfalme wake aliyekuwa mateka, lakini leo hii imesahau au imejisahaulisha ombi lake la msaada kwa Khalifah wa Waislamu, na imeanza kuufanyia kejeli Uislamu na Mtume wa Uislamu ﷺ bila ya kuwepo mwangalizi au wa kuiwajibisha kwa sababu ngao ya Uislamu imeondoka... Wajukuu wa Khalifah Selim III, ambaye katika zama zake Marekani ililipa kodi ya kila mwaka ili kuruhusu meli za Kimarekani kupita salama kutoka Bahari ya Atlantiki kuelekea Bahari ya Mediterania bila kushambuliwa na jeshi la majini la Kiothmania katika mkoa wa Algeria. Na kwa mara ya kwanza, Marekani ililazimika kutia saini mkataba kwa lugha nyingine isiyo yake, bali kwa lugha ya dola nyingine (Dola ya Kiothmania) mwaka 1210 H - 1795 M, na sasa Marekani inawadhibiti watawala wa Kiislamu ikiwaambia: "Lipeni, kwani sisi ndio tunaowalinda"... Wajukuu wa Khalifah Abdul Hamid ambaye hakuhadaika na mamilioni ya dhahabu yaliyotolewa na Mayahudi kwa hazina ya dola ili kuwaruhusu kuishi Palestina, na akasema kauli yake maarufu: (Kukatwa kwa kisu mwilini mwangu ni rahisi kwangu kuliko kuona Palestina ikikatwa kutoka kwenye Dola ya Khilafah), kisha akaongeza (...basi Mayahudi na wabaki na mamilioni yao... na kama Dola ya Khilafah itasambaratika siku moja, basi wakati huo wataweza kuichukua Palestina bila gharama yoyote). Na hili ndilo lililotokea!... Wajukuu wa wale waliovumbua saa na kumpa zawadi moja mfalme Charlemagne, mfalme mkuu zaidi wa Ulaya wakati huo, na wasaidizi wake, ambao walikuwa wasomi wakubwa kwake, wakadhani kuwa imejaa majini na mashetani! Hivyo ndivyo tulivyokuwa katika fikra zetu zenye kuelimika, na hivyo ndivyo walivyokuwa katika fikra zao tupu na mgonjwa!

Hivyo ndivyo mlivyokuwa enyi Waislamu wakati Khilafah ilipokuwa inawafunika, na hivyo ndivyo mlivyokuwa wakati Khilafah ilipoondoka kwenu. Basi chukueni zingatio enyi wenye kuona...

Na mwisho, naelekea kwenu enyi watu wenye nguvu na kinga (Ahlul Quwwah wal Man’ah)... Enyi wajukuu wa Khalid, Salahuddin, na Muhammad al-Fatih...

Nyinyi pekee ndio mnaoweza kuponya nyoyo za Umma kutokana na maadui wake – maadui wa dini yenu. Nyinyi pekee ndio mnaoweza kuvunja udhalili uliowafikia Waislamu katika nchi zao, ardhi za Uislamu... Na mtapata heshima ya kuanza na kutimiza matumaini ya Umma, na hakika Umma wote utawafuata, na majeshi yake yote yatakuwa mbele yenu na nyuma yenu. Hamtakuwa peke yenu kwa idhini ya Allah Ta’ala. Basi simameni kutekeleza wajibu wenu, Allah awabariki. Simameni kutunusuru, kunusuru Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashidah. Hii si njia ya ushindi tu kwa mujibu wa uhalisia, bali kwanza kabisa ni faradhi kuu. Kwani kwayo sheria zinasimamishwa, na mipaka (hudud) inatekelezwa, na bila hiyo sheria hazitekelezwi kwa watu wala mipaka haisambazwi miongoni mwao... Na yule asiyefanya kazi ya kusimamisha Khilafah na kumpata Khalifah ilhali ana uwezo, basi dhambi yake ni kubwa kana kwamba amekufa kifo cha kijahiliya kuonesha ukubwa wa dhambi hiyo:

وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً

“...na yule atakayekufa na hana kiapo cha utiifu (bay'ah) shingoni mwake, basi amekufa kifo cha kijahiliya.” (HR Muslim)

Na Waislamu walishughulika na kutoa bay'ah kwa Khalifah kabla ya kuanza kumwandaa Mtume wa Allah ﷺ na kumzika, pamoja na umuhimu na utukufu wa jambo hilo. Yote hayo ni kwa sababu ya utukufu wa Khilafah na umuhimu wake...

Enyi watu wenye nguvu na kinga... Enyi watu wa nusra... Enyi majeshi ya Waislamu

Je, miongoni mwenu hamna Mus’ab bin ‘Umair, As’ad bin Zurarah, Usayd bin Hudayr, na Sa’d bin Mu’adh ambao walimnusuru Allah (swt) na Mtume Wake ﷺ wakafaulu duniani na Akhera? Hata Kiti cha Enzi cha Mwingi wa Rehema (Arsh) kilitikisika kwa kifo cha Sa’d bin Mu’adh kwa sababu ya kuinusuru dini ya Allah. Al-Bukhari amepokea kutoka kwa Jabir (ra), nilimsikia Mtume ﷺ akisema:

اهْتَزَّ العَرْشُ لِمَوت سعد بن معاذ

“Kiti cha Enzi kilitikisika kwa kifo cha Sa’d bin Mu’adh.” (HR Bukhari)

Je, miongoni mwenu hamna mtu muadilifu atakayenusuru Allah, Mtume Wake na watu wa da’wah Yake? Hakika Umma unawasubiri, unasubiri kutoka kwenu mpige takbira nao wapige takbira pamoja nanyi, na bendera ipepee mikononi mwenu nao washahadie kwenu. Na kwa hili pekee, Umma utainuka na kusimamisha Khilafah Rashidah itakayotekeleza Uislamu ndani na kuubeba kwa ulimwengu kwa da’wah na jihadi, na Allah (swt) ataunusuru:

إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ

“Hakika Sisi tunawanusuru Mitume Wetu na wale walioamini katika maisha ya duniani na siku wataposimama mashahidi.” (Ghafir [40]: 51)

Enyi askari wa Allah: Tunatambua kuwa hakutashuka malaika kutoka mbinguni kutusimamishia Khilafah na kutuongozea jeshi litakaloupa utukufu Uislamu na Waislamu, bali Allah (swt) atashusha malaika wa kutusaidia ikiwa tutafanya kazi kwa bidii, ukweli na ikhlasi ili kurejesha maisha ya Kiislamu duniani na kusimamisha Khilafah. Hiyo ni ahadi isiyo na shaka katika Kitabu cha Allah (swt) na Hadith ya Mtume Wake ﷺ. Na kauli ya wanaosema kuwa kusimamisha Khilafah leo ni ndoto ya mchana haina athari yoyote; ukweli ni kwamba anayesema kusimamisha Khilafah ni ndoto, yeye ndiye anayefuata ndoto. Ama kusimamisha Khilafah ni ukweli ambao lazima utokee kwa idhini ya Allah, ukithibitishwa na mambo manne ya kweli:

Kwanza: Ahadi kutoka kwa Allah:

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ

“Allah amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuwa kabla yao.” (An-Nur [24]: 55)

Pili: Bishara kutoka kwa Mtume wa Allah ﷺ ya kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala huu wa mabavu. Mtume ﷺ anasema:

...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ

“...kisha utakuwepo utawala wa mabavu, na utakuwepo kwa muda anaotaka Allah uwepo, kisha Allah atauondoa anapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha akanyamaza ﷺ. (HR Ahmad kutoka kwa Hudhayfah)

Tatu: Umma ulio hai na wenye nguvu, Umma bora uliotolewa kwa watu:

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ

“Nyinyi mmekuwa Umma bora uliotolewa kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Allah.” (Aali ‘Imran [3]: 110). Hivyo basi, hata kama Umma umetulia kusimamisha Khilafah kwa siku moja, huo si chochote ila ni utulivu wa simba kabla ya kushambulia...

Nne: Chama ambacho kwa idhini ya Allah kina ikhlasi Kwake (swt), ni mkweli kwa Mtume Wake ﷺ, kinakwenda kwa kasi, kikiunganisha usiku wake na mchana wake ili kutimiza ahadi na bishara hiyo. Na ni kana kwamba chama hicho ni uthibitisho wa kauli ya Mtume ﷺ:

لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ عَلَى الْحَقِّ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ كَذَلِكَ

“Halitaacha kundi miongoni mwa Umma wangu kuwa dhahiri juu ya haki, hawadhuriki na wanaowaacha mkono mpaka amri ya Allah ije na wao wapo hivyo hivyo.” (HR Muslim kutoka kwa Thawban)

Hakika lolote kati ya haya manne linatosha kusema kuwa kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah si ndoto, sembuse yakiungana yote manne?! Hivyo basi, kusimamishwa kwa Khilafah ni ukweli utakaotokea katika wakati usio mbali kwa idhini ya Allah. Na kwamba uthabiti na utulivu wake baada ya kusimamishwa ni jambo lililohakikishwa In Shaa Allah. Na kwamba majengo ya madola ambayo ni makubwa leo yatasambaratika hadi kwenye shimo la uharibifu. Madola haya ni duni mbele ya Allah na mbele ya waja wa Allah. Na kile ambacho kiumbe mdogo (COVID-19) asiyeonekana alichofanya kwa madola hayo na kiongozi wao Marekani ni ushahidi wa hilo... Angalieni nini kiliwapata katika uchaguzi wao: upande mmoja unauona ni wizi na udanganyifu, na mwingine unauona ni ushindi mkubwa! Kisha haikuishia kwenye makombora ya maneno tu, bali hadi kuvamia taasisi rasmi, na kupoteza maisha kwa makombora ya vitendo katika korido za kiongozi wa mfumo wa kirasimali, na pande zote mbili zinapigia debe demokrasia iliyochakaa! Huyu ndiye ulimwengu wa leo, mkubwa wake kabla ya mdogo wake... Na hutaokoka ila kwa kusimamisha Dola ya Kiislamu, Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume...

Enyi Ndugu: Tulikuwa tunafanya kazi na kumnyenyekea Allah ili kusimamishwa kwa Khilafah kuwe kabla ya maadhimisho ya miaka mia moja. Siku zilikuwa zinatupita katika miaka hii sabini ya umri wa Hizb, karibu tunaishika Khilafah kisha inakaa mbali kidogo. Pamoja na hayo, hatukati tamaa na rehema za Allah. Sisi tunafanya kazi na macho yetu yanatazamia Khilafah, na nyoyo zetu zinadunda kuelekea kwayo, na sote tuna uhakika na kusimamishwa kwake kwani Mtume wa Allah ﷺ alituhabarisha hilo na kutubashiria:

...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ

“...kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Na haya yote yanastahiki kuamsha ari, kuimarisha azma, kuwasha moto wa juhudi upya, na kumfanya mtu kuwa kiumbe mwingine; kutoka kwa aliyekuwa amezimia msiba unapompata, hadi kwa anayefurahi kwa kutarajia faraja msiba unapotokea.

Hivyo ndivyo alivyotuhabarisha Mwenye Kujua, Mwenye Habari:

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً * إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْراً

“Basi kwa hakika pamoja na uzito kuna wepesi. Hakika pamoja na uzito kuna wepesi.” (Ash-Sharh [94]: 5-6)

Na hivyo ndivyo alivyotuhabarisha mkweli mwenye kusadikiwa katika Hadith ya Razin:

وَلَنْ يَغْلِبَ عُسْرٌ يُسْرَيْنِ

“Na uzito mmoja hautashinda wepesi miwili.”

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa barua ya Umar kwenda kwa Abu Ubaidah: (Kwani hakuna uzito wowote isipokuwa Allah hujaalia faraja baada yake, na uzito mmoja hautashinda wepesi miwili). Basi faraja inakuja kwa idhini ya Allah Mola wa walimwengu, na Khilafah inasimama kwa mikono ya Waumini wa kweli. Itatokomeza upandikizaji wa Kiyahudi na Palestina itarejea katika Nyumba ya Uislamu (Dar al-Islam), na Roma itafunguliwa baada ya dada yake (Constantinople) kufunguliwa. Na koo takatifu zitapaaza sauti kwa kauli ya Mwenye Nguvu, Mwenye Utukufu:

وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وزهق الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقاً

“Na sema: Kweli imefika na uongo umetoweka; hakika uongo ni wenye kutoweka.” (Al-Israa [17]: 81)

Na dunia itajaa sauti za Takbira, na ardhi itang’ara kwa nuru ya Uislamu:

لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزّاً يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلّاً يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ

“Hakika jambo hili (Uislamu) litafika mahali ambapo usiku na mchana hufika. Na Allah hataacha nyumba ya udongo wala ya ngozi isipokuwa Allah ataingiza dini hii ndani yake, kwa utukufu wa mwenye kutukuzwa au kwa udhalili wa mwenye kudhalilishwa; utukufu ambao Allah atautukuza nao Uislamu na udhalili ambao Allah ataudhalilisha nao ukafiri.” (HR Ahmad kutoka kwa Tamim ad-Dari)

Tunatambua kuwa maadui wa Uislamu wataona utekelezaji wa hayo kuwa ni muhali, na watakariri kauli ya wenzao wa zamani kwa kejeli:

غَرَّ هَؤُلَاءِ دِينُهُمْ

“Dini yao imewahadaa hawa.” (Al-Anfal [8]: 49)

Lakini kama vile kauli hiyo ilivyokuwa maangamizi kwa walioisema, na Allah akaitukuza dini Yake na kuwanusuru watu Wake, basi vivyo hivyo leo hii itakuwa maangamizi kwao. Kwani Allah Mwenye Nguvu, Mwenye Hikima yupo pamoja na waja Wake wanaomtegemea, wenye ikhlasi Kwake (swt), na wakweli kwa Mtume Wake ﷺ, wanaofanya kazi kwa bidii na juhudi, bila nyoyo zao na viungo vyao kuachana na kauli Yake Ta’ala:

إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً

“Hakika Allah anatimiza amri Yake. Hakika Allah amekwishajaalia kila kitu na kipimo chake.” (At-Talaq [65]: 3)

Hawa, kwa kila siku inayopita, wanakaribia “kipimo” hiki.

وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

“Na Allah ni Mwenye kushinda katika jambo Lake, lakini watu wengi hawajui.” (Yusuf [12]: 21)

Wassalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh.

Jumamosi, 29 Rajab 1442 H
Sawia na 13 Machi 2021 M

Ndugu yenu,
Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah
Amiri wa Hizb ut Tahrir

Share Article

Share this article with your network